NEC: CHADEMA inaweza kuchukua hatua ya haraka dhidi ya Daily News? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC: CHADEMA inaweza kuchukua hatua ya haraka dhidi ya Daily News?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dopas, Sep 24, 2010.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wadau wa JF nimeikuta hii katika gazeti la mwananchi leo.

  Makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisema kauli kwamba Dk Slaa hataingia Ikulu, inaumiza lakini ni juu ya Chadema na Dk Slaa kuamua kulalamika kama wataona imemwathiri.

  Jaji Makungu alisema Nec imesikia kauli hiyo lakini haiwezi kuifanyia kazi mpaka kuwe na mlalamikaji.

  "Sijalisoma hilo gazeti hilo lakini kauli hiyo inauma... inatakiwa walioumizwa walalamike. Wakikaa kimya, sisi hatuwezi kuchukua hatua. Kamati ya maadili ipo; Chadema au Dk Slaa akilalamika, tutawaita wanaolalamikiwa," alisema Jaji Makungu.

  "Tupo tayari kupokea malalamiko. Tuna kamati ya maadili, wakicomplain (wakilalamika), tutajadili na kutolea uamuzi."


  Ombi kwa uongozi wa Chadema ngazi ya taifa kuchukua ya haraka ili kuwaumbua hao mafisadi wa CCM. Msijali gharama mtakayotumia, wananchi na wapenzi wa Chadema tutachangia.

  Muhimu ni kuwa tunaingia Ikulu mwaka huu ili ukombozi wa kweli umfikie mtanzani aliyekata tamaa.
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yes ashitakiwe au atuambie kaona wapi kwamba Dr slaa kashindwa na kwa asilimia ngapi..?

  na kwa sababu ni gazeti la serikali , its obvious kuwa kuna mipango hiyo tayari..!
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani nyie mnaopiga kelele humu kuwa Dr. Slaa atashinda "mmeona wapi" kwamba kashinda na kwa asilimia ngapi.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  another defeat fear syndrome:
  1. Gazeti sijasoma kila ofisi ya serikali daily news included inapewa gazeti la daily news bure kwelimakamu mwenyekiti alishindwa kusoma Gazeti hilo na uona kama ni kweli au auongo????

  2. Kwa nini asimuambie mwandishi nitakupigia baadaye baada ya kulisoma gazeti?

  3. Kwa nini kuwe na mlalamikaji wakati mwenyewe kwa maneno yake anasema na kukiri kuwa inaumiza.

  Twahitaji sio tume ya uchaguzi bali tume huru ya uchaguzi hii sio huru kabisa unaweza kuona mwenendo wake wako ki CCM zaidi.
   
 5. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yaani kama mtu kavunja sheria ili achukuliwe hatua lazima mtu mwingine alalamike. Kweli hiyo ndiyo serikali yetu inayofuata utawala wa sheria.
  Hii inamaanisha kuwa hata kama nikiua mtu, kama familia yake au mtu yeyote hatalalamika basi nitaendelea kupeta uraiani. Please, let us be real.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sisi humu kusema hivyo ni okey, BUt government owned newspaper, that's is run by taxpayers' money? No way!
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nadhani sheria ndio inataka hivyo
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  so chadema hakuna kuijishauri hapo
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tofautisha kati ya kesi za madai na za jinai! Kesi za madai, kama hiyo Dkt Slaa vs Daily News, lazima Dkt Slaa alalamike, otherwise tunahesabu "volenti non fit injuria!"
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,200
  Trophy Points: 280
  Sioni sababu ya kushitaki kila jambo hiyo ni siasa watashitaki mangapi wao waendelee tu na kampeni afterall kampeni yao inakwenda vizuri kama vipi kampeni manager aitishe waandishi wa habari na wao waseme Kikwete hawezi kushinda simple.
   
 11. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Sina Hakika kama unajua maana halisi ya neno KELELE...Back to school soma than rudi utoe comments zako punjufu....Humu watu wanaandika kuhusu kushinda kwa Dr. Slaa kwa sababu wanaona ndo atawafaa kwa Maendeleo yao na Vizazi vyao...Mimi nilitembelea shule yangu ya Msingi mwaka huu, na nimekuta bado wanafunzi wanakaa chini....Hapa namaanisha Chini uijuayo wewe...ni vumbi full. Ni miaka zaidi ya Kumi tano bado hali ni ile ile......

  Bado JK alisema anawajua Mafisadi, wauza Madawa na walarushwa wakubwa. lakini hakuthubutu kuwataja wala hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa so far.....zaidi ya issue ya BOT ambayo marando aliiongelea siku ya Ufunguzi wa Kampeni za Chadema pale Jangwani mpk TBC (Chombo cha UMMA) kikata matangazo ili UMMA usisikie wala Kuona.....

  Jamaa (SLAA) amefichua issue kibao hata wewe shahidi.....swali ulishaona nchi gani zaidi ya TZ mwizi anaiba anaambiwa arudishe alichoiba then ndo inakua imetoka then inatuhubiria nchi inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria??? while mwizi wa Kuku anakamatwa na kupelekwa mahakamani na hatimae anafungwa?????

  THINK BRO....Najua unajua ukweli ila unakua unaleta comment zinazokera .....next tym dont comment kama huna cha msingi cha kucomment.....
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sure kaka...hapo ndo utajua kuwa bado tuna safari ndefu.......Sheria inabidi iwe kama computer....Kila mtu aijue kutokana na fani yake.....
   
 13. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani wewe unamatatizo ya kiakili, unahitaji kupimwa, mimi si shabiki kivileeeeeeeeeeee, ila kauli kama hiyo ya kusem FULANI HATASHINDA, huo ni uchochezi, kumbuka gazeti la serikali ni mamlaka iliyojitosheleza, lingekuwa la chama sawa, kama utakuwa huelewi sana kwa nini tunapiga kelele ajihuzuru au afukuzwe kazi angalia movie ya sometimes in april ya rwanda, uone kilichotokea!
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Sep 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole sana ndugu, kumbe ulisoma ukiwa unakaa chini?
   
 15. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Angalia kura za maoni kenye mitandao inayoendesha hizo kura. Endesha mchakato wako wa kura za maoni kitaalam halafu utuambie matokeo hapa. Nasisitiza neno kitalaam ili tuheshimu matokeo yako.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tafadhali Jaji Omar Makungu usitufanye wajinga. Hivi kazi ya NEC ni nini kama si kusimamia mwenendo na mchakato mzima wa uchaguzi na kuhakikisha kuwa maadili na sheria za uchaguzi zinaheshimiwa na hazikaukwi na mtu au chombo chochote. Je NEC kazi yake ni kusubiri hadi malalamiko yafikishwe kwake hata kama kuna ushahidi wa wazi kabisa kuwa kuna mtu, chombo au kikundi kimetenda kosa la jinai. Mpaka sasa NEC inasemaje kuhusu yafuatayo ?

  • Salma Kikwete kwa kutozingatia sheria na katiba ya nchi anatamba kuwa ana haki kutumia NGO ya Wama kumkampenia mumewe, kwa nini ?
  • Salma Kikwete anapokelewa na viongozi wa serikali na yadaiwa anataka apewe ripoti ya maendeleo ya wilaya/mkoa, kama nani ?
  • Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanatumia nyadhifa zao ndani ya serikali kuikampenia CCM wazi wazi na bila kificho, kwa nini ?
  • Vyombo vya dola na vyombo vya UMMA kama redio na TV mfano Daily News na TBC1 vyote vinaipendelea wazi wazi CCM, kwa nini ?
  • Dr. Bilal ambaye ni mgombea mwenza wa Uraisi wa CCM kwa sasa ana cheo gani mpaka anapokelewa kama kiongozi wa serikali, kwa nini ?
  • Ridhwani Kikwete katika harakati zake za kumfanyia kampeni baba yake anapokelewa na DC, RC pamoja na Kamanda wa Polisi, kwa nini ?
  • Jaji Omar Makungu kitendo cha Daily News hakimwathiri Dr. Slaa ama Chadema peke yao, kinaathiri mfumo mzima wa demokrasia na utawala wa sheria, haki na usawa.
  • Watanzania wote kwa ujumla wao wameumizwa na kuathirika na wengine tumebaki twajiuliza kwa nini tunapoteza mamilioni katika uchaguzi kama NEC ikishirikiana na serikali tayari mmeshapanga mshindi, ndiyo kwa nini ?
   
 17. J

  Jikombe Senior Member

  #17
  Sep 24, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa liko kwenye mfumo.bado inchi inaendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja kwenye madhabau ya mfumo wa vyama vingi.

  Gazeti la serikali bado lina feel kama ni mali ya chama kama vilvyo viwanja vingi vya michezo. Viwanja vilijengwa kwa pesa za walipa kodi (tena kwa kukamuliwa kwelikweli) lakina ccm ika viodhi.

  Hivyo hata pesa za EPA wali feel (na bado wana feel) ni sehemu ya mali za chama.
   
 18. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wewe unaweza kuwa kati ya watanzania wachache wazito wa kufikiri, jamii forum si chombo cha serikali hivyo si kosa kusema nani atashinda ila gazeti la daily news ni la serikali halipaswi kuwa na upande wa utetezi kwenye maswala ya uchaguzi/kampeni wanapaswa kuwa fair kwani wanaendesha shughuli zao kwa kodi za wananchi na sio michango ya wanachama
   
 19. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe hujui kuwa serikali inashikwa na chama na hatuna wagombea binafsi? Hujawahi kusikia kitu kama chama kilichokuwa madarakani?
   
 20. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shule nimeenda na wewe hauko kwenye nafasi ya mahubiri ya elimu.

  Kama "Humu watu wanaandika kuhusu kushinda kwa Dr. Slaa kwa sababu wanaona ndo atawafaa kwa Maendeleo yao na Vizazi vyao" basi na huyo Mhariri wa gazeti la serikali anaona vengine kwa maoni yake na ndiyo maana hayo yote yameandikwa kwenye column ya "Maoni ya Mhariri". Tatizo lako liko wapi? Au lazima kila mtu akubaliane na hayo mnayoyaandika na mnayoyaona kwa maoni yenu? Kwanini mtu asiwe na maoni tofauti na nyie?

  Wapi umesikia kuwa whistle blower ni sifa ya kuwa kiongozi mzuri?
   
Loading...