Kazimzubwee
Member
- Nov 7, 2016
- 51
- 57
Amani iwe nanyi, Tanzania tulipata uhuru kutoka kwa Mwingereza na tangu uhuru mpaka leo naandika hapa tupo chini ya utawala Wa CCM chini ya mfumo wa vyama vingi kuanzia 1992 kwa mwongozo wa katiba yetu ya mwaka 1977 na marekebisho ya mara kwa mara(viraka). Sina nia ya kuwasimanga CCM,maana wote ni mashahidi mambo ya hovyo nchi, iwe rushwa, ujangili wa kutisha, ufisadi, utakatishaji pesa na kila wezi serikalini ulilelewa na utawala wa CCM katika awamu zilizopita. Nasema huu si wakati wa kutafuta mchawi wote tunamjua;kikubwa nasihi tumuunge mkono Rais Magufuli kwani ameonyesha kuchukizwa na uozo huo, ameonyesha uthubutu wa kukemea haya madhambi ana nia njema na anafaa kutuongoza,nchi ilifika pabaya. Tumpe muda Amiri jeshi wetu aweke misingi ili kukomesha udhalimu huu, nawasihi tuvumilie tunapoenda si mbali chini ya Mh Magufuli tutafika tumtangulize muumba.