NEC: Chadema acheni kauli za uchochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC: Chadema acheni kauli za uchochezi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 30, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  NEC: Chadema acheni kauli za uchochezi

  Na Ramadhan Semtawa


  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeionya Chadema kuacha kauli zake za kwamba, kuna njama za kuandaa karatasi za kupigakura za kuwezesha ushindi wa Rais Jakaya Kikwete, kwani zikiingia kwa watu wasioweza kuzichambua zinaweza kuleta hatari.

  Onyo hilo la NEC linakuja baada ya Chadema kutangaza hadharani kwamba, kitengo chake cha usalama kimebaini njama za kuwepo mpango wa kutengeneza karatasi nje ya nchi ambazo zitasaidia kuchakachua matokeo ili Kikwete awe rais.

  Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa NEC Jaji Lewis Makame, alisema tuhuma hizo ni za uongo na za kutungwa.

  Kwa mujibu wa Jaji Makame, kama kungekuwa na mpango kama huo NEC isingeweza kuamua kupeleka karatasi hizo nje ya nchi kwa ajili ya kuchapishwa kwa usalama zaidi.

  "Mimi nasema tuhuma hizo ni za uongo kwani hazina ukweli wowote. Hivi inawezaje kuingia akilini tukafanye mpango kama huo nje ya nchi, si tungeweza kuamua kufanya hapa kwetu?" alihoji Makame.

  Mwenyekiti huyo alifafanua kwamba, kauli kama hizo zinaweza kuwa na hatari kama zitaingia kwenye akili za watu wasiojua kuchambua mambo na kubaini mbivu na mbichi.

  "Sisi tutahakikisha Rais anayeshinda ni yule aliyechaguliwa na wananchi tu na si vinginevyo. Hatuwezi kukiuka matakwa ya wananchi," alisisitiza Jaji Makame.

  Makame alisisitiza kwamba, kilichofanyika katika kuipata kampuni hiyo iliyopewa zabuni ni kutangazwa zabuni ya wazi kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

  Jaji Makame alisema kampuni hiyo, iliyopewa dhamana ya kuandaa karatasi hizo, haikuchaguliwa na CCM wala Rais Kikwete.

  "Kampuni ilichaguliwa baada ya kufuatwa taratibu zote husika za zabuni, tulitangaza zabuni kwa mujibu wa sheria. Sasa kuanza kusema kuna mpango wa kuharibu matokeo kupitia ballot papers ni uongo mkubwa," alisisitiza.

  Alisema NEC imejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki huku akisisitiza kwamba, tumekuwa tukituma vijana wetu mara kwa mara kuangalia mchakato huo kwa kampuni husika.

  Jaji Makame aliweka bayana kwamba, hatua hiyo ya kutuma vijana wake mara kwa mara ni kuona kama kazi iliyopangwa kufanywa kwa mujibu wa zabuni, inatekelezwa.

  Alisema NEC ina dhamana na uchaguzi mkuu na kwamba mchakato mzima wa kuandaa karatasi za kupigiakura uko chini yao, hivyo kuhusisha taasisi nyingine ni hatari.

  Juzi Dk Slaa, akizungumza na waandishi wa habari pasipokutaja nchi yenyewe, alisema wanazo taarifa za siri kutoka kitengo chao cha usalama alichokiita makini, kimebaini mpango huo wa kuchezea kura kupitia karatasi hizo.

  My take:
  Kama kemeo hili ni mojawapo ya shughuli ya NEC mimi sina namna ya kulipinga. Lakini hapo hapo nashangaa kwa nini huyo huyo Lewis Makame anakuwa bubu kwa vifuatavyo;

  1.1. Hajakemea jinsi mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, na familia yake, wanavyotumia nyenzo za umma kama magari, ndege katika kampeni yake? Suala hili halina mjadala hata kidogo.

  2.2. Hajakemea vurugu za wafuasi wa CCM dhidi ya mikutano ya Chadema.

  3.3. Hajakemea kwa nini mgombea wa CCM Jakaya Kikwete anafanya mikutano baada ya muda unaoruhusiwa (eg huku mkoa wa Shinyanga juzi) na hafanywi lolote, huku wale wa vyama vya upinzani wakifanya hivyo huteremshwa majukwaani na polisi.

  4.4. Hajakemea tabia ya serikali ya ghafla kuwahamisha wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo katikati ya kampeni (eg Arusha mjini na Hai) bila ya yeye kushirikishwa. Hivi kweli Makame hakerwi au angalau kushitushwa na hilo? Anaweza kujidai hao ni wafanya kazi wa Tume yake?

  [FONT=&quot]....Wadau, madudu yake mengine mnaweza kuogezea hapa.....
  [/FONT]
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Swali kwa Makame

  Kuna Chama chochote au Mtu yeyote aliyelalamika kuumizwa ka Kauli hizo? Kama Hakuna mtu aliyelalamika nyinyi NEC kipi kinawawasha?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu:
  Nauliza- Kwa nini huyu Makame hataki kustaafu au kustaafishwa? Analazimishwa kuendelea kuongoza chaguzi zetu pamoja na kwamba kesha kuwa dead wood. Yote hii kwa sababu anawafaa sana CCM kuliko upinzani.

  Hatujasahau jinsi Tume yake ilivyomhujumu Mrema mwaka 1995 katika mkoa wa Dsm, ambayo ilikuwa ngome kubwa ya NCCR, pale kwa niaba ya mabwana zake CCM, na kwa makusudi mazima, alichelewesha kupeleka vifaa katika vituo vingi na kulifanya zoezi zima la upigaji kura katika mkoa wa Dsm kuvurugika na hivyo kurudiwa three weeks later.

  Tume yake iliweza kupeleka vifaa Tunduma, Ngara na Newala in time, like Ukonga, Kawe na Mbagala vilifika saa 9 alasiri. Hadi leo hajawajibu Watz kisawsawa kuhusu hujuma hiyo kubwa!!!!


  Asijidai hapa kuwa yeye ni independent, uongo huo. YEYE NI KADA MKUU WA CCM NA YUKO HAPO KWA MASILAHI YA CHAMA HICHO!!!!!!
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Have ever seen a dog biting his own master? Makame ni mteuliwa wa CCM hawezi kuipa kisogo!
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tendwa na Makame wote ni wale wale tu! Tangu lini mbwa akamng'ata anayempa chakula? Mbona hajakanusha kuhusu mashushu kupelekwa mikoani kuwatisha watu na serikali kuwaandikia barua wakuu wa mikoa na wilaya kuwataka waipe CCM ushindi kwa gharama yoyote? Huu uchaguzi una dalili nyingi tu za kuwa unfair.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  basi kumbe tunakazi kubwa duu kama ccm ikiingia tena madarakani sipati picha maisha yataendaje!!
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hayo kwenye nyekundu aape mbele ya mungu kuwa yanatoka moyoni na atatimiza hayo!!
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  If you stick a knife nine inches into my back and pull it out three inches, that is not progress. Even if you pull it all the way out, that is not progress. Progress is healing the wound. NEC BE FAIR
   
 9. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uzuri kama Makame amejibu, basi messege delivered! Tunatunza kumbukumbu yakitokea tutamhukumu kwa kauli yake
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  I like it
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  mbona wakati wa ile editorial kichechefu ya daily news walisema lazima kuwe na mlalamikaji, hii ya sasa mlalamikaji ni nani????????
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ndege, uko sahihi. kwenye tahariri ya Daily news walisema hawawezi kuchukua hatua (hata kalipio!) mpaka walioumizwa natahariri hiyo wapeleke malalamiko yao rasmi
   
 13. e

  emalau JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nilishawahi kuuliza hapa JF kwamba huyu makame alirudisha kadi ya CCM lini? Kingine inavyoonekana ni kwamba uchaguzi huenda ukaharibiwa na CCM kutokana na hii hamisha hamisha ya watumishi, viongozi wa vyama shindani wasilalamike tu hapa ndani, ni wakati wa kuieleza jamii ya kimataifa hususan ni wafadhili wakuu wa nchi hii kama Sweden na wengineo madudu yanayofanywa na CCM. Watu wa nje wanatusifia bila kujua mambo yanayoendelea chini chini. Nina imani mkwara wao unaweza ukasaidia in one way or the other.
   
