Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa

Pole sana ndugu, jifunze pia kuandika naona elimu yako na ulichoandika hapa akisadifiani
Story ni ndefu mno japo kunavitu sikuviandika imenipa tabu sana kuifupisha, pia sim yangu ukiandika mambo inakuletea may be nahisi screen haipo poa.
 
Editi taratibu ikae sawa maana hapa watakuja kusoma mpaka vijukuu vyako, watashangaa
 
Kunisaidia kwahiyo ndio hata kwenye msiba wa baba yangu wasije? Sijakataa kuwa hawajanisaidia ndio maana kuna kipindi huwa nawapigia kuwasalimia tu lakini sim zangu hazipokelewi utaelewaje hapo?
vitu vidogo hivyo sio vya kuvibebelea mtoto wa kiume. wangekuja wangebadili nini? na unafahamu chanzo cha ugomvi wa baba na mama yako mpaka wakaachana? huenda ndio sababu.fikiria zaidi ya hapo na uache kutaka kusaidiwa tu na kulaumu
 
unasaidiwa unalalamika. we katika historia yako umewahi kusaidia nani na ilikuwaje?
Wapo watoto wa marehem baba yangu mdogo nawasaidia, na ninawasomesha unalingine? Pia babu yangu namtumiaga pesa ya matumizi kila mwisho wa mwezi.
Pia kuna dada yangu ambae ni binam nilimpa mtaji afanye biashara na hiyo pesa nilimpa tu japo huyu dada yangu ananijari kwenye shida na raha.
 
Pole sana ndugu!

Inakupasa usikate tamaa. Mungu ana sababu ndio maana pamoja na magumu ya ndugu lakini amekupa mke ambaye ni faraja kwako. Jipe moyo. Wewe ni mtu mwema.
 
Kwa sasa nipo mbali nao ila Roho inaniuma sana maana ninacho hitaji tu nikuwa karibu na ndugu zangu, japo kuhusu msaada sihitaji ila ukaribu tu unatosha.
Wewe Ng'ang'ana tu na ndugu hao. Watu hawakujali unataka ukaribu kwao kiaje?
 
Wapo watoto wa marehem baba yangu mdogo nawasaidia, na ninawasomesha unalingine? Pia babu yangu namtumiaga pesa ya matumizi kila mwisho wa mwezi.
unawasomesha shule zipi? private au hizi za bure? au unanunua tu madaftari inasema unawasomesha? unajua wanaishi kwa kula na kutibiwa vp? wao pia wakisema matibabu huwasaidii utawaelewa na wewe uwezo wako ni wamadafatri tu? vp kama wangetaka uache harakati zako za kuoa ili uwapatie kila wanachohotaji ungeweza? hiyo ndio ilikuwa kwa baba zako wadogo walikusaidia walipoweza ili na mambo yao yaende. level up bro
 
Mkuu mimi nimeajiliwa wadogo zangu tayari kaisha anza shule, hivyo hata hayo madaftari ni msaada tosha na hata huwa akiniambia anaumwa nampeleka hospitali, au wewe mpaka nimpeleke private ihali sina miaka mingi ajirani?
 
unawasomesha shule zipi? private au hizi za bure? au unanunua tu madaftari inasema unawasomesha? unajua wanaishi kwa kula na kutibiwa vp? wao pia wakisema matibabu huwasaidii utawaelewa na wewe uwezo wako ni wamadafatri tu? vp kama wangetaka uache harakati zako za kuoa ili uwapatie kila wanachohotaji ungeweza? hiyo ndio ilikuwa kwa baba zako wadogo walikusaidia walipoweza ili na mambo yao yaende. level up bro
Anyway asante mkuu maana ushauri wako sio mbaya ila mda mwingine napitia magum sana kutokana na kuugua na kupona bila dawa, yaani mpaka sasa huwa napata shida na chakushangaza naenda hospitali kubwa kupimwa hakuna hawaoni ugonjwa na hapo nakua hoi balaa.
 
Unatakiwa kujua ya kuwa ‘haya maisha ni VITA’ hasa kwa jinsia ya kiume.
Ukishaelewa hilo mkuu utafocus na familia yako, acha kuweka vinyongo
 
Mkuu huwa sina kinyongo kabisa japo nimepitia mengi na manyanyaso, nilishawahi soma kwahuyo baba yangu mdogo kipindi niko secondary mke wake alininyanyasa hadi kuninyima chakula lakini nilipo ajiliwa nilikuwa namtoa hata out huyo mamdogo aliye ninyanyasa.
Haya pamoja na hayo ndugu zangu wote nilikuwa nawapigia hata kuwasalimia tu pamoja na kuwa wamenipitisha mengi, nikipata likizo naenda kuwasalimia japo wao kuja kwangu hawajawahi.
 
Mimi naona wewe ndyo huna maamuzi na maisha yako na unaishi labda unataka kuwafurahisha kujiweka karibu nawo anyway ndugu ata akiwa Yule wa damu kwenye kujenge maisha yako wewe ni WA muhimu kuliko yeye jiangalia wewe na maisha yako Kwanza kabla ya mwingine maana naona mbeleni utakuwa na mzigo mkubwa sana WA kurudisha fadhila na usipokuwa makini utasikiliza lawama zao utaaribu mwelekeo WA maisha yako
 
Mkuu sio kwamba nashindwa kujiwekea msimamo, tatizo wamenisaidia mno hata hii ajira niliyo nayo nikwasababu yao nikiangalia kunamazuri wamenifanyia japo mabaya ndio hayo, nashindwa kujiweka mbali nao nahitaji ukaribu nao maana siku zote tuangalie mazuri ila kilicho nishinda nikuendelea kuwabembeleza kuwatafuta. Na pia wale ni mama zangu na baba zangu yaani nawaza mpaka moyo unataka kuchomoka labda niliwakosea mimi sijui.
 
Kwa sasa nipo mbali nao ila Roho inaniuma sana maana ninacho hitaji tu nikuwa karibu na ndugu zangu, japo kuhusu msaada sihitaji ila ukaribu tu unatosha.
Pole sana mkuu, inaumiza sana najua hali unayopitia. Jaribu kujenga ukaribu sana na watoto wako pamoja na ndugu wa mke wako itasaidia
 
Back
Top Bottom