Uchaguzi 2020 NEC: CHADEMA na CCM ndio vyenye sifa ya kupata Wabunge wa Viti Maalum kwenye Bunge la 12

bg2017

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
501
1,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Vyama viwili kati ya 20 vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu ambavyo ni CCM na CHADEMA ndio vyenye sifa ya kupata wabunge wa viti maalum kwenye Bunge la 12.

Wakati NEC ikieleza hayo, jana Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alieleza kuwa mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 utaanza jijini Dodoma Jumanne ijayo, huku mambo matatu yakitawala katika vikao hivyo ikiwamo uchaguzi wa Spika wa naibu wake.

Idadi ya wabunge wa viti maalum hutokana na idadi ya kura za wabunge wote wa chama husika, ambapo chama kinatakiwa kupata asilimia tano ya kura zote halali za ubunge.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata kura za ubunge milioni 8.3m CHADEMA milioni 4.6 na CUF milioni 1.2. kutokana na kura hizo CCM ilipata viti 64, CHADEMA 36 na CUF 10.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Wilson Mahera hakuweza kutaja idadi ya wabunge hao na kutaka kiulizwe chama husika.

Chanzo: Mwananchi
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
9,888
2,000
Mbowe ni mtu makini sana, hawezi acha izo nafasi kwa presha za mitandaoni. Kikubwa aombe kuonana na Rais ili kuweka mambo sawa kuondoa sintofahamu ya kwenye uchaguzi uliopita.
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
4,134
2,000
Mbowe ni mtu makini sana,awezi acha izo nafasi kwa presha za mitandaoni.kikubwa aombe kuonana na Rais ili kuweka mambo sawa kuondoa sintofahamu ya kwenye uchaguzi uliopita.
Maisha yanaenda kasi sana
1. Leo Mbowe ni mtu makini kwako?
2. Uchaguzi ulikuwa na sintofahamu?
3. Nani aombe kukutana na mwenzake? Mimi naona Magufuli afike pale Ufipa aombe kukutana na Mwenyekiti maana ameshikwa pabaya
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,564
2,000
Hivi nyinyi wehu CCM si mlikuwa mnataka mbaki peke yenu bungeni Mpaka mkadiriki na kuua watu ili mshinde vuti vyote, hebu endeleeni na bunge lenu humo kijani kibichi kitupu achaneni na Chadema sisi hatutaki ubunge wa kupewa barabarani. Endeleeni tu ndio faida hizo za ushindi wa kishindo wa damu za watu.
 

Brother Kaka

Member
Jun 11, 2013
77
125
Hatuwezi kuacha chama kikose ruzuku kwa sababu ya misimamo ya watu wachache. Kesho tutapeleka orodha ya wabunge wa viti maalumu ili waendelee kupigania na kutetea haki za wananchi Bungeni.

Mkumbuke kupitia hao wabunge ndio chama kinapata Ruzuku ya kujiendesha. Harakati zingine za kupigania haki ya uchaguzi uliopita bado zinaendelea..
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,943
2,000
Maamuzi magumu yanahitajika jumuia za kimataifa na wahisani pia iwabane vya kutosha uhuni huu usipite.
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,447
2,000
Maamuzi magumu yanahitajika jumuia za kimataifa na wahisani pia iwabane vya kutosha uhuni huu usipite.
Jumuiya za kimataifa tayari wametoa congratulatory notes kuutambua ushindi wa kimbunga nendeni bungeni acheni siasa nyepesi haxitawasaidia
 

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,081
2,000
Mbowe ni mtu makini sana, hawezi acha izo nafasi kwa presha za mitandaoni. Kikubwa aombe kuonana na Rais ili kuweka mambo sawa kuondoa sintofahamu ya kwenye uchaguzi uliopita.
Ndugai na Pombe wameshapata walichokihitaji na kukipigania sasa wanalia lia nini? Msimamo wetu ni ule ule kuwa hakukuwa na uchaguzi n hatutatoa ushirikiano wowote kwa hii serikali zaidi ya kuitakia mabaya popote pale ndani na nje ya Tanzania.
 

Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,423
2,000
Hatuwezi kuacha chama kikose ruzuku kwa sababu ya misimamo ya watu wachache. Kesho tutapeleka orodha ya wabunge wa viti maalumu ili waendelee kupigania na kutetea haki za wananchi Bungeni. Mkumbuke kupitia hao wabunge ndio chama kinapata Ruzuku ya kujiendesha. Harakati zingine za kupigania haki ya uchaguzi uliopita bado zinaendelea..
Soma sheria ya vyama vya Siasa. Ruzuku ya chama haitokani na idadi ya viti maalum bungeni.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,915
2,000
Mbowe ni mtu makini sana, hawezi acha izo nafasi kwa presha za mitandaoni. Kikubwa aombe kuonana na Rais ili kuweka mambo sawa kuondoa sintofahamu ya kwenye uchaguzi uliopita.
Kwa taarifa yako na wengine wenye kuwashwa, Mbowe Hana muda mchafu wa kufanya mjadala na yeyote kuhusu lolote! Yupo anajenga chama.

Hao NEC na CCM wanatosha kujiteua viti maalum! Wajichague wenyewe itapendeza kwani waliyataka! Mahera na jaji wake aibu hii mmeitaka!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom