Ndugu zangu Waislamu msitutie aibu, matokeo mabaya chanzo sio serikali tujipime wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu zangu Waislamu msitutie aibu, matokeo mabaya chanzo sio serikali tujipime wenyewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Profesa, Jun 10, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kuilalamikia serikali kuhusu matokeo mabaya ya Mtihani wa Dini ya Kiislamu, na hata baada ya kupitiwa upya hayaonyeshi ubora wowote unaoridhisha, ni uvivu wa kufikiri ndugu zangu Waislamu. Kaeni chini muwe wenye fikra si kukurupuka na kulaumu kumbe maimamu hawafundishi yanayopaswa au basi hawana elimu inayotarajiwa, hivyo basi labda tunahitaji kuanza kuandaa walimu na kuwajengea upya uwezo. Je, mlitaka wawekewe alama nzuri hata kama wamefanya vibaya? Kwani zimekuwa shule za Wagalilaya wao huweka vema tu na kuonekana watoto wanafanya vema ikija mtihani wa taifa vituko. Kitabu chetu kitukufu cha Quran (القرآن الكريم) kinaeleza bayana jinsi gani tunavyopaswa kuzingatia Elimu Dunia na si tu Elimu ya Akhera na Imani ya Mwenyezi Mungu.

  Hebu tukae chini tutafakari tusiilaumu serikali na kutaka njia ya mkato. Tujipime tujikosoe na tujipange kuwaandaa watoto wetu katika somo hili muhimu wa imani yao na maisha yao.

  Pia mimi nina wazo kwa maimamu na Mashehe viongozi wangu, mnaonaje katika madrasa tukaingiza somo la kujifunza elimu dunia katika hatua za awali, na si Qur’an Tukufu tu pekee, ili basi wawe na tija na waweze kushindanq na watoto wengine wanapokuwa kwenye shule za kawaida na kuweza kuongoza na kushika hatamu katika nafasi muhimu serikalini na katika taasisi mbalimbali? Maaba upendeleo bila elimu na ujuzi wapi na wapi? Na mnaonaje tukaanza kampeni ya kujenga mahospitali yetu wenyewe kwa wingi, na mashule ya msingi na sekondari ya kisasa, na vyuo vya ufundi ili watoto wetu waweze kuwa na uwezo wa kushindana na wengnine na kuchukua hatamu badala ya kutegemea shule za wenzetu, na tukaweza kutoa Maimamu wazuri kabisa wenye elimu dunia na elimu bora ya Qur’an Tukufu.

  Je mwajua huko dini ya Kiislamu ilikoanzia watoto wao huwapeleka hata Marekani na Ulaya kupata elimu na wana ujuzi mkubwa sana, na wameendelea sana wenzetu si tu kwa bahati, ila kwa elimu Dunia ambayo iko juu sna. Ukweli uko palepale, Elimu ya Qur’an Tukufu itatujengea imani, uadilifu na maisha masafi mbele ya Mwenyezi Mungu lakini woote tunaafiki pia utakapokosa elimu dunia, inakuwa taabu kwelikweli maana ufukara na dhiki vinakuwa sehemu ya maisha yako, huwezi pata ajira wewe, wala huna ujuzi wa kutosha wa jinsi dunia ya sasa inavyofanya mambo yake.
   
 2. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbona serikali imekiri kuwepo kwa tatizo? au nao ni wavivu wa kufikiri?....tafadhali usituongezee hasira tulizo nazo
  Madrassa zinafundisha watoto baada ya kutoka kujifunza elimu dunia mashuleni! vipi uwepo wa Madrassa unakukera nini?
  Kuongoza na kushika hatamu mbalimbali serikalini kunahitaji elimu, kitu ambacho Waislamu wananyimwa.......angalia sakata la mitihani linaloendelea, serkali na baraza la mitihani wamekiri kuwepo na "makosa" katika kuwafaulisha (si usahihishaji) wanafunzi
  Tutajenga vipi mashule ya kisasa, vyuo vya ufundi na mahospitali wakati tumetiwa umasikini (matokeo ya kukoseshwa elimu) kiasi cha kuwa hata nyumba zetu wenyewe kwenye miji yetu wenyewe inabidi tuziuze kwa wamisheni (Waliochukua nafasi zetu za masomo) ili tupate mlo wa kula tu!
  Upande wa pili tuna vijana wetu wa Kiislamu ndio wanaoongoza kwa utumiaji wa madawa ya kulevya, uwingi katika magereza, yote haya yanafuatia baada ya kukoseshwa elimu na kukatishwa tamaa kimfumo kuwa hata wakisoma hawatafauli.
  Na kama vile haitoshi baada ya yote hayo una mabohora (kama ni kweli wao ndio walioandika, rejea kwenye maoni yao kuhusu udini tz) nao hawako nyuma katika kuwabughudhi Waislam kwa kutuambia kuwa nafasi ndogo sana ya elimu tunazopewa na Serikali ni msaada kwetu ilhali hili ni wajibu wa serikali yoyote ile kwa raia wake wa aina yoyote ile!
  Hii ndio hali ambayo Waislamu tumefikia sasa! katika nchi yetu wenyewe!
   
 3. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hivi nawe muislamu?
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Katika hili hujawatendea haki ndugu zetu waislamu! Pamoja na kuwa ni ukweli kuwa matokeo bado si mazuri sana hata baada ya kutolewa upya lakini ukweli unabaki pale pale kuwa NECTA walikosea katika ukukokotoaji wa matokeo ya awali katika somo hilo. Na kwa kweli ukweli huu unaongeza mashaka kuhusu integrity ya systems zao kwa miaka mingine pia si kwa waislamu lakini hata kwa masomo mengine yasiyo ya kiislamu. Kwenye, ukaguzi wa mahesabu, kuna kitu kinaitwa "analytical review"...inaelekea suala hili huwa halifanyiki au anayepaswa kufanya alikuwa mvivu wa kufikiri na matokeo yake NECTA nzima inaweza kupoteza kuaminika kwake.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Sideeq,
  Do you think anachosema jamaa ni uongo? Hata kama umaskini upo, bila mikakati endelevu umaskini utaishaje? Kama wanyarwanda au waisraeli wangekuwa na attitude hiyo unafikiri wangefika walipo sasa hivi? Profesa anasema kweli kabisa. Think about what he says critically. Hakuna kitu kitakuja bila proper use of brain and planning.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135

  Kiukweli msipobadilisha hii attitude ya Kuonewa hamtokaa mfanye la maana wala kufika mbali...Haya ni mawazo mgando na nawashangaa sana waislamu wa Jf maana ni tofauti na waislamu wastaarabu, wanaojishughulisha na wenye upendo kwa dini zote ....wengi nimesoma nao kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu...wengine wafanyakazi wenza, wengine washirika katika mambo mbali mbali ya kijamii na biashara...ninapoingia humu JF nashangaa mawazo yanhayotolewa humu na naunga mkono hoja ya mmopjawapo wa wana JF alowahi kusema huenda kuna watu wanajisahili humuna wanajifanya waislamu kuuchafua uislamu...

  Hivi tunasemaje kuhusu waislamu waliosoma tena wengine weeengi tu kwenye shule za kikristu na wamepasua pepa sasa wana nafasi zao??


  Unaifahamu historia ya elimu katika nchi hii?? Tukiendelea na mawazo mgando kiasi hiki hatutokaa tuadress the real problem tutabaki kulalamika hata pasipokuwa na sababu...Shida iliyotokea NECTA imefafanuliwa vizuri na hatua zimeanza kuchukuliwa kikubwa wadau wa Elimu na walioathirika (Shule za Kiislamu) wameelewa ila ambao hayatuhusu moja kwa moja (waathirika wa matokeo ya kidato cha sita 2012 - islamic knowledge) sio wanaoandamana wala wazazi wao wala waalimu wao kwani wanajua walikuwa wakifanya pepa 3 na kuanzia mwaka jana wamefanya pepa mbili mfumo ama haukubadilishwa ku capture hizo pepa mbili ama haukurespond ulipobadilishwa then ukaculculate matokeo ya pepa 3...On top serekali imeshaunda tume itakayohusisha hata baraza la shule za kiislamu. Wahusika wameelewa lakini wasiojua au wasitaka hata kujua nini kilitokea ndo wamekuwa wasemaji wakuu...Techical fault zipo mahali pote...wangapi wanarukwa hata kwenye payroll?? mara ngapi hata benki wanakosea transaction zao??

  Eti NECTA tangu ianzishwe jakuna makatibu watendaji waislamu....ivi ndalichako alijiteua mwenyewe?? Kuna mmoja humu aliwahi kusema ndalichako aondolewe awekwe sheikh ponda....Yaani tumefikia mahali ambapo dini inatakiwa kuwa qualification katika uteuzi??
  Change of Attitude is desirable otherwise tutaishia kubaya.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  ngojea matusi
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Matusi will never deliver the results we would like to see...not in our life time. The only way to get the desire of our hearts is to pursue our way ways more objectively.
   
 9. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,384
  Likes Received: 6,563
  Trophy Points: 280
  aibu..
   
 10. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  @Mkuu Sideeq na Mkuu Nabihu

  Kuwa mbishi sana sio ndio kigezo cha uislamu bora. Sometimes you have to think positive. Ni kweli tatizo lilitokea, lkn je, dawa ni kukaa chini na kunung'unika mwaka mzima?

  NECTA na serikali walishatoa ufafanuzi ni kwa nini wastani ulishuka na kosa limeonekana kuwa ni uzembe ambao si jambo geni kwetu, ndio maana kuna mtu muhimbili alipasuliwa kichwa badala ya mguu, sasa manung'uniko yasiyoisha yana tija gani?

  Yaliyotokea juzi yasiwe kigezo cha kuhalalisha ujinga wa miaka yote. Mkuu Sideeq umekiri kuwa magerezani na kwenye vijiwe vya madawa ya kulevya kumejaa vijana wa kiislamu jambo ambalo ni kweli na umedai kuwa sbb ni kuwa walinyimwa elimu, jambo ambalo si kweli.

  Ukweli ni kwamba msingi wa maendeleo ya mwanafunzi hujengwa na wazazi nyumbani, mwalimu ni daraja. Hawa unaowasema vijiweni wengi wao hata darasa la 7 hawakumaliza, je elimu ya msingi nayo ilihitaji mamilioni?

  Nakupa mfano wa rafiki zangu wawili niliokuwa nao shule ya msingi. Shafii Anzuruni hatukumaliza naye, kwao wamezaliwa 9 na hamna hata mmoja alimaliza darasa la saba. Sasa hivi yupo makaburini pale Sinza anavuta bangi kwa hela anazopata akichimba makaburi. Mohammed Baruani tulimaliza naye STD IV, akasoma Kibasila, mimi nikasoma Makumira na tukakutana A Level Makumira. Sasa tunavyoongea yupo South Eastern University anachukua Masters ya BA. Kwao wapo watatu tu, yeye na dada zake wawili na baba yake ni (alikuwa) dereva wa Coca-cola, ilhal baba yake Shafii alikuwa karani wa mahakama huko Unguja.

  Lipo jambo la nyie kama waislamu kuliaddress kwa jamii yenu kuhusu elimu. Huu msingi mwarabu aliyewaletea dini yenu hakuwaachia kwa hiyo mlipaswa wenyewe mshituke na kuitafuta. Hakuna sehemu Mwarabu alijenga shule wala zahanati kwa hiyo liwekeni akilini hilo na ndio sbb mko nyuma.

  Suala hapa ni kupunguza kuzaa watoto msioweza kuwalea na ile mihadhara yenu mnayotumia kutukana wakristo kuwa hawajatahiriwa mngeitumia kukosoa jamii yenu ambayo kwa maoni yangu inahitaji ukarabati mkubwa. Unapooa wake wengi na kuzaa watoto kwa sbb nyepezi za kila mtoto anakuja na riziki yake matokeo ndio haya. La NECTA limeeleweka, tuangalia nyumbani kwenye familia

  Hongera Profesa, kutambua ubovu wa chombo ndio hatua muhimu katika kufanikisha matengenezo yake.
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwnini nyiunyi waisla mmekosa utulivu wa akili ,hekima na busara kupambanua na kusolve mambo yenu kwa akili na utashi kwni hao viongozi wenu ni watoto futaeni protocal andikeni barua ,waoneni wahusika macho kwa macho muwa hoji
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Umetumwa na nani?
   
 13. N

  Nafasi Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Na mimi naomba nichangie hapa, hata baada ya serikali kukiri kukosea na kusahihisha tena matokeo, bado imeonekana failure kwa somo la Islamic knowledge, niulize pia kuna University gani hapa Tanzania ambayo inachukua wanafunzi waliofaulu somo la Dini (what i understand all Divinity/Bible knowledge and Islamic Knowlegde have not any credit for entering to the University).
   
