Ndugu zangu Waislamu msitutie aibu, matokeo mabaya chanzo sio serikali tujipime wenyewe

Kuilalamikia serikali kuhusu matokeo mabaya ya Mtihani wa Dini ya Kiislamu, na hata baada ya kupitiwa upya hayaonyeshi ubora wowote unaoridhisha, ni uvivu wa kufikiri ndugu zangu Waislamu. Kaeni chini muwe wenye fikra si kukurupuka na kulaumu kumbe maimamu hawafundishi yanayopaswa au basi hawana elimu inayotarajiwa, hivyo basi labda tunahitaji kuanza kuandaa walimu na kuwajengea upya uwezo. Je, mlitaka wawekewe alama nzuri hata kama wamefanya vibaya? Kwani zimekuwa shule za Wagalilaya wao huweka vema tu na kuonekana watoto wanafanya vema ikija mtihani wa taifa vituko. Kitabu chetu kitukufu cha Quran (القرآن الكريم) kinaeleza bayana jinsi gani tunavyopaswa kuzingatia Elimu Dunia na si tu Elimu ya Akhera na Imani ya Mwenyezi Mungu.

Hebu tukae chini tutafakari tusiilaumu serikali na kutaka njia ya mkato. Tujipime tujikosoe na tujipange kuwaandaa watoto wetu katika somo hili muhimu wa imani yao na maisha yao.

Pia mimi nina wazo kwa maimamu na Mashehe viongozi wangu, mnaonaje katika madrasa tukaingiza somo la kujifunza elimu dunia katika hatua za awali, na si Qur’an Tukufu tu pekee, ili basi wawe na tija na waweze kushindanq na watoto wengine wanapokuwa kwenye shule za kawaida na kuweza kuongoza na kushika hatamu katika nafasi muhimu serikalini na katika taasisi mbalimbali? Maaba upendeleo bila elimu na ujuzi wapi na wapi? Na mnaonaje tukaanza kampeni ya kujenga mahospitali yetu wenyewe kwa wingi, na mashule ya msingi na sekondari ya kisasa, na vyuo vya ufundi ili watoto wetu waweze kuwa na uwezo wa kushindana na wengnine na kuchukua hatamu badala ya kutegemea shule za wenzetu, na tukaweza kutoa Maimamu wazuri kabisa wenye elimu dunia na elimu bora ya Qur’an Tukufu.

Je mwajua huko dini ya Kiislamu ilikoanzia watoto wao huwapeleka hata Marekani na Ulaya kupata elimu na wana ujuzi mkubwa sana, na wameendelea sana wenzetu si tu kwa bahati, ila kwa elimu Dunia ambayo iko juu sna. Ukweli uko palepale, Elimu ya Qur’an Tukufu itatujengea imani, uadilifu na maisha masafi mbele ya Mwenyezi Mungu lakini woote tunaafiki pia utakapokosa elimu dunia, inakuwa taabu kwelikweli maana ufukara na dhiki vinakuwa sehemu ya maisha yako, huwezi pata ajira wewe, wala huna ujuzi wa kutosha wa jinsi dunia ya sasa inavyofanya mambo yake.

profesa,,,ni kweli hayo usemayo wala sikupingi hata kidogo,,,kwamba waislam na taasisi zetu pia ni chanzo cha matatizo hasa,mimi ni mwalim na nipo kwenye taasis za kiislam,taasisi zetu zinafanya kazi kiujanjaujanja tuuu,pamoja na kwamba matokeo yamebadilishwa bado wapo wanafunzi wangu wana F,so ina maana tatizo lipo kwao,ila kwa hili lililotokea NECTA ,bila kuangalia itikad za KIDINI necta wanapaswa kujiangalia UPYA,pale ndo kwenye base ya elimu tanzania
 
Kwa kuwa wamelalamika waislam basi imekuwa nongwa, tuangalie na anayelalamikiwa. Kuna mzazi aliuiliza imekuwaje mwanae amefaulu darasa la saba ilhali hajui kusoma wala kuandika? Ipo wapi hadhi ya Baraza la mitihani, hivi changamoto ya kuvuja mitihani wameimaliza au ndo inakolea? Kiukweli Baraza hili ni mzigo na linachangia matatizo.
Nikija kwa huyu popesa namtilia shaka juu ya ushauri wake hasa kwa kutojua takwimu halisi za jitihada za waislam katika kujitafutia maendeleo yao. Sasa kama kuna dosari mahala fulani basi wasiseme kwa kuwa wewe huoni jema lao? Badala ya kuandika nenda kachangie kwenye taasisi hizo uone kama hakuna atakayefaidika na huduma hizo.
Ila nakupongeza kwa kushambulia na kutuzindua tuongeze bidii
 
Mimi binafsi siamini kwamba kuna njama za dini moja kuikandamiza nyingine kimaendeleo hapa Tanzania. Kwanza, Sidhani kama kuna mshikamano rasmi wa wakristo wote dhidi ya dini nyingine. Madhehebu ya kikristo nayo yamegawanyika sana yakihusisha ushindani mkali wa vipengele vya kiimani. Inawezekana wakristo wana ile bahati tu ya kuwa wa kwanza kupata elimu dunia iliyoletwa na wakoloni kupitia taasisi za makanisa - wapo hata waislamu waliofaidika nayo. Hali hii unaweza kuiona pia katika maeneo ya kijiografia. Kule wamissionari walikojisimika zaidi kama uchagani, uhayani na unyakyusani, kiwango cha elimu na maendeleo kimekuwa juu kwa muda mrefu.

Tatizo kubwa la nchi yetu ni uongozi usiokuwa na uoni (vision) na utashi wa kuiendeleza jamii kwa dhati. Ukijumlisha hiyo pamoja na jamii ya waislam (na wengineo) kutokuwa na misingi mizuri ya kielimu toka mwanzo, tatizo linazidi kukua. Aidha, sijawahi kusikia vijana wa kikristo wakipewa misaada maalum ya elimu na serikali zaidi ya juhudi za wazazi na jamaa zao. Mbona wapo wakristo wengi tu waliokwama kielimu kwa sababu ya umasikini? Nimesikia Serikali ikidai kusaidia/kutoa upendeleo kwa kwa jamii kama za wamasai, wanawake n.k. Nako siamini kama kuna cha maana sana kilichofanyika.

Ukiondoa matatizo kama ilivyotokea NECTA ambayo naamini zaidi ni ya utendaji mbovu tu (incompetence), tulione tatizo kubwa zaidi katika utendaji mzima wa Serikali. Badala ya kupoteza muda kufikiri kuwa jamii ya kiislam iko nyuma kielimu kwa sababu ya ubaguzi na vilelelezo visivyo na maana kama "mfumo kristo", hebu tuibane serikali na viongozi wetu wachukue hatua za dhati kuimarisha elimu katika jamii zetu zote. Watu wakielimika si rahisi kuwahubiria hoja nyepesinyepesi wakazikubali tu.
 
ninachoelewa mimi wa kristo wanapigana vijembe baina yao kisa madhehebu yao au maslahi,na waislamu hali ndio hiyo hiyo.kudai haki zako kama unadhulumiwa ni haki yako ya msingi,jali taratibu zitakazo kufanikishia kupata haki zako,kuna jamaa mmoja mmiliki wa bar aliniambia rafiki ukija huu mwezi wa ramadhan nakosa nguvu kabisa,kwani mauzo hupungua kupita maelezo,nilipomuhoji kwa nini aliniambia waislamu wengi ndio walevi wakubwa,hiyo moja nyengine baadhi ya madoctor wa kikristo huwa wanaheshima kwa mgonjwa haswa wa kike kuliko ma doctor wengi walio waislamu"jina"uislamu si abdu llah au muhammad au abdu lhalim,uislamu ni vitendo,uislamu si kanzu nyeupe tu,uislamu ni kuuelewa kama allah alivyoushusha kwa mtume wake s.a.w,uislamu si ndevu refu tu kama maarifa ya nini kisawa sawa huna!
anasema allah subhanahu:""إن الله لا يغير ما بقوم حتى يغيروا ما بأنفسهم""
kwa kifupi hiyo aya inatuelekeza kuwa allah hato badilisha hali ya kundi"umma"wa kiislamu mpaka kwanza wazirekebishe nafsi zao,nini umuhimu wa kusema waislamu tanzania ni wengi kuliko wa kristo kama uislamu wenyewe hawaujui wala hawauthamini wala hawana ujasiri wa kusema mimi muislamu nafunga na swali na na jiepusha na makatazo yote ya allah kama necta ina matatizo sawa!lakini hiyo si sababu tosha kwa watoto wa kiislamu kufeli chunguzeni maadili yao wawapo shule na wawapo nyumbani,je kuna mazingiza mazuri ya watoto hao kuwa bora shuleni na kupasi,asilima 75% jibu mazingira ni machafu na yanawadidimiza wanafunzi na kuwasaidia kufeli.
sijui nimeeleweka,au kama vipi ni post ki france!!!
 
Kuilalamikia serikali kuhusu matokeo mabaya ya Mtihani wa Dini ya Kiislamu, na hata baada ya kupitiwa upya hayaonyeshi ubora wowote unaoridhisha, ni uvivu wa kufikiri ndugu zangu Waislamu. Kaeni chini muwe wenye fikra si kukurupuka na kulaumu kumbe maimamu hawafundishi yanayopaswa au basi hawana elimu inayotarajiwa, hivyo basi labda tunahitaji kuanza kuandaa walimu na kuwajengea upya uwezo. Je, mlitaka wawekewe alama nzuri hata kama wamefanya vibaya? Kwani zimekuwa shule za Wagalilaya wao huweka vema tu na kuonekana watoto wanafanya vema ikija mtihani wa taifa vituko. Kitabu chetu kitukufu cha Quran (?????? ??????) kinaeleza bayana jinsi gani tunavyopaswa kuzingatia Elimu Dunia na si tu Elimu ya Akhera na Imani ya Mwenyezi Mungu.

Hebu tukae chini tutafakari tusiilaumu serikali na kutaka njia ya mkato. Tujipime tujikosoe na tujipange kuwaandaa watoto wetu katika somo hili muhimu wa imani yao na maisha yao.

Pia mimi nina wazo kwa maimamu na Mashehe viongozi wangu, mnaonaje katika madrasa tukaingiza somo la kujifunza elimu dunia katika hatua za awali, na si Qur’an Tukufu tu pekee, ili basi wawe na tija na waweze kushindanq na watoto wengine wanapokuwa kwenye shule za kawaida na kuweza kuongoza na kushika hatamu katika nafasi muhimu serikalini na katika taasisi mbalimbali? Maaba upendeleo bila elimu na ujuzi wapi na wapi? Na mnaonaje tukaanza kampeni ya kujenga mahospitali yetu wenyewe kwa wingi, na mashule ya msingi na sekondari ya kisasa, na vyuo vya ufundi ili watoto wetu waweze kuwa na uwezo wa kushindana na wengnine na kuchukua hatamu badala ya kutegemea shule za wenzetu, na tukaweza kutoa Maimamu wazuri kabisa wenye elimu dunia na elimu bora ya Qur’an Tukufu.

Je mwajua huko dini ya Kiislamu ilikoanzia watoto wao huwapeleka hata Marekani na Ulaya kupata elimu na wana ujuzi mkubwa sana, na wameendelea sana wenzetu si tu kwa bahati, ila kwa elimu Dunia ambayo iko juu sna. Ukweli uko palepale, Elimu ya Qur’an Tukufu itatujengea imani, uadilifu na maisha masafi mbele ya Mwenyezi Mungu lakini woote tunaafiki pia utakapokosa elimu dunia, inakuwa taabu kwelikweli maana ufukara na dhiki vinakuwa sehemu ya maisha yako, huwezi pata ajira wewe, wala huna ujuzi wa kutosha wa jinsi dunia ya sasa inavyofanya mambo yake.

Wanafiki kuna sura nzima ndani ya Qur'an mmeshushiwa ! Wewe unatucheza shere tu !
 
Na mimi naomba nichangie hapa, hata baada ya serikali kukiri kukosea na kusahihisha tena matokeo, bado imeonekana failure kwa somo la Islamic knowledge, niulize pia kuna University gani hapa Tanzania ambayo inachukua wanafunzi waliofaulu somo la Dini (what i understand all Divinity/Bible knowledge and Islamic Knowlegde have not any credit for entering to the University).

Nami nianze na weye kidogo:

kwanza kabisa nakutajia vyuo hapa tanzania vinavyolitambua somo la dini kama somo la kuingilia university:

1. Muslims university of morogoro (MUM)

2. Zanzibar university- kipo tunguu unguja.

3. International university of africa, university college of education- chukwani zanzibar.

Ktk ngazi za kimataifa vipo vingi tu kikiwemo chuo kikongwe duniani yani al azhar-misri, vipo vyuo uturuki, saudia, uganda, malesia etc ambavyo vinatambua rasmi somo la dini ya kiislam ktk kujiunga na chuo.

Sasa nije ktk hoja yenyewe ya msingi.

Umesema hata baada ya kupitiwa upya matokeo bado somo la kiislam linaonesha failure hapo sina hakika lkn hata iwe ni kweli haitokua kama mwanzo.

Lkn pia ikumbukwe kua somo hili halina walimu mana walimu wa somo hili hawalipwi na serikali, kulingana na maisha yalivyo ni ngumu walimu kujitolea bure huku ukijua kua waislam ni maskin hawawez kujisomesha.

Wengine munasema eti familia nzima ya waislam haisomi tokea shule ya msingi wanatoroka. Ni sawa maana wao ndio wataftaji chakula wakenda shule wakirudi wale nini? Ni athar za mda mrefu za kufelishwa kwa wazee wao.

Mmoja hapo juu anasema eti wizara ya elimu imetoa ufafanuzi kuhusu kufelishwa kwa waislam. Ni ufafanuzi gani huo?

Wizara inasema eti tatizo ni kugawa kwa 3 badala ya 2 kulingana na idadi ya pepa.

Kama hilo ni kweli, je inawezekanaje mtu ambae mwanzo amepata F lkn baada ya malalamiko anapata A?

Km ishu ni kugawa kw 3 badala ya 2. Haiwezekan mtu ambae maksi zake baada ya kugawa kw 3 akapata F lkn eti baada ya kugawa kw 2 anapata A.
 
Kuilalamikia serikali kuhusu matokeo mabaya ya Mtihani wa Dini ya Kiislamu, na hata baada ya kupitiwa upya hayaonyeshi ubora wowote unaoridhisha, ni uvivu wa kufikiri ndugu zangu Waislamu. Kaeni chini muwe wenye fikra si kukurupuka na kulaumu kumbe maimamu hawafundishi yanayopaswa au basi hawana elimu inayotarajiwa, hivyo basi labda tunahitaji kuanza kuandaa walimu na kuwajengea upya uwezo. Je, mlitaka wawekewe alama nzuri hata kama wamefanya vibaya? Kwani zimekuwa shule za Wagalilaya wao huweka vema tu na kuonekana watoto wanafanya vema ikija mtihani wa taifa vituko. Kitabu chetu kitukufu cha Quran (?????? ??????) kinaeleza bayana jinsi gani tunavyopaswa kuzingatia Elimu Dunia na si tu Elimu ya Akhera na Imani ya Mwenyezi Mungu.

Hebu tukae chini tutafakari tusiilaumu serikali na kutaka njia ya mkato. Tujipime tujikosoe na tujipange kuwaandaa watoto wetu katika somo hili muhimu wa imani yao na maisha yao.

Pia mimi nina wazo kwa maimamu na Mashehe viongozi wangu, mnaonaje katika madrasa tukaingiza somo la kujifunza elimu dunia katika hatua za awali, na si Qur’an Tukufu tu pekee, ili basi wawe na tija na waweze kushindanq na watoto wengine wanapokuwa kwenye shule za kawaida na kuweza kuongoza na kushika hatamu katika nafasi muhimu serikalini na katika taasisi mbalimbali? Maaba upendeleo bila elimu na ujuzi wapi na wapi? Na mnaonaje tukaanza kampeni ya kujenga mahospitali yetu wenyewe kwa wingi, na mashule ya msingi na sekondari ya kisasa, na vyuo vya ufundi ili watoto wetu waweze kuwa na uwezo wa kushindana na wengnine na kuchukua hatamu badala ya kutegemea shule za wenzetu, na tukaweza kutoa Maimamu wazuri kabisa wenye elimu dunia na elimu bora ya Qur’an Tukufu.

Je mwajua huko dini ya Kiislamu ilikoanzia watoto wao huwapeleka hata Marekani na Ulaya kupata elimu na wana ujuzi mkubwa sana, na wameendelea sana wenzetu si tu kwa bahati, ila kwa elimu Dunia ambayo iko juu sna. Ukweli uko palepale, Elimu ya Qur’an Tukufu itatujengea imani, uadilifu na maisha masafi mbele ya Mwenyezi Mungu lakini woote tunaafiki pia utakapokosa elimu dunia, inakuwa taabu kwelikweli maana ufukara na dhiki vinakuwa sehemu ya maisha yako, huwezi pata ajira wewe, wala huna ujuzi wa kutosha wa jinsi dunia ya sasa inavyofanya mambo yake.

Wanafiki kuna sura nzima ndani ya Qur'an mmeshushiwa ! Wewe unatucheza shere tu !
 
Umesema mambo ya msingi sana Proffesor. lakini nani atakuelewa wewe unaewaambia mambo ya msingi? wanafundishwa na Mashehe namna ya kulalamika bila kuchukua hatua wakati wenzao wako busy kujenga Vyuo vikuu. wao wamshukuru mkapa kuwapa majengo ya Tanesco Moro, vinginevyo pasingekua na chuo kikuu kinachomilikiwa na taasisi ya kiislam.
 
Back
Top Bottom