Ndugu zangu yamenikuta, nina tatizo kubwa la low sperm kiasi cha milioni nane

Negrodemus

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
2,310
2,000
Ni matumaini yangu muwa wazima wa afya.moja kwa moja naingia kwenye mada.Ilikuwa juzi tuilitoka kumwona dr.kwa mambo ya kupima uzazi ikaja kubainika nina tatizo kubwa la low sperm kiasi cha milioni nane .naombeni msaada wenu kama kuna dawa litakalotibu hili tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Piga mbegu za maboga au unga wake chukua mlonge mdarasini na asali mbichi changanya kunywa then uje utoe majibu yako. pia tende na maziwa ya mbuzi unaloweka unakula siku inayofuata huna haja ya koroga kingine acha kula chips gonga dona

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Adjoub Adjoub

Member
Sep 11, 2017
81
125
Ni matumaini yangu muwa wazima wa afya.moja kwa moja naingia kwenye mada.Ilikuwa juzi tuilitoka kumwona dr.kwa mambo ya kupima uzazi ikaja kubainika nina tatizo kubwa la low sperm kiasi cha milioni nane .naombeni msaada wenu kama kuna dawa litakalotibu hili tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana mdau mwenzangu hapa JF, usipanic. Nina ushuhuda juu ya hilo. Calm down kijana. Mwaka 2013nilikwenda kupima kiwango changu cha sperms baada ya kukaa ndani ya ndoa kwa mwaka 1 takribani. Sperms count yangu was too low kiasi cha kunifanya nijione si lolote. Nikaandikiwa referal Muhimbili ili nihidhurie kliniki maalumu ya uzazi. Kwa upande wa mwenzangu yeye alikuwa hana tatizo kila wakipima. Nikawa najiona mkosefu kwenye ndoa. Familia ikaanza maneno na vijembe kiwa sina lolote miaka inakwenda sina hata
Wa kusingiziwa. Sikuweza kuanza kliniki kwa kuwa sikuwa na muda wa kutosha sana, nilikuwa
chuo. Nikaachana na wazo la kupata dawa maalumu z kunifanya niongeze sperms. Nikajiuliza nina tatizo gani ilhali sijawahi kufanya jambo la kunipelekea sperms zangu ziwe low sana? 2 years later nikaenda tena pale pale kupima. Nikaambiwa bado zipo low na sasa tatizo limeongezeka kwamba speems hazina mikia kabisa. Sikutishika na wala sikutaka dawa. Nikaanza kufuatilia vyakula ninavyokula kila siku, nikagundua ninapenda sana take aways foods. Soda, Chips, Sousages etc. Nikaacha kabisa. Nikaanza kula vyakula vya kawaida tu michemsho, chukuchuku foods, viazi etc. Few months baadae nikaenda tena kupima, sperms zilikuwa nyingi mpaka nikaogopa. Sikuamini. Now, I am a father of two heathy kids. Bila hata kumeza kidonge kimoja cha kuongeza SC. So, usipanic bali jiangalie namna unavyokula na ikibidi anza sasa kula vyakula vya kiasili ili ufanikiwe kwenye hilo
 

aminas

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
3,543
2,000
Karanga mbichi mkuu, maharage mengi, samaki wabichi tafuna na carroti sana.

Alafu pia kuna mzizi mmoja wa kimaasai unaitwa "Ngororiii" unautafuna utakusaidia sana kwenye show zako yaani hadi wife ataniletea zawadi kwa kukujulisha kuhusu hii kitu.
mjr95
 

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
2,000
ulipokuwa hapo hospitali huyo dokta alipaswa akupe ushauri wa kitaalamu kuhususiana na tatizo lako la low sperm count (oligospermia)..
na ili kuweza kupata matibabu ya tatio lako, kuna baadhi ya mambo yanatakiwa uyaweke wazi ili kuweza kupewa matibabu yaliyosahihi.
yawezekana ulikuwa una matatizo ya tezi za uzazi(testicles) hapo nyuma au lifestyle yako ya sasa hivi imepelekea lupata tatizo hilo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom