Ndugu zangu wa Kike Huwa najiuliza Eti Kwanini...?

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Ndugu zangu nauliza kwa vile kiukweli sifahamu kwanini ndugu zetu wa kike walio wengi huachia maungo yao kuonekana hadharani?
Nazidi kuchanganyikiwa iwapo mwanamke huyo yuko tayari katika mahusiano ya kweli kama ndowa au urafiki wa kupendana hasa!



Natanguliza samahani iwapo nitamkosea yeyote lakini ni kweli kuwa natafuta sababu nashindwa kuzipata. Ndugu zangu wa kike nahisi wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kunisaidia.
 
wanaacha wazi kwa sababu wanataka kuacha wazi.

Kama wanakukera vaa miwani ya mbao,
 
Wewe mbona pua yako umeiacha wazi hatusemi (au pua si ungo la mwili)?

Nani alisema au aliweka sheria nini kifichwe na nini kisifichwe?
 
lakin mi nafkiri kaka kuna mazingira ya kuachia mwili na yasiyo yakuachia mwili wazi...mfano upo club, swimming na maeneo mengne ya starehe za usiku...na ukiwa na mpenzi wako sion tatizo ....lkn km m2 ataamua from no where kukaa uchi atakua na intension yake piaa...may be yupo ktk makasino anajiuza...nk.
 
mbona mm naona makalio na mifereji ya wanaume njeeeee peupeee mchana!!
 
Ngekewa tatizo tunaishi katika jamii ambazo zimechanganikana kimaadili Linapokuja sula zima la mavazi. Kuna wanasema manamke akivaa blouse na skirt yupo uchi, kuna ambae akiona dada amevaa skirt ndefu hadi chini na blouse singlet, ataona yupo uchi, basi ili mradi tu.... Sasa tokana na kwamba hilo suala ni relative term katika jamii yetu, wewe unaona avae vipi mwanamke ili usione yupo uchi?
 
ngekewa, ni maadili yamekuwa mabovu,hata mimi sioni sababu ya kuacha maungo wazi, anaye takiwa kuona ni mwanaume wako tu, na kaunga, pua ipo wazi na nje cku zote kwanini mungu aliwavalisha admu na eva ngozi akawafunika asiwavalishe puani.? ni vizuri kuyaficha maungo yako kwani ukiyafunika pia utakuwa umeepuka dhambi.
 
kombai 3.jpg kombai 1.jpg kombai 2.jpg

Unaona hawa
Wala hawalalamiki
Na heshima mbele
Na hakuna kutamani mke wa mwenzio

Hahaha. . . wanafundisha nini huko na mimi niende?
 
View attachment 46090View attachment 46091View attachment 46092

Unaona hawa
Wala hawalalamiki
Na heshima mbele
Na hakuna kutamani mke wa mwenzio
Hua nikiangalia vipindi vinavyohusiana na watu wa aina hii hua nashangaa iweje wao waweze kujicontrol/wawe na discpline na sisi tushindwe. Maana wangekua kama hawa wakwetu nadhani kila siku kungekua na kesi kadhaa za ubakaji.

Tatizo hawa ndugu zetu tamaa na kujiendekeza vinawasumbua sana, kila kitu wanahusisha na ngono, mpaka urembo wa mwanamke achilia mbali mavazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom