Ndugu zangu waislamu naomba kuelimishwa tofauti ya Mwezi wa Kidunia na mwezi wa Kitaifa ilhali kalenda ya kiislamu ni moja!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,898
141,836
Nimesikia kupitia Imaan tv kuwa mahakama ya juu nchini Saud Arabia imetangaza mwandamo wa mwezi na kwamba kesho ni sikukuu ya Idd.

Tena wamesisitiza kuwa kuna waislamu wengine watakula sikukuu ya Idd Jumatano kwa sababu wanausubiria mwezi wa kitaifa uandame hapo kesho kunako majaliwa.

Na mwisho wamesisitiza kuwa watakaosherehekea sikukuu kesho na wale wa jumatano wote wapo sahihi.
Hapo ndipo naomba kuelimishwa hizi tofauti za siku zinasababishwa na nini wakati kalenda ya kiislamu ni moja?

Nawatakia Eid Mubarak!
 
TATIZO WANALO VIONGOZI BAKWATA...WANATAKA KILE WALICHOPANGA WAO KISIBADILIKE...NA NDIO MKAMGANYIKO WANAOULETA...

KWA MFANO LEO MWEZI UMEONEKANA BAADHI YA SEHEMU TANZANIA LAKINI WAMEUPINGA WAZI...KWA KUHOFIA HESABU YAO YA MWEZI KUTIMIA SIKU 28 BADALA YA 29, WATAONEKANA WALIWAPOTEZA WATU WAZI WAZI WAKATI MWEZI UMEANZA KWA KUTAKA KUPINGANA NA AHLU SUNNA WAL JAMAA(SALAFY)...
 
Nimesikia kupitia Imaan tv kuwa mahakama ya juu nchini Saud Arabia imetangaza mwandamo wa mwezi na kwamba kesho ni sikukuu ya Idd.

Tena wamesisitiza kuwa kuna waislamu wengine watakula sikukuu ya Idd Jumatano kwa sababu wanausubiria mwezi wa kitaifa uandame hapo kesho kunako majaliwa.

Na mwisho wamesisitiza kuwa watakaosherehekea sikukuu kesho na wale wa jumatano wote wapo sahihi.
Hapo ndipo naomba kuelimishwa hizi tofauti za siku zinasababishwa na nini wakati kalenda ya kiislamu ni moja?

Nawatakia Eid Mubarak!
Ni kweli watu wanaosheherekea jumanne na wanaosheherekea jumatano wote wanakuwa sahihi kutokana na tofauti ya masaa (Time difference) ya sehemu mbali mbali duniani.wakati wewe unaamka wenzako wa sehemu nyingine wanalala au ndo mchana hivo haiwezekani ulimwengu mzima sikukuu ikawa moja,ukitaka ku test we amka bongo asubuhi saa moja alafu mpigie simu mtu wa USA au australia ndo utajua kuwa dunia duara.
Nategemea nimeeleweka kidogo.
 
Kwani Tanganyika na Saudi Arabia tunatofautiana masaa mengi?
 
Sababu ya muda kati ya Tanzania na nchi za Mashariki ya kama Saudia,Iraq nk haina mashiko. Kama Tanzania ni saa 11:35 alfajiri ya Jumanne,basi Saudia ni Jumanne ya Alfajiri,muda ukiwa ni saa 11:35,pia. Kwenye hili viongozi wetu wa dini wanatulisha tangopori. Mwezi ungekua unaonekana Newzealand,Australia au Queensland hapo kulikua na mashiko,kwani kuna tofauti kubwa ya masaa. Hii issue inakua treated unnecessarily.
 
Kwani Tanganyika na Saudi Arabia tunatofautiana masaa mengi?
Hakuna tofauti ya masaa! Hoja kuu ni sheria yenyewe iliyoanzisha kufunga na kufunga inatamka ' fungeni kwa kuuona mwezi na fungulieni kwa kuona mwezi' Sasa ni hiari yako ukitafsiri kuwa hata ukionekana Brazil wewe unakuhusu sawa, ukisubiri uuone mwenyewe sawa. Kuhusu calender "HAKUNA CALENDER MOJA KWA WAISLAM WOTE'
 
Tofauti ya masaa haibadili siku. Kama Idd ni Jumanne Marekani basi inatakiwa iwe Jumanne Tanzania. Mfano Idd katika baadhi ya nchi za kiislamu ni Jumanne na nyingine ni Jumatano na nchi hizi hazina tofauti ya masaa au kama ipo ni masaa machache sana.

Ni kweli watu wanaosheherekea jumanne na wanaosheherekea jumatano wote wanakuwa sahihi kutokana na tofauti ya masaa (Time difference) ya sehemu mbali mbali duniani.wakati wewe unaamka wenzako wa sehemu nyingine wanalala au ndo mchana hivo haiwezekani ulimwengu mzima sikukuu ikawa moja,ukitaka ku test we amka bongo asubuhi saa moja alafu mpigie simu mtu wa USA au australia ndo utajua kuwa dunia duara.
Nategemea nimeeleweka kidogo.
 
Hakuna tofauti ya masaa! Hoja kuu ni sheria yenyewe iliyoanzisha kufunga na kufunga inatamka ' fungeni kwa kuuona mwezi na fungulieni kwa kuona mwezi' Sasa ni hiari yako ukitafsiri kuwa hata ukionekana Brazil wewe unakuhusu sawa, ukisubiri uuone mwenyewe sawa. Kuhusu calender "HAKUNA CALENDER MOJA KWA WAISLAM WOTE'
Hapana umekosea kidogo, sio Kwa kuuona Bali Kwa kuoneka. Hii maana yake sio lazima muuone nyote, wengine watapewa habari Tu na waliouona na hii ilitokea hata wakati waa Mtume.
 
Hapana umekosea kidogo, sio Kwa kuuona Bali Kwa kuoneka. Hii maana yake sio lazima muuone nyote, wengine watapewa habari Tu na waliouona na hii ilitokea hata wakati waa Mtume.[/color]
Shukran, neno lililotumiwa ni 'kuuona' na tafsiri inajuzu iwe umeuona wewe au yeyote katika umma. So hakuna hatia yeyote kwenye swala hili. USHAHIDI WA MWISHO NI KUWA SAUDI HAWAKUBALI MWEZI USIPOONEKANA KWAO!
 
Tofauti ya masaa haibadili siku. Kama Idd ni Jumanne Marekani basi inatakiwa iwe Jumanne Tanzania. Mfano Idd katika baadhi ya nchi za kiislamu ni Jumanne na nyingine ni Jumatano na nchi hizi hazina tofauti ya masaa au kama ipo ni masaa machache sana.
 
Waislamu wanahesabu siku zao kwa kutumia mzunguko wa mwezi, mwezi muandamo hutofautiana kutoka sehemu na sehemu, wajuzi wa elimu ya falaki wanatambua hilo, hivyo tukija kwenye msingi wa kuanza na kumaliza kwa funga ndiyo tumeambiwa tufunge kwa kuuona mwezi na tufungue kwa kuuona mwezi kama kukiwa na mawingu ambayo hamtaweza kuuona mwezi basi kamilisheni siku 30, na katika kalenda ya kiislamu mwezi huwa una siku 29 au 30. Kuna wanvyuoni waliyoonea kuwa mwezi ukionekana sehemu yoyote duniani basi ufuatwe ni kwa ajili ya waislamu wote wawe wamoja katika ibada zao, hii inawezekana kutokana na teknolojia ya mawasiliano kukuwa, lakini kama kusingekuwepo na mawasiliano kama ya simu na TV au internet ingekuwa vigumu sana kupeana habari ya mwezi muandamo kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Na kuna wanavyuoni waliyokuwa na msimamo wa kila nchi wafuate muandamo wao wa mwezi kwa sababu ya kutofautiana kwa kundama kwa mwezi katika sehemu mbalimbali ya dunia na huu ndiyo msimamo wa Saudia na nchi nyingine kama Oman, Libya, Yemen n.k. hata Tanzania kupitia BAKWATA wanafuata msimamo huu. Hakuna ubaya kama nchi wafuate mwezi muandamo wa sehemu yao au wafuate mwezi muandamo wa kimataifa, lakini si vizuri katika nchi moja kuwe na makundi ya wenye kufuata mwezi wa kimataifa na wengine kifuata mwezi muandamo wa sehemu yao huko ni kuwachanganya watu wenye uelewa mdogo katika dini. Na hali hii tungeomba baraza kuu la waislamu Tanzania wachukue hatua za makusudi za kulitafutia jambo hili utatuzi kwa kuwashirikisha katika mazungumzo baina ya wanavyuoni wenye misimamo hii miwili ili waje na kauli moja kwa maslahi ya watanzania, na ikiwezekana wawaalike wanazuoni kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni ili waje kutusaidia katika jambo hili, na ingekuwa vizuri masheikh wa Saudia wangekuja kutoa mihadhara kuhusu jambo hili huenda tukapata muwafaka.
 
Back
Top Bottom