Elections 2010 NEC: Chadema acheni kauli za uchochezi

Naamini kuwa bado muda upo na masuala muhimu yatafuatiliwa.
CHADEMA anzeni kulinda kura kuanzia kwenye fikra zetu kwanza ili shughuli ya kuzilinda kwenye sanduku iwe rahisi
 
Naomba kutofautiana na NEC katika hili.

Hivi ni nani anayetoa kauli za uchochezi kati ya CCM na CHADEMA?
Nataka kwanza NEC waikemee CCM na serikali yake inapotumia vyombo vya dola kufanya UCHOCHEZI.

Juzi tumesikia kuhusu MHARIRI WA GAZETI LA DAILY NEWS(Serikali) akisema kuwa Dk. Wilbroad Slaa hatakuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tena akasisitiza kuwa hata vyombo vingine vya habari vinaweza KUMNUKUU HIVYO!!!
Baadaya tukasikia kuhusu WARAKA WA SIRI wa serikali(CCM) kwenda kwa wakuu wa mikoa,serikali na wanausalama KUFANYA KILA MBINU kuhakikisha CCM WANASHINDA!!!!

Haya ni matamshi gani kama siyo uchochezi huu???????????????
Huyu mhariri inaonekana anaandika kwa kujiamini kabisa kudhihirisha kuwa ametumwa na CCM(Serikali).

Je,hivi Watanzania kama wataamua kupitia ballot box kumpa Dk.Slaa kuwa Rais wao wa awamu ya 5 CCM au serikali ya CCM iliyopo madarakani kwa sasa watafanya nini??? Ni dhahiri kabisa kuwa watafanya kile kilichotokea pale Nairobi mwaka 2007. Hakika watafanya hivo na matokeo yake kila mtu anayayafahamu.

NEC wapo kwa ajili ya kutetea CCM na si vinginevyo.

Kama NEC wanataka uchaguzi ambao ni FREE AND FAIR waanze kuwadhibiti CCM kwanza vinginevo wao ndio watakuwa chanzo cha umwagikaji wa damu kwa mara ya pili Tanzania baada ya ule wa Visiwani mwaka 2005.NEC wakumbuke kuwa hatujasahau kile kilichotokea kule Zanzibar 2005 na chanzo ilikuwa ni haohao CCM.
 
NEC ni miongoni mwa jumuiya za CCM. wapo pale kwa kiapo cha boss wao na si kuutumikia umma.
 
Logic kwamba kama wangetaka makaratasi ya siri wangechapisha ndani ya nchi ni mbovu. Mbona kuna kipindi mitihani ilichapishwa Uingereza ili iwe ya siri?

Jaji Makame anajua kweli fall out itakayokuwepo kama Slaa akibidika KUMKATAA?
 
Nawashauri wale wanaotaka mageuzi ya kweli,dawa iliyobaki ni moja tu.Maana kwa nguvu hatunazo za kuwaondoa hawa jamaa,pesa hatuna,majini hatuna maana wao wanalindwa na majini.Dawa ni moja tu wanamageuzi tuingie nasi kwenye ulimwengu wa Roho tumwombe Mungu kupitia kwa Yesu tu,yote yatawezekana.Tuwape sapoti ya maombi hawa walio msitari wa mbele katika haya mapambano.
 
Alisema NEC imejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki huku akisisitiza kwamba, tumekuwa tukituma vijana wetu mara kwa mara kuangalia mchakato huo kwa kampuni husika.

NEC siyo wa kweli kabisa kwa sababu kama kweli wanataka uchaguzi uwe ni huru na wa haki wangelitushirikisha wapigakura katika kushuhudia hakuna mtu asiyehusika ambaye ataingia kwenye vyumba vya kuhesabia kura. Utaratibu huo upo wazi ya kuwa wapigakura tunaruhusiwa kuwa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura lakini NEC hiyo hiyo safari hii imesema tukipiga kura tuishie majumbani. Kuna nini kama siyo kuna mpango kamambe wa kuchakachua matokeo?

Ili NEC ilirudishe imani kwa wapigakura tunawashauri watushirikishe kwenye zoezi la kuhakikisha uchaguzi unakuwa ni wa huru na wa haki kama nilivyofafanua hapo awali.
 
Back
Top Bottom