Ndugu zangu mnanilaumu bure tu. Mngenisikiliza kwanza

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Imagine nimetua tu siku chache ago nmepokelewa na lawama sana.watu mnanilaumu mpaka nashindwa hata kula.mpishi wangu huyu kutoka India anaanza kukosa raha anadhani sipendi chakula chake kumbe sivyo.

Mimi misaada nliyokuwa natoa kwa watu haikuwa na lengo la kunifanya nigombee ubunge au urais.sikuwa na nia hiyo. Ni kautaratibu kangu tu nmeweka kuwa kwa mwaka angalau nitumie tumilion mia kadhaa kusaidia wenye uhitaji.

Wala haikuwa kampeni. Nmeshangaa walinzi wanaolinda nyumba ninayoishi nao wamelalamika kuwa Mzee... Tulitegemea uchukue form nikashangaa form za nini tena.ndo wananambia za urais au ubunge.

Na hili nmeligundua baada ya kusikia kuwa walinzi mpaka wanalogana ili wawe wanapangiwa lindo kwenye nyumba yangi Oysterbay kumbe wanagombania hiyo nafasi sana huwezi amini wengine wanawaambia supervisors wao wapangiwe kuja kulinda kwangu na mshahara wao uchukuliwe na supervisors.

Leo wamesikia nimerudi wamekuja hapa zaidi ya 20 na familia zao kuja nisalimia na ndio wanalalamika kuwa why sikugombea nafasi hizo nimeshtuka sana nimeshangaa maana mimi nina uraia wa nchi nyingine.

Jamani msinilaumu bure mimi sitaki urais wala ubunge nafasi nliyonayo nikitaka kuwa raisi maana yake nakuwa demoted.sitaki kushuka cheo.niacheni tu ndugu zanguni. Tutasaidiana bila masharti. Mkiwa na shida msisite kunambia ntawasaidia tu.

Nitakuwepi nchini kwa siku chache halafu nisafiri tena nchi za wenzetu.ntapita pia canada na sweden kusalimia jamaa zangu.
 
Dah! Kiduku leo nimekukumbuka ukatokea. Mkuu kwani huhitaji kijana wa kufutafuta viatu vyako vumbi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom