Ndugu zangu wakulima tukumbuke kuweka akiba ya chakula

baraker88

Senior Member
Feb 26, 2014
124
147
Habari JF,

Wakulima nao waongelea hapa, ni wale ndugu zangu wanaotegemea kilimo cha jembe la mkono ambao ni wengi kuliko wale wanaofanya kilimo cha kisasa.

Pamoja na kuwa na mahitaji mengine yanayolazimisha kuuza akiba ya chakula ili uweze kupeleka watoto shule, mahitaji ya matibabu nk, bado kuna uhitaji mkubwa sana wa kuwa na akiba ya chakula.

Mfano kwa wakulima wa mahindi, bei iliyoachwa sokoni kwa sasa haiwanufaishi wananchi waliohusika kwenye kilimo kwa kuwa kwa sasa mazao mengi yapo mikononi kwa wafanyabiashara.

Hivyo bei ya mahindi iliyopo sokoni kwa sasa inawarudia wakulima wenyewe.

Mkulima kumbuka kuweka akiba ya chakula kwa maisha yako ya sasa na ya baadae.
 
Back
Top Bottom