KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,896
- 36,213
Habari za muda huu ndugu na jamaa.
Nina masikitiko yangu kuhusu hawa ndugu zetu wanaoendesha magari bila ya kujali kuwa ni ya kwao au ni ya ofisini.
Hawa ndugu zetu wanaoendesha hivyo vyombo vya moto vyenye miguu minne wanakuwa wanajisahau sana kuhusu usalama wa wengine hasa sisi watembea kwa miguu, ni ukweli kuwa barabara zetu nyingi hapa mjini sio za kuridhisha lakini ninachowashangaa ndugu zetu hawa ni kulithamini gari lake kuliko hata mwili wa binaadamu mwenzake.
Yaani mtu anaona bora alikwepe shimo ili gari lake lisije kupata hitirafu na kukufuata kukuvunja mguu, kweli kabisa yaani ni kheri uvunjike mfupa wangu au kiuno changu kuliko wewe kuvunjika kwa spring zako?
Ubinaadamu umeenda wapi ndugu zangu? Tangu lini thamani ya mwanadamu ikalingana na ya gari kwa kuwa wewe tu gari ni ya thamani, utu kwanza ndugu zangu hivyo vyombo vya moto havina muamana.
Ni mara ngapi mnapata hitirafu na sisi waenda kwa miguu mnaotuona takataka tunawasaidia ni mara ngapi mnapata ajali na sisi waungwana waenda kwa miguu tunawasaidia huduma za kwanza mali zisitutoe utu binadamu wote ni sawa.
NB; Nimeyaandika haya baada ya kukumbana na matukio mengi huko barabarani ikiwemo leo asubuhi gari moja iliponisukuma mtaroni baada ya dereva kujaribu kulikwepa shimo lililopo mbele yake lakini namshukuru Mungu kwa neema zake sikuumia popote.
Na tukio lingine ni la gari moja aina v8 kunimwagia maji machafu mwili mzima baada ya yule dereva kujaribu kulikwepa shimo ambapo nililazimika kurudi nyumbani kubadilisha nguo.