Ndugu zangu mliosoma masomo yasiyo ya sayansi na mkasoma astashahada stashahada na shahada na hakuna matumaini ya kupata ajira badilikeni msome ufundi

Profesa ntare nkobe

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,957
8,071
Hali ni ngumu sana mkikaa mnasubuli ajira wakati mda na wakati una jieleza wenyewe mtachelewa kufanikiwa ni kheri mkachukua kozi za ufundi mwaka mmoja VETA au chuo kinacho tambulika na VETA fani haimtupi mtu mwezi form zinatoka mwezi wa kumi kuna mtihani wa kujiunga na VETA January masomo yana anza changamkieni fursa.....
 
ushauri mzuri,
mm asaiv nikiona tu dogo kaenda arts advance napata mashaka na huko anakoelekea, japo hata hio sayansi nayo jau, ila ukifaulu vzr sio rahs ukasota,
 
Hali ni ngumu sana mkikaa mnasubuli ajira wakati mda na wakati una jieleza wenyewe mtachelewa kufanikiwa ni kheri mkachukua kozi za ufundi mwaka mmoja VETA au chuo kinacho tambulika na VETA fani haimtupi mtu mwezi form zinatoka mwezi wa kumi kuna mtihani wa kujiunga na VETA January masomo yana anza changamkieni fursa.....
Wewe ndiyo unayowaza ajira yako .Wenzako wanakusubiri uje kukopa mchele unga ili ulipe mwisho wa mwezi .Mwenyewe umeona umepatiaaaaaa kumbe umeingia umaskininj.
 
Na heshimu maoni yako hupo sahihi...Sijawai kuwa masikini fani yangu ya Mason inanilipa nashukuru Veta kunipa ujuzi utakao ni saidia maisha yangu yote na mwisho fani haijawai kumtupa mtu..
 
Mason inahusu nini na kwa hapo veta gharama zake zimekaaje na ni kwa muda gani hadi umalize na soko lake la ajira kwa hapa bongo limekaaje mkuu
 
Samahani niulize swali..asilimia nyingi mafundi nimeahuhudia kwa macho yangu anaishi nyuma hafifu au nyumba ya kupanga ..shida huwa iko wap km ww ni fundi ujenzi🤔
 
Mafundi wanaishi maisha magumu Sana sjui Kwa nn, kuna Mwamba hapa ana vifani vya electronics,kazi kutengeneza simu, tv , kufunga vingamuz n.k, kufunga wiring, lakn kachakaa kinyama , anaishi chumba cha 20000, ana mke na watoto wawili, mke anauza karanga barabarani , sioni future kabisa labda ngekewa imtokee,....sa hv ili utoboe inahtaj akli nyingi sana,
 
Sio wote mkuu mimi nimeishi na mafundi wengi kuanzia mzee wangu mwenyew(R.I.P) alikua mechanic hatukuwahi kukosa mahitaji muhimu,
Mwingine fundi wangu aliye nifundisha kazi yupo vizuri anamiliki plot ya gerej yake mwenyew ana gari pia.
Kwa kifupi kazi ya ufundi ukiifanya kwa weledi itakulipa vizuri mkuu ila usipoheshimu kazi yake ndo matokeo yake hayo, from my experience nimeshudia mafundi wengi wanafeli kwa sababu ya lifestyle zao tu hakuna kingine.
 
Kweli kabisa, mwaka 2016 nilihitimu Shahada ya Ualimu nikaona mtaani hakukaliki 2018 nikazama VETA kuchukua kozi fupi ya UMEME WA MAJUMBANI na pesa ya vocha hainipigi chenga. Mwezi huu wa 9 narudi tena VETA kusoma UMEME WA VIWANDANI huku nikichukua na ujuzi wa kusuka mota na welding machine.
 
Mason inahusu nini na kwa hapo veta gharama zake zimekaaje na ni kwa muda gani hadi umalize na soko lake la ajira kwa hapa bongo limekaaje mkuu
Mason nu uashi(fundi ujenzi) hii ndo naweza kusema ni fani mama Yaani fundi umeme, rangi, mabomba, vigae, welding wanamtegemea yeye. Bila uashi fundi umeme hana kazi nk.
 
Back
Top Bottom