Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Embu mbinu mloitumia niianze mwishoni mwa mwezi ili nijhesabie maana kwa sasa bajeti yangu kwa sasa ni kubwa sana kwenye huu ulevi unaoitwa SIGARA
 
Ndugu zangu, kaka, dada zangu na wadogo zangu...

Nimekuja mbele yenu nikiwa na tatizo moja ambalo ni kubwa sana kwangu..........

Ni hivi...

Kama miezi michache iliopita ((mwezi wa saba mwaka Jana)) kijana mwenzenu nilipatwa na tatizo kubwa sana LA kusimamishwa kazi eneo nililokua nafanyia kazi,,,,tulisimamishwa mim na wenzangu watatu kwa kuonekana kuna upotevu flan wa fedha nyingi sana ambazo zinatumwa na wahisani kwa ajili ya watoto yatima na walioathirika na VVU.

Ukweli niliohapa mbele ya Mungu wangu ni kwamba sikuhusika kabisa na uwizi huo wala sikushiriki kutafuna hizo hela,,,na mim ni mfanyakazi wa chini sana pale ofisini lkn nikashangaa kwa nn nihisiwe mm wakati mahela wana yacontrol wao,,!!! na mpka uchunguzi ulipo fanyika nilionekana sina hatia juu ya fedha hizo na nikarudishwa kazini......wenzangu wawili mpka Leo hawajarudishwa..

Sasa shida ni kwamba..
Kipindi kile nilijikuta mwenye stress na mawazo sana jambo lililonipelekea kua mlevi niliepindukia yani pombe asubuhi mpaka jioni na uvutaji wa sigara uliokithiri....sio siri nilikua napiga sigara na pombe kiasi ambacho siwez hata kuelezea vizur mkaelewa.....

Upande wa pombe nilikua nagusa kidgo kidgo tangu miaka mingi iliopita lkn sikufikia hatua ya kuitwa mlevi,,lakn upande wa sigara ndo nilikua nimeanza kipindi hicho cha matatizo....before sikuwahi kabisa kutumia...

Sasa japo matatizo yalikuja kuisha lkn bado nimekua naendelea tu kuvuta maana nimekua nikikaa tu masaa manne au matano bs najiskia hamu ya sigara vibaya mno na kuamua kununua na kuvuta........yani huwa najaribu kujizuia sometimes inafika mpka jioni ghafla nakuta kiu kimekolea ile mbaya bs napiga tenaa........

Kilichonileta hapa ni kwamba naomba sana ndugu zangu mnisaidie nifanyeje ili niweze kupunguza kwa kiasi kikubwa kuvuta sigara na kupambana na kiu inayokua inanibana mpka mwishowe niache kabisa...kabla madhara makubwa sana ya kiafya yajaanza kunivaa..

Naamini humu kuna watu wamewahi kua wavutaji wakubwa wa sigara na wakafanikiwa kuacha.......

Msaada wenu tafadhar..
Note:: mpka Leo hii hakuna ndugu anaefahamu kama navuta sigara.......wakija kujua...kama mama angu ndo nahisi atachanganyikiwa sana na ataumia sana.....hata girl friend wangu hajawahi bahatika kunikuta na harufu ya sigara,,akija kujua tu bs naamini kabisa uwanja wa mapenzi utaota nyasi....daaaahh

Nisaidieni niache hii kitu ndugu zangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndo hapo kaka....yani wameniedita heading yangu na kuandika upuuzi ambao hauleti mantiki.....yn wamemaanisha kwamba nataka niache sigara sababu ya ndugu.....akati kwenye mada nimedhihirisha wazi kwamba nahitaji kuacha sababu ya afya yangu
Hapa mods mbona wamekufanya uonekane mnafiki! Eti unataka kuacha kuvuta sigara ili uonekane mzuri mbele ya watu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndo hapo kaka....yani wameniedita heading yangu na kuandika upuuzi ambao hauleti mantiki.....yn wamemaanisha kwamba nataka niache sigara sababu ya ndugu.....akati kwenye mada nimedhihirisha wazi kwamba nahitaji kuacha sababu ya afya yangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana, mkuu!!! Hapa mods kama ana ustaarabu anahitajika kukuomba msamaha.
 
Amenikosea sana kaka.....ila fegi zinanisumbua sana nazo

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuachana na fegi, mkuu utahitaji nidhamu ya hali ya juu sana. Anza kwa kupunguza uvutaji kidogo kidogo kila siku, na huku ukianza mazoezi na chakula yenye lishe bora! Punguza zile mawazo zinakufanya uvute! Pia kuna kitu inaiitwa 'nicotine patches' ni kama plaster hivi, unabandika mahali na pole pole inakusaidia kuacha kuvuta fegi.
 
Ahsante mkuu....sijawahi kusikia kuhusu huo nicotine plaster.....nielezee kidgo
Kuachana na fegi, mkuu utahitaji nidhamu ya hali ya juu sana. Anza kwa kupunguza uvutaji kidogo kidogo kila siku, na huku ukianza mazoezi na chakula yenye lishe bora! Punguza zile mawazo zinakufanya uvute! Pia kuna kitu inaiitwa 'nicotine patches' ni kama plaster hivi, unabandika mahali na pole pole inakusaidia kuacha kuvuta fegi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom