Elections 2010 Ndugu zangu watz: Msiweke matumaini makubwa ktk mabadiliko!!

meddie

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
432
250
Ndugu zangu Watanzania, baada ya kumalizika kwa shughuli za uchaguzi mkuu kundi kubwa la watanzania wanamshukuru Mungu kwamba uchaguzi umemalizika kwa amani na Tanzania inaendelea kuwa kisiwa cha amani.
Kutokana na sababu mbalimbali swala la amani kwa wengi ndo linakuwa mwanzo na mwisho lakini kwa wengine wanaenda hatua zaidi wakitarajia mabadiliko (maboresho) serikalini ktk uendeshaji, usimamizi, uwajibikaji, uadilifu na ugawaji sawa wa raslimali.


Wakati tukiendelea kusubili kuundwa kwa serikali mpya napenda kutaadhalisha hasa kundi hili la pili kwamba matarajio yao wasiyaweke juu sana kutokana na sababu zifuatazo:

· Watu ambao tuliwaona na kuwatuhumu kwamba wanatuhujumu/ wanakwamisha maendeleo yetu na ambao wanahata kesi, Raisi wetu aliwaita wachapakazi na upo uwezekano wa wao kupewa nafasi za juu serikalini
· Wakati wa kampeni raisi wetu aliulizwa swali kuhusiana na taswira ya serikali yake itakavyokuwa….nakumbuka hakuonyesha kuwepo kwa mabadiliko makubwa ktk muundo wa serikali yake!!!
· Watuhumiwa wa ufisadi wanasafishwa mmoja mmoja kupitia chombo chetu cha kusimamia corruption na kupata ujasiri wa kuwania usipika wa bunge.


(Masikitiko yangu ni waletuliowaona kuwa msaada na watetezi wa watz, sasa wanaitwa waongo,wazushi na watu wasiojua wajibu wao…namanisha 6)

 

Mountainmover

Member
Nov 9, 2010
45
95
Unaweza kuudanganya Umma mara moja lakini huwezi kuudanganya Umma siku zote.. Mwanzoni tuliamini kila alilosema mwinyimkuu ila sasa tunatafakari maneno yake na tunachukua hatua. Yeye kama aliwaona mafisi ni wasafi ni yeye, sisi hatudanganyiki!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom