- Mwanasheria wa TCRA anasema tatizo la JamiiForums haifuati masharti na kutolea mfano tovuti kadhaa zinazofata masharti, cha ajabu tovuti hizo hazifati sharti ambalo JamiiForums imepelekwa nalo mahakamani. Je kuna sharti la nyuma ya pazia ambalo hawajatuambia?
- TCRA ni mwanachama wa muda mrefu humu jamvini tena verified na last seen yake ipo ya wiki hii, ni kwa nini anakuwa mwanachama hai wa mtandao ulio kinyume cha sheria.
- TCRA ni taasisi ya serikali, ni kwanini anaziacha taasisi zilizo nae chini ya mwamvuli mmoja na kukimbilia kutoa boriti za sekta binafsi tena mahakamani.
- Nipashe waliandika habari flani mkaja na kututoa hofu na kusema nipashe wamepotoka na hiyo habari wameandika peke yao katika magazeti yote, mmebadili msimamo? Wengine tunapata ukakasi na mabadiliko yenu ya ghafla.
- Mwanasheria kukimbilia kusema tutafungia kabla hata kesi yenyewe haijaanza kunatupa mashaka, naomba siku ya kufunga wafungie tovuti zote zenye dot com na waone hasara yake.
Naomba wakawakamate wakurugenzi/mawaziri wa taasisi za serikali(msishitaki taasisi) zilizo na wavuti za .com wawekwe ndani kwanza wakati wanatafutiwa makosa rasmi tena na viongozi wengine wakubwa wa serikali wana tovuti binafsi zenye .com, haiitaji kuwatafuta kwani wametajwa kwenye gazeti mojawapo la leo.