Ndugulile: Magufuli hajui sheria, anakurupuka tu...

walipomzomea na yeye akawaambia piga mbizi, wamemwaga ugali kamwaga mboga.

lakini hadhi yake na wao hazilingani na kwa kuwa huo mkutano haukuwa rasmi hivyo wengi ya aliowakuta pale instant ni wachuuzi na mateja wanaokaa kule kwenye mawe. Huku ni kushusha hadhi yake kwani kichaa akibeba nguo zako mtoni nawe ukamfukuza ukiwa utupu basi hakutakuwa na mwenye tofauti hapo
 
shida yangu na hii nchi ni kuwaachia watu wasiokuwa na ufahamu kufanya maamuzi kwa kuwa tu wamepewa mamlaka.
Huyu Magufuli sababu zake anazozitoa kupandisha nauli etc hazina maana hata kidogo

Anasema kuwa Nauli ya chato ni sh 300, kw ahiyo na kigamboni walipe sh 200 etc.Hivi huyu kilaza hajui kitu kinaitwa economies of scale?hajui kuwa Kigamboni kuna high flow of traffic hence kwa kutumia resources zilezile kigamboni inaleta almost or more return on invested cash per every trip?anataka kutuaminisha kuwa kwa kuwa mtu anapanda teksi kariakoo hadi ubungo kwa 10,000 basi na wa daladala atoe hiyo hiyo?
Anataka kutuaminisha kuwa watu wa dar es salaam kwa kuwa kipato chao kiko juu basi walipie zaidi gharama ambazo hazina ulazima wa kulipia kwabei ya juu?kwa mantiki ya huyu magufuli gari ya toyota ingeuzwa bei rahisi tanzania kuliko japan kwa kuwa sisi ni masikini,na japan ni Matajiri.JE HII NDIO HALI HALISI?si kweli,wajapan na uchumi wao mkubwa wananunua magari mapya kwa gharama nafuuu kuliko sis tanzania,na sababu ni za kiuchumi sio za kisiasa au kijamii.
daladalal inauwezo wa kumpeleka mtu sehemu ile ile inayoenda teksi kwa gharama nafuu kwa sababu ya economies of scale na si vinginevyo.asilazimishe pantoni linalobeba watu 2000 litoze naulisawa na lile linalobeba watu 200.

Watu wanafikiria tatizo ni nauli kupanda kutoka 100 hadi 200 peke yake,hawafikirii kuhusu kupanda kwa nauli ya bajaji,mikokoteni etc,ambayo kutokana na ukichwa panzi wa huyu waziri wenu wabeba mikokoteni na waendesha bajaji,watalazimika kulipa zaidi ya gari ndogo aina ya salo.hivi ulishaona wapi?kwani sasa mikokoteni ni 1800,sgari ndogo ni 1500.sasa kama sio ujuha ni nini huu?

Hiki kinchi kinakera sana....,magufuli ndio mchapakazi,kiongozi wa mfano...,a person who can't even comprehend simplest issues in economics,that explains the sate we are in as a nation
 
magufuri big up kigamboni sio dar es salaam huyo mbunge mmoja muulize kwao kilombero kivuko shilingi ngapi?, alafu wanakigamboni wakome kutuegemea we miaka 14 nyento hii aibu wapige chiniiiiiiiii
 
Kuna kitu kimoja magufuli amefanya vizuri kabisa katika hii saga: ameonyesha msimamo, hakukubali kuyumbishwa na kelele. Hii ndo inayotakiwa hasa dhidi ya uhuni wa wabunge wanaojidai kutetea maslahi ya wananchi kwa upande mmoja, huku upande mwingine wanauma na kupuliza kwa kujilimbikizia maposho ya ajabu bungeni.

Magufuri angeonyesha zaidi ubunifu kama kupitia wizara yake wangekuja na suluhisho dhidi ya ufisadi wa mapato ya kivukoni kabla hata ya kupandisha hizo bei. Hivi kwanini wasiweke mfumo wa kununua ticket za msimu? ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kutoa ticket pande zote za kuvuka. Sidhani kama hili lingetushinda kuendesha.
 
Kuhusu guta, naona si haki.
Ila nauli ya 200 sioni haja ya watu kulalamika... acheni siasa mbuzi kapigeni kazi.
 
Magufuri angeonyesha zaidi ubunifu kama kupitia wizara yake wangekuja na suluhisho dhidi ya ufisadi wa mapato ya kivukoni kabla hata ya kupandisha hizo bei. Hivi kwanini wasiweke mfumo wa kununua ticket za msimu? ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kutoa ticket pande zote za kuvuka. Sidhani kama hili lingetushinda kuendesha.
Hizo zingechapishwa mitaani na kama huna watu wanaojiheshimu, mtaa mzima wange share ticket moja kwa kupokezana.
Tulipe 200, ndiyo maisha yalivyo.
 
Back
Top Bottom