Ndyesumbilai Acha Fitna, JPM ana Gwiji wa Media za Electroniki Nchini

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
105
150
Na Dereck Mrusuri

Ndugu yangu Ndyesumbilai Frolian, habari ya siku kaka na rafiki yangu. Nimesoma makala yako kwa umakini mkubwa kuhusu JPM kusafisha nyumba yake.

Kuna usemi katika mchezo wa ndondi alipata kuutumia Chaplain wa Navy Command ya Marekani, ambae pia ni motivational speaker, Barry C. Black.

Alipata kusema, "all blows in the boxing ring are important but it is the LAST blow that really counts."

Ni ngumi ya mwisho inayoleta ushindi wa "knock out." Ninaamini ujumbe wako umeuficha mwisho, ulipoelezea kitengo cha mawasiliano cha Ikulu. Basi na mimi naomba nijikite hapo hapo.

Ndyesumbilai, sidhani kama umetumia vigezo sahihi kufananisha uwezo wa wasaidizi wa kitengo cha mawasiliano cha Ikulu enzi za JK na hawa wa Mh JPM. Ulinganifu wako si sahihi na sijui unalenga kupata nini hasa.

Kwanza Mkurugenzi hajateuliwa. Aliyepo ana kaimu, hivyo nachelea kumlinganisha na aliyeondoka. Maadam umeandika, basi itabidi tu nilizungumzie ili kutenda haki.

Kaka yako Salva Rweyemamu ambaye wewe Ndyesumbilahi unayemtetea, unampaka tope kwa hisia za watu kuwa amekutuma. Mi namfahamu ni mtu safi lakini hii makala yako inautia doa wasifu wake.

Siwezi kubisha kuwa Rweyemamu hakuwa mwandishi mzuri, la hasha. Lakini umahiri wake ulikuwa wapi? Alikuwa mzuri kwenye print na na spinning tu, hakuwa na weledi wowote katika televisheni.

Anayekaimu ni mahiri sana katika televisheni. Msigwa ameleta mapinduzi katika mawasiliano ya umma ya Ikulu kwa kutengeneza documentary za nguvu na yeye mwenyewe akiweka voice over.

Electronic media katika zama hizi ni "very effective" na hilo ndio eneo la Msigwa la kujidai. Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake bwana mpeni.

Utasababisha watu wadhani unatumiwa na watu wenye chuki ya wivu kwa maboresho makubwa na weledi katika kitengo cha mawasiliano cha Ikulu.

Kweli kaka yako Salva Rweyemamu alikuwa mzuri kwenye print media hata kama Press Release zilikuwa hazionyeshi uchambuzi wa kifikra lakini hakuwa na uzoefu wowote wa Television kama alivyo Msigwa. Hili halihitaji uende TSJ kulielewa.

Siku hizi Press Release zinatumwa haraka na zaidi ya mara mbili tena kwa njia nyingi hadi whatsapp.

Ni kazi tu. Unafikishiwa mkeka umekaa kitini newsroom, ukipiga simu inapokelewa fasta, hakuna chembe ya urasimu. Wewe Ndyesumbilai acha hizo kaka, Mwalimu Nyerere alituasa tuache hayo mambo unayoyafanya. Be professional.

Usiendelee kulitia doa gazeti lako la Mwananchi. Tunajua mlipolalia. Usiendelee ku "justify". Uchaguzi umekwisha. Sasa tujenge nchi. Majungu hayana nafasi, hapa ni kazi tu, we vipi kaka?

Jamani, kuna kosa gani picha ya Mhe Rais ikitumwa kwenye blog binafsi? Kwani hizo TV na Magazeti yote ni ya Serikali? Si ni ya binafsi pia. Sasa kosa liko wapi? Au ndio unataka kumchuna ngozi kiroboto. Tafuta lingine super tall, usije pinda mgongo kwa majungu.

Waandishi wengi siku hizi wanachukua habari na picha kwenye blogs. Wengine bila aibu hata credit hawatoi, sana sana wanaandika "Na Mpiga Picha wetu" juu ya picha (hahaha) yenye watermark ya Michuzi Blog! Aibu, na Mwananchi mnafanya hivyo sana.

Blogs ni source nyingine ya habari siku hizi. Toka huko newsroom upunge upepo uone mabadiliko ya tasnia. Jichanganye uandike vitu "relevant". Rweyemamu kakaako muda wake umekwisha ebo! Acha majungu.

Kitengo cha mawasiliano kina mpiga picha maarufu na makini, mwenye ubunifu mkubwa sana hapa nchini. Muhidin Issa Michuzi ni mahiri na picha zake ni high quality. Muache amtumikie Rais wetu. Mtu hadi anapiga picha za drones. Kwenye kampeni ya Dk Magufuli uliziona zile picha au macho yalikuwa wapi? Au kwa nini wahariri wanaacha picha za wapigapicha wao na kutumia za Ikulu. Ni ubora upi uusemao kaka.

Unapoongelea mgongano wa kimaslahi una maana gani. Michuzi blog ambayo inatamba duniani? Watu wanaona kazi za Rais kupitia blog ya Michuzi, tena ina staff wanaojitegemea? Au unataka Rais asionekane duniani kote? Unachekesha kaka. Kwani unataka wakachukue picha hizo MAELEZO? Unajua RV? Kama kuna effort binafsi, ndio tuivunje moyo ilhali wewe umekaa unahariri habari na kupika majungu? Acha watu wapige kazi.

Namaliza kwa ushauri. Mimi ni rafiki yako na nakuheshimu sana. Jifunze kuwa mzalendo na uangalie dunia kwa mtazamo chanya. Tuko katika zama za elektroniki. Najua wewe umejifunika na mabaki ya magazeti huko Tabata relini. Mjini huji. Dunia imebadilika. Usiendelee kujiaibisha hivi. Toka uone reporting ilivyobadilika Ndyesumbilai. Halafu, chapa kazi, acha majungu na fitna za kitoto.
COPIED
 
cbfb0eda-ceb4-49b4-bf0d-18d86ee1b1d2.jpg


Mchezo huu hautaki Hasira!
 
Ngoja niulize kidogo. Hivi mpiga picha mkuu wa ikulu uwa ni Fredy Maro au Michuzi?
 
Back
Top Bottom