Ndugu zangu waislam dini yenu inasemaje kuhusu wageni mwezi wa Ramadhani?

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
5,903
8,230
Niwatakie mfungo mwema.

Nimesikia kwenye kipindi cha njiapanda leo huyo mdada alikaribishwa na mwenyeji wake huko dar, lakini juzi wakati mfungo unakaribia mwenyeji wake akamwambia aondoke maana mfungo unaanza!

Sasa mwezi mtukufu na kutimua wageni inakaaje kaaje hii? Ukizingatia mgeni mwenyewe alikuja kwa ajili ya matatizo ya kuuguza.

Dini inasema hivyo au ni roho mbaya tu ya mwenyeji?
 
1)Inawezekana huyo alikua anamtafutia sababu toka mda tu..

2)Inawezekana huyo mgeni siyo mfungaji kwahiyo ostazi hataki aone mtu anakula mbele yake kipindi yeye amefunga
 
1)Inawezekana huyo alikua anamtafutia sababu toka mda tu..

2)Inawezekana huyo mgeni siyo mfungaji kwahiyo ostazi hataki aone mtu anakula mbele yake kipindi yeye amefunga
Hii namba mbili mbona sioni kama ina mantiki huwani watu na roho zao tu kwani mtu akila na wewe ukifunga kuna shida gani?

Kama huyo anayekula labda huwa anakushikia panga na kukufunga kamba kisha anakulisha kwa lazima sawa ila kama anakula kivyake sioni shida .
 
Wanasema ni dini ya myaanzimumgu..dini ya haki..hapo keshatenda haki tayari.

#MaendeleoHayanaChama
 
Katika uislam Kuna watu ambao wameruhusiwa kula mchana wa ramadhani miongoni mwao ni wagonjwa, wazee, waliorukwa na akili, mtoto ambae hajabalehe na wasafiri

Kwahiyo Kama kamfukuza mgonjwa hiyo ni uamuzi wake na siyo mafunzo ya dini ya kiislam.
 
Kuna watu humu ndani huwa wanaleta habari kwa ajili ya kuwachonganisha watu,bila kujua kwa Mwenyezi Mungu hakuna dogo kila kitu kiwe kidogo au kikubwa tutakikuta siku ya hukumu.

Hakuna Dini inayosisitiza upendo kama Uisilamu,iwe kwenye shida au raha,tena hawabagui mtu,kama kufuturu watu wanajitolea kufuturisha wasiokuwa na uwezo na hawaangalii wewe wa dini gani,

Najua kutokana na kubana kwa maisha kipindi hiki hata wasio kuwa waisilamu huwa wanajichanganya kuanzia watoto wadogo mpaka watu wazima
 
Sijajua uhusiano baina ya hao wawili.

Kwa haraka haraka jamaa kaemda kinyume na dini, tumefunzwa kuwakirimu wageni, kuna thawabu kedekede, maswahaba walikuwa wanagombea kukirimu wageni. Uislam unatufunza tupendane, tuunge udugu, sasa huyo sijui muislam wa wapi.

Ila kuna UISLAM na muislam, tusichanganye hivi vitu. Naweza kuwa ostafh mkubwa tu ila mzinifu, mganga wa kupiga ramli, haimaanisji kuwa dini yangu ndio imeruhusu hayo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom