Ndugu zangu huko TBC, katika kuboresha vema muonekano wenu, tunaomba mtuwekee "Digital Clock and Date" upande wa chini - kushoto wa screen zetu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Mambo vp ndugu zangu wa hapa jamiiforums.

Kwanza ninaomba kuanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo pamoja na shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kuamua kuwa Wazalendo kwa vitendo zaidi na kuamua kuboresha muonekano wa TBC.

images.jpg

Sasa hivi huwa nikiwa ninatazama TBC ARIDHIO ile saa moja jioni ni kama vile ninatazama CNN, BBC au Al Jazeera kwa maana camera na majukwaa ni ya kisasa, watangazaji wa kiume ni watanashati sana, hao akina dada ndio usiseme yaaani ni warembo saaaaana hususan yule dada wa kipare sijui mchagga wanamuita Elizabeth Mramba.

I congratulate you guys once again. Huyo Elizabeth Mramba kama hajaolewa mpaka sasa ninaomba mwenye number zake anipe mara moja wakuu kwa maana sio kwa weupe ule. Hahahahahaaaa, I am joking.

Sasa ngoja niende moja kwa moja kwenye ombi langu. Mimi ombi langu kwa siku ya leo ni kuhusiana na "Digital Clock and Date" upande wa chini - kushoto kwa maana sio kila sehemu watu wanatumia saa ya ukutani na sio kila muda mtu anakuwa ameshika simu mkononi ili aweze kutazama muda.

Kama mnaweza kuiweka hiyo "Digital Clock and Date" wakati wa kipindi cha ARIDHIO, kwanini ishindikane kuwa pale muda wote? Kwanini huwa mnaiondoa baada ya ARIDHIO kuisha nyie wazalendo wenzangu?

frdgfgfrfvd.jpg

Kama mtaweza kuboresha muonekano wenu kwa kuweka hiyo "Digital Clock and Date Gadget" muda wote mnaokuwa mpo hewani mtakuwa mmwewasaidia sana watu kama wale vijana wanaokula kwa mama lishe, wanaokuwa wananyoa kwenye barbershops huku wanatazama TBC.

Pia hata sisi ambao kila asubuhi kabla ya kwenda katika shughuli yangu kijiweni ya kuendesha TAXI BUBU huwa ni lazima nitazame TBC kwanza ili kuweza kufahamu kuna kipi kimejiri hata Tanzania na hata duniani. Ukitazama kwa umakini picha mbili nilizoambatanisha hapo juu, unaweza ukaelewa ninachoshauri mimi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom