Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

30 OKTOBA 2020

Tumekuwa wafuatiliaji wakubwa wa kampeni zako tukiwa na matarajio ya kupata mengi mazuri baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ukionyesha hali ya kushiriki vema katika kampeni zako.

Na kwa kweli ulianza vema ufunguzi wa kampeni zako kupitia CHADEMA yetu, ila tulianza kupata shaka baada ya kuona kauli zilizoanza kutoka muda mfupi baadaye ambazo zilitukumbusha msemo wa wahenga 'Asiyekubali kushindwa si mshindani.'

Hii ni kwa sababu ulituonyesha kuwa hukuja kushindana bali ulikuja kushinda kwa njia yoyote ile. Kauli zako zilionyesha hamasa za kuleta vurugu kati ya jamii na ndugu zetu Watanzania ili kuiangusha CCM hata kwa kumwaga damu ili wewe ukae katika kiti cha urais.

Leo tumesikiliza taarifa yako ya kukataa matokeo yanayoendelea kutolewa ukishinikiza jamii ya kimataifa kukataa uchaguzi huu. Tunadhani mshtuko mkubwa ulioupata wewe na viongozi wetu wa CHADEMA ni kuangushwa kwa Mgombea Freeman Mbowe ambaye amekuwa ni mbunge kwa miaka mingi na wabunge wengi mashuhuri hali ambayo hukufikiria.

Pengine ni kutoijua vizuri nchi yako kwa kipindi ulichokuwa ughaibuni. Ila tungependa kukujulisha yafuatayo kwa faida yako na viongozi wengine wa CHADEMA tukijibu mazungumzo yako ya leo.

1. UCHAGUZI NI HURU NA WA HAKI
Hakuna Mtanzania hata mmoja aliyekataliwa kupiga kura ikiwa na vigezo vinazohitajika. Mawakala wetu wa CHADEMA wametujulisha kuwa walikuwepo na wameshuhudia zoezi isipokuwa wanashangaa video zilizosambaa mtaani zikionyesha uzushi wa kutengeneza kuwa kura zimekamatwa.

Jamii za kimataifa zimefika na kuangalia zoezi zima. Hivyo, unachosema ni kujaribu kutafuta sababu ikiwa hali halisi unaijua. Tukubali tu tulizoea ubabaishaji ila sasa hivi tujipange upya kwa ajili ya uchaguzi ujao. Pia suala la mawakala kutopewa nakala za matokeo ni uzushi kwani chama chetu hadi kufikia usiku wa tarehe 28/10/2020 tulishajua upepo si mzuri.

2. HATUKUONEWA
Wanachadema tunajiuliza swali; Kama mawakala walikuwepo na hakuna aliyetoa ushahidi wa kukataliwa kuingia kituoni kwa nini hatusikii malalamiko hayo toka kwa mawakala na matokeo yake malalamiko yapo kwa wagombea walioshindwa ukiwemo wewe?

Tulisimamisha wagombea 244 lakini hatukuwawezesha fedha wagombea wetu wa ubunge kutokana na ukata katika chama. Fedha zipo lakini mwenyekiti na sekretarieti yake walikataa kutoa fedha hizo ili zikatusaidie na badala yake zimeendelea kupelekwa kwenye miradi binafsi ya viongozi.

Wabunge wetu walichangishwa kwa muda wa miaka mitano kwa sababu ya kuandaa fedha za kampeni lakini muda ulipofika hawakurudishiwa fedha zile hivyo kushindwa kuzunguka na kuomba kura.

Tujitafakari Wanachadema na viongozi wetu wametuangusha. Tunaamini walijua hawawezi kushinda ndio sababu.

3. HATUKO TAYARI KUANDAMANA WALA KUGOMA
Kura tumepiga tukimchagua kiongozi ambaye kwa miaka mitano amejinyima na kukaa na sisi Watanzania kwa kuijenga nchi yetu iweze kujitegemea. Tukitegemea uje na sera nzuri za kuboresha maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kuendelea kupunguza utegemezi ila muda mwingi wa kampeni zako ulitumia kuisema CCM kwa kusema unataka maendeleo ya watu na si vitu ili kuenda kinyume na mengi makubwa yaliyofanywa na CCM kuboresha barabara, shule, zahanati. Hali hii ilitufanya tujiulize maswali mengi juu ya uwezo wako.

Pia ulitumia muda mwingi kueleza ulivyoshambuliwa lakini sisi wafuasi wako tulitaka kujua utafanya nini ukichaguawa au kwanini tukupe dhama ya uongozi wa nchi? Ulishindwa kujibu maswali hayo na badala yake ulitumia muda mwingi kuonyesha umma wa wanachadema na Watanzania kuwa unaonewa. KWA MAELEZO HAYA HATUWEZI KUANDAMANA KABISA KWA AJILI YAKO.

4. CHAMA HAKIKUJIANDAA KUHUSU WEWE
Sisi Wanachadema tumechoshwa na maandalizi duni ya chama hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Pamoja na malalamiko ya kutokuwa na fedha. Zipo taarifa kuwa wewe haukuandaliwa kugombea na ujio wako hakukubalika katika chama hadi kufikia kukataa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni zako.

Pia, ushirikiano wako na viongozi wa juu wa chama haukuwepo na hawakuonekana katika mikutano yako. Kwetu sisi kama wanachadema tuliona ni tatizo kubwa sana. Taarifa tulizopata zilionyesha kuna mgogoro mkubwa wa maslahi ndani ya chama na mwenyekiti hakukukubali ndio maana hakuweza kukusaidia kampeni zako.

5. UNATUMIKA NA MATAIFA MAKUBWA KUHATARISHA AMANI YA NCHI
Tunafahamu wewe ni mwanasheria mzuri wa kimataifa. Kwa nini umlete Robert Amsterdam aje kama mwanasheria wako? Je, kuna maslahi gani amekuja kuyasimamia? Tumekuwa tukipinga sana ushoga na zipo taarifa kuwa umedhaminiwa na mataifa makuwa ili ukipata uongozi uidhinishe ushoga na kuuza madini yetu nje ya nch na ukishindwa uanzishe hata vurugu kwa mgongo wa demokrasia ili kutufikisha kama Libya ambako wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi sasa. Leo, Robert Amsterdam yupo Uturuki akisubiri Watanzania tupigane kwa uchochezai aliouandaa kupitia wewe. Tunakushauri kaungane naye tu muendelee na maisha yenu.

HITIMISHO

Tanzania itabaki kuwa nchi ya amani na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kamwe hatutakubali kununuliwa kwa bei yeyote tupo macho.

NI SISI WANACHADEMA KANDA YA KASKAZINI
Sawa. Sahihi. Tundu lisu amekuta nchi iko smart na well organised. Haamini macho yake.
 
Akubali haya matokeo uchwara ya kupika
Screenshot_20201029-225300.png
Screenshot_20201029-225254.png
Screenshot_20201030-152323.png
IMG_20201030_151047.jpg
IMG_20201030_151037.jpg
 
Back
Top Bottom