Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO ambaye amekuwa akitamba kwa muziki ya mahadhi laini, anatarajiwa kuwasili nchini Mei 19 kwa mwaliko wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jembe Media Limited.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 36 Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, anatarajiwa kufanya onyesho mei 21 jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba kwenye tamasha lililopewa jina la JEMBEKA NA VODACOM 2016.
Kwa mujibu wa waratibu wa Tamasha hilo, NE_YO pia anatarajiwa kushiriki kwenye shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi ya Vodacom.
Source: Channel ten