Ndugu zangu tupunguze maneno, tuongeze vitendo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu zangu tupunguze maneno, tuongeze vitendo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by geek, Sep 16, 2009.

 1. g

  geek Member

  #1
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha wenzetu wanatuzi ubunifu, ingawa siasa zao ni hatari kuliko za kwetu, ikija kupiga hatua za kimaendeleo hata robo hatuwakaribii. Nawaonyesha mfano kutoka Kenya ambao wametumia brand ya Tinga Tinga kuandaa cartoons, au animated chatacters kupata deal kubwa ya kibiashara Ulaya na Marekani. Soma story ya BBC hapa.

  Hiyo ni sehemu ya story nyingi za mafanikio ya teknolojia Kenya, wamejipanga vizuri sana kutumia fibre optic cable. Sisi kwetu Tanzania, Waziri wa teknolojia akiombwa interview na vyombo vya nje anaingia mitini [kama wako competent wanaogopa nini kuhojiwa? - ingawa kipimo cha kazi yao siyo kutoa interviews], TCRA wameombwa interview na BBC zaidi ya mara tano wanatoa visingizio.

  Inakera kuona tunaongozwa na watu wasiokuwa na shauku ya kuisogeza mbele nchi yetu, inakera kuona tunaongea zaidi kuliko tunavyotekeleza mipango.

  Katika modern society, Tanzania inatakiwa kuwa na rivals, au benchmark za kujipima nazo progress ya nyanja mbali mbali. Hayo yote hayafanyiki, badala yake kipimo chetu ni CCM na wapinzani. Blah blah.....
   
 2. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu maneno kama haya wengi hatutaki kuyasikia, sisi hapa tunataka kusikia ccm chini chadema juu.Habari ndo hiyo.

  Tunawalaumu sana viongozi lakini ukiona sisi tunavyochonga hapa utaona ni afadhali ya chilingati.

  Haiwezekani kabisa kama mtu unapiga mzigo kama wenzetu hawa waupe yani mtu within no second awe na posts 5000.

  Nawapongezeni wote wenye posts nyingii lakini pia nikiashiria cha uzembe hatufanyi kazi ,tumekalia propaganda.
  Bora Kikwete mara mia elfu.
   
Loading...