Ndugu zangu TCRA, muanze kujitumbua kabla ya kuishika shati JamiiForums

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,153
2,000
  1. Mwanasheria wa TCRA anasema tatizo la JamiiForums haifuati masharti na kutolea mfano tovuti kadhaa zinazofata masharti, cha ajabu tovuti hizo hazifati sharti ambalo JamiiForums imepelekwa nalo mahakamani. Je kuna sharti la nyuma ya pazia ambalo hawajatuambia?
  2. TCRA ni mwanachama wa muda mrefu humu jamvini tena verified na last seen yake ipo ya wiki hii, ni kwa nini anakuwa mwanachama hai wa mtandao ulio kinyume cha sheria.
  3. TCRA ni taasisi ya serikali, ni kwanini anaziacha taasisi zilizo nae chini ya mwamvuli mmoja na kukimbilia kutoa boriti za sekta binafsi tena mahakamani.
  4. Nipashe waliandika habari flani mkaja na kututoa hofu na kusema nipashe wamepotoka na hiyo habari wameandika peke yao katika magazeti yote, mmebadili msimamo? Wengine tunapata ukakasi na mabadiliko yenu ya ghafla.
  5. Mwanasheria kukimbilia kusema tutafungia kabla hata kesi yenyewe haijaanza kunatupa mashaka, naomba siku ya kufunga wafungie tovuti zote zenye dot com na waone hasara yake.
Mwisho kabisa naomba nichepuke kwa ndugu zetu polisi, DPP kukamata watu bila kosa kisha ndio mnawatafutia kosa ni sawa au uliteleza au ulinukuliwa vibaya? Mimi mtanzania wa kawaida ambae sina publicity wala nguvu kubwa ya mawakili mnanitia mashaka na kupoteza imani nanyi. Na hayo makosa mliyoyatawanya si kuna kesi ya kikatiba iko mahakamani?

Naomba wakawakamate wakurugenzi/mawaziri wa taasisi za serikali(msishitaki taasisi) zilizo na wavuti za .com wawekwe ndani kwanza wakati wanatafutiwa makosa rasmi tena na viongozi wengine wakubwa wa serikali wana tovuti binafsi zenye .com, haiitaji kuwatafuta kwani wametajwa kwenye gazeti mojawapo la leo.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,884
2,000
Hili la kukamatwa then utafutiwe kosa ni aibu kwa taifa. Ni vyema tujenge umoja na utaifa kwa kutenda haki. JPM nimekuunga mkono ili ulete mabadiliko ya kweli ikiwemo mkondo sahihi wa kisheria. Hili la Max limetushtua wengi na kutufanya tujiulize kama tupo sahihi ktk misimamo ya kukuunga mkono. Tumia mabavu kwa mafisadi na mambo ya msingi lakini si uhuru wa habari. Hakuna uhuru usio na mipaka lakini mipaka isitumike vibaya.
 
mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
927
1,000
Ambacho sijaelewa mpk sasa unapoishtaki Jamiiforums unapaswa kumkamata CEO wake ama unaishtaki yenyewe kama Kampuni ambapo itakuja kuwakilishwa na wanasheria wake endapo kesi itafika mahakamani. Mfano TIGO leo kukiwa na ukiukwaji wowote ule wa sheria, huwa akamatwi CEO wa Tigo na kushtakiwa bali TIGO kama kampuni. Wanasheria mtusaidie.
 
Cognitivist

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,058

Good observation, ukipata majibu nijulishe na mimi
 
Jun 8, 2013
16
45
Ambacho sijaelewa mpk sasa unapoishtaki Jamiiforums unapaswa kumkamata CEO wake ama unaishtaki yenyewe kama Kampuni ambapo itakuja kuwakilishwa na wanasheria wake endapo kesi itafika mahakamani. Mfano TIGO leo kukiwa na ukiukwaji wowote ule wa sheria, huwa akamatwi CEO wa Tigo na kushtakiwa bali TIGO kama kampuni. Wanasheria mtusaidie.
Hapo sasa
 
General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,796
2,000
TCRA kumejaa vilaza hatari...
Wanatamani kuufungiaa huu mtandao lkn hawana watu wenye ujuzi huo.

Ile taasisi mnaiogopa tu bure lkn hamna kitu mlee.
 
Calaboca

Member
Dec 18, 2016
19
45
Ambacho sijaelewa mpk sasa unapoishtaki Jamiiforums unapaswa kumkamata CEO wake ama unaishtaki yenyewe kama Kampuni ambapo itakuja kuwakilishwa na wanasheria wake endapo kesi itafika mahakamani. Mfano TIGO leo kukiwa na ukiukwaji wowote ule wa sheria, huwa akamatwi CEO wa Tigo na kushtakiwa bali TIGO kama kampuni. Wanasheria mtusaidie.
Ni mwendo wa kutumia nguvu tuu.. Tatzo kubwa kila mtu anatafuta kiki. Yaani mpaka shida.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom