Ndugu zetu zaidi ya 400 wamekwama India na wanapigana kuja Tanzania wamekwama

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Please Serikali iwasaidie ndugu zetu zaidi ya 400 waliokwama India wanataka kuja nyumbani.

Ubalozi wa India utoe ushirikiano wa kutosa watu mpaka wanalia hali ngumu walipo wanaogopa kwamba hawapo salama.

Wapo wanafunzi, wagonjwa walioenda kutibiwa, wafanyabiasha. Please Air Tanzania shughulikieni kibali shughulikieni ndugu zetu haya ndio majukumu yenu.

Kenya wameweza kuwachukua watu wao china.
 
Mbona unatoa taarifa nusu nusu, Je, wamekwenda Ubalozi wetu kuomba msaada?

Je, wanachohitaji ni nini sasa msaada wa kusafirishwa kwa sababu hawana pesa au wamekwama kutumia ticket zao kwa sababu hakuna usafiri? Je, wanawasiliana na nani hivi sasa?

Kama wanawasiliana na wewe waambie wawasiliane na Balozi wetu aliyepo India.
 
Wabaki huko mpaka korona iishe!

Mbona tuna roho zisizo na utu na ukatili kwa raia wetu?

nchi zilizopiga hatua, raia wao ana thamani kubwa sana kuliko fedha yeyote. kwao kutuma ndege kumfuata raia wao hata mmoja aliekwama popote duniani siyo shida..

kama tuliweza kuruhusu wachina kuingia nchini kwa kigezo cha utalii ili kuongeza mapato, shida ikowapi kwa raia wetu kuruhusiwa kurudi ama kufuatwa?

Corona tayar ilishaingia nchini, na hatujawahi kufunga mipaka ili kuizuia, hofu yetu ni nini endapo wakija?

kama ishu ni gharama, sidhani kama watashindwa kulipia ticket kwa gharama ya ndege kutoka dar kuwafuata, na kuwatoa huko kuja dar. (to and fro)
 
Watu wamekwama kila kona ya dunia sio India tu
Wengine 6 raia tofauti walikutwa wamelala kwenye pango baada ya kutoka kwenye Hotel walizokuwa wanaishi
Walikaa pangoni kwa siku 26
Kweli ni mitihani imewakuta watu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Please Serikali iwasaidie ndugu zetu zaidi ya 400 waliokwama India wanataka kuja nyumbani.

Ubalozi wa India utoe ushirikiano wa kutosa watu mpaka wanalia hali ngumu walipo wanaogopa kwamba hawapo salama.

Wapo wanafunzi, wagonjwa walioenda kutibiwa, wafanyabiasha. Please Air Tanzania shughulikieni kibali shughulikieni ndugu zetu haya ndio majukumu yenu.

Kenya wameweza kuwachukua watu wao china.

Hekima muhimu kutumika.
 
Mbona unatoa taarifa nusu nusu, Je, wamekwenda Ubalozi wetu kuomba msaada?

Je, wanachohitaji ni nini sasa msaada wa kusafirishwa kwa sababu hawana pesa au wamekwama kutumia ticket zao kwa sababu hakuna usafiri? Je, wanawasiliana na nani hivi sasa?

Kama wanawasiliana na wewe waambie wawasiliane na Balozi wetu aliyepo India.
Kwani ubalozi haujui watanzania wapo huko?

Wizara ya mambo ya nje wana kumbukumbu zozote?
 
Dada @wangarimaathai nakuona kwenye emoji comment za watanzania zinavo kuvunja mbavu
 
Back
Top Bottom