Mocumentary
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 765
- 1,954
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Vyama viwili kati ya 20 vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu ambavyo ni CCM na CHADEMA ndio vyenye sifa ya kupata wabunge wa viti maalum kwenye Bunge la 12.
Wakati NEC ikieleza hayo, jana Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alieleza kuwa mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 utaanza jijini Dodoma Jumanne ijayo, huku mambo matatu yakitawala katika vikao hivyo ikiwamo uchaguzi wa Spika wa naibu wake.
Idadi ya wabunge wa viti maalum hutokana na idadi ya kura za wabunge wote wa chama husika, ambapo chama kinatakiwa kupata asilimia tano ya kura zote halali za ubunge.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata kura za ubunge milioni 8.3m CHADEMA milioni 4.6 na CUF milioni 1.2. kutokana na kura hizo CCM ilipata viti 64, CHADEMA 36 na CUF 10.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Wilson Mahera hakuweza kutaja idadi ya wabunge hao na kutaka kiulizwe chama husika.
Chanzo: Mwananchi