 14. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani haya yote yaliisha kuwa reflected kwenye kauli mbio yao (CCM) ya " USHINDI NI LAZIMA" maana yake come rain come sun lazima JK aende ikulu hata kama ni on the expenses of our blood!
   
 15. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hakuna cha kuwambia wafadhili wala nini?Nchi hii ni yetu na hakuna mwenye hati miliki ya uongozi.Naona hii amani tuliyo nayo ni ya kinafiki,huwezi kusema una amani wakati unanyimwa haki yako,amani huanzia moyoni.Hapa mpaka tunyukane ndo kieleweke.
   
 16. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu unafikiri hawa wafadhili hawajui kinachoendelea hapa ndani! mimi naimani kabisa wanajua sana, si wana balozi zao hapa? mzuri ni kipindi kile cha sakata la EPA na Richmondna kufungiwa gazeti la Mwanahalisi, serikali ya Sweden kama nakumbuka ilitishia kusitisha misaada yake kama serikali haitachukua hatua stahiki. Imani yangu ni kuwa kwa namna moja ama nyingine hawa wafadhili nao wanafaidika kwa nchi hii ikiwa na uongozi dhaifu kama wa JK, si unajua ule msemo maafuru wa wana sheria " Quid pro quo" yaani " Nothing goes for nothing" sawa na msemo wa kiingereza" There is nothing like free lunch"!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I love this!!!!!
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Si unajuwa ni walewale, wanajiona wao na watoto wao npeke yao ndiyo wenye akili. Wengine wote mabwege!!!
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ukiona Makame anag'aka hivyo, tena bila kulalamikiwa rasmi kwake, basi kuna jambo. Nauliza: Hivi vyama vilielezwa mchakato mzima wa kuchapisha karatasi za kura pamoja na lay-out zake?

  To Mr makame: You and your team are stinkingly pro CCM. Dont deny this. You are silent over many wrongs being committed by your party.
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nisome ktk bold yako.
  Nina mashaka kwamba hawa wapinzani wana uroho wa madaraka ili waje kuwa kama ccm. maana kuna madudu kibao yanafanyika dhidi ya demokrasia nchini wanafunga midomo yao ilihali wao wapo kwenye position ya kuweza kuujulisha ulimwengu kinachoendelea.
  Nawasihi Ninyi CHADEMA et all kuwa msitufanye sisi wananchi kama carpets au daraja la kufikia malengo yenu ya kushika madaraka.
  Wengi humu nikiwemo mimi tumeshadeclare interest kuwa hatuna vyama ila tumeside na chama cha ukweli (CHADEMA) katika kampeni za sasa, tumeshatoa angalizo nyingi tu humu ambazo ni clue tosha kwa mwanasiasa makini kufuatilia na kuanza kuchukua hatua ili kunyoosha masuala.
  Kama leo mnafanyiwa rafu na CCM kabla ya uchaguzi halafu mnaishia kulalama majukwaani bila kuchukua hatua huku mkitoa onyo, fahamuni kwamba kura zikiibiwa sisi WATANZANIA hatuko tayari kumwaga damu zetu kwa uzembe wenu mnaoanza kuuonesha sasa. Chukueni hatua kwa kuuambia ukweli kwa jumuiya za kimataifa ili waikemee ccm. Au labda hamuwezi kufanya hivyo kwa sababu ninyi ni matawi ya CCM?

  Nawasihi muwe fair kwa WATANZANIA na si kwa vyama vyenu pekee. Wekeni maslahi ya Wantanzania mbele kwanza kisha maslahi ya vyama vyenu yafuatie.


  Kusitasita kwenu ndio kunaishia kukemewa na tume ya uchaguzi ambayo sisi wooote tunajua ipo pale kwa maslahi ya nani. Ijulisheni jumuia ya kimataifa na hao wanaomwaga pesa zao nchini (zinazochezewa na CCM) kuwa wajue hali ilivyo na waikemee serikali
   
Loading...