 14. a

  adolay JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Mkuu professor

  Hako kaidentity kanakufaa kabisa., bila ushabiki umehiti points.
  Umeonambali na umejadili mambo mazito kwa ufasaha, tunahitaji wachambuzi kama wewe, wenye mtizamo chanya na sio kulaum tu.

  Tatitizo likitambulika na kueleweka vema kinachofuata ni mikakati ya kupambana nalo. Kuweka malengo ya mda mfupi na muda mlefu, kukusanya resources kuunda mazingira ya kulitatua kwa ufanisi.

  Huwezi hata siku moja kutoka katika matatizo kwa kulalamika tuu bila kujua historia na mzizi wa tatizo. Kulalamika na kuishambulia serikali pasi nakuukubali ukweli ilikulishughulikia tatizo linalokusumbua, itakua hekaya za abunuasi au fisi na mkono wa mwanadamu kwamba utadondoka apate kitoweo ilihali kiuhalisia mkono upomahala pake na kamwe hautadondoka.

  Waislam waufuate ushauli wako hakika watashinda, ukiboresha elimu na afya ya waumini wako, imeikomboa jamii kwa ujumla wake na hizi propaganda za tunakandamizwa, tunaonewa, tunanyanyaswa, wakristu wanapendelewa, kunamfumo kristu nk vitaisha.

  waislamu wajipange na waweke mikakati ya makusudi ya kuelimisha kizazi cha leo na kesho, wakiukubali ukweli watafanikiwa wakindeleza habali za lawama bila kuenda kwenye rootcourse for sure the history is there to explain.
   
 15. E

  Etairo JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyo ndo anajiita profesa. kama ndo hivyo hatuna haja ya kuwa na profesa asiyeweza hata kufanya utafiti mdogo na kubaini ukweli wa dhuluma ya makusudi dhidi ya waislam. Mchezo mchafu ulianza tangu enzi-rejea kitabu cha padri john sivaloni (kama wewe ni profesa kweli) uone mikakati ya kanisa dhidi ya waislam ilivyo ya enzi na enzi.
  Pia rejea mfumo wa elimu kabla ya matumizi ya namba za badala ya jina kwenye mitihani yote-mambo yalikuwaje kwa waislam? Wengi wao walishindwa hususan kutoka mikoa yenye waisla wachache kama vile mara, mwanza, kagera na kwingineko -fanya uchunguzi tafadhali
  Kwa taarifa -elimu ya awali lengo lake si kuwafanya watoto wajue kusoma na kuandika, sidhani wewe uliiipta elimu hiyo, lkn leo u profesa (fake)
  Angalia mfumo na jiridhishe ndo upata fursa ya kusema mbele za watu wanaoelewa ubndani wake suala hili. Tazama MoU kati ya serikali na kanisa katoliki malipo ya mabilioni yanaenda huo kufanya nini? Lkn ujue tu kuwa uvumlivu una mwisho wake' ikibidi waislam wengi hawana la kupoteza katika vurugu-nyie mnaoogopa kuacha mahekalu -kazi kwenu
   
 16. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndipo hapo mnapodanganyana...mambo ya vurugu kwenye karne hii hayana nafasi...ukitaka kupambana hakuna ni jinsi ni lazima kurudi shule...
   
 17. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Miskiti mingi sikuiz ina shule za chekechea ambazo zinafundisha Quran ma masomo mengine ya kishule( eg Annur - Sinza, Mtambani - Kino, Qubbah, Kichangani, Tawba, Tayma na mingineyo mingi tu).TUNACHOSUBIRI NA SISI WAISLAM TUSIGN MOU NA SERIKALI ILI TUJITANUE KIELEIMU (MOU itatuwezesha kupata best Teachers, kupata best facilities) NA KUJENGA MAHOSPITALI, MASHULE, NA MENGINEYO: Wenzetu wa mlengo wa kushoto walituzunguka wakasign MOU kimya kimya /kisiri siri na Serikali matokeo yake ndo tofauti/Gap ambayo waislam Tunaipigia kelele. INSHALLAH kila lenye Mwanzo Lina mwisho wake.
   
 18. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Professor MAJI MAREFU.
   
 19. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hili ni wazo zuri. Kuna haja ya Bakwata kwenda Uganda na kujifunza jinsi shule za Kiislam zinavypfanya vizuri sana.
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  Na sisi Singasinga NECTA inatuonea sana, tunataka mkurugenzi wa necta awe singasinga
   
Loading...