Ndulane alibobea kwenye michezo Mwanyika alibobea kwenye Madini

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
CV ya Naibu Waziri wa Madini inakatisha tamaa kuona anapewa sehemu nyeti kiasi hiki.

Uwekezaji uliofanyika kwenye Madini unahitaji msimamizi mwenye business mind kama akina Mwanyika ambaye anaelewa michezo na sarakasi za mabeberu na makaburu au Kimei ambaye anaelewa maana ya sekta binafsi.

Kumchagua mwanamichezo ambaye amefanya kazi Halmashauri, amefanya kazi Tanroads na maeneo ambayo hayaendani kabisa na madini, TULIKOSEA.

Wizara za kitaalamu kwa kasi ya awamu ya tano ni Nishati, Fedha, Teknologia, Uwekezaji, Utalii na Madini. Haya maeneo yanahitaji kuteua wabunge kutoka nje ya waliopigiwa kura waje wayasimamie na si kumpa mtu hivihivi. Naamini haya maeneo hadi miaka mitano iishe watakuwa wametumbuliwa wote except uwekezaji ambapo amekaa mtaalamu na endapo atakataa kuendeshwa na upepo wa kisiasa.

Nadhani sasa Mwanyika akivaa viatu vya madini pamoja na madhaifu yake na tamaa zake, atajaribu kuendesha hii sekta.
 
Back
Top Bottom