Ndugu yenu nafilisika very soon

nanonya

Senior Member
Sep 3, 2014
151
277
Kijana nimejichanga hela kidogo nikaagiza mzigo wa simu na bidhaa zingine kutoka china kupitia shirika la usafirishaji wa DHL,sasa biashara yangu hii naona karibia nafilisika kabisa kutokana na kodi ninazolipa TRA.

Sasa wadau naomba njia yoyote itakayoniwezesha mimi kukwepa kodi au kuniwezesha nipunguze kiasi cha kodi nacholipa.

Nalipa kodi halali ila kiasi ni kikubwa sana kinaniumiza kwa kuzingatia Biashara hii yangu bado ndogo.

Nakaribisha maoni yenu na hata watakaonipa ushauri PM kunisaidia mimi mdogo wenu njia za kuweza kukwepa kodi.

Ahsante na karibuni.

tax_confused.jpg
Note: mambo ya #escrow pia yananipa machungu. :confused2:

cc: you
 
Sasa kufundishwa kukwepa kodi ni somo karibia la miezi 6 au mwaka. Kodi inapigwa kwenye faida yako sasa faida = mauzo - manunuzi, sasa hapo kwenye uwe mjanja kwenye kuongeza vigharama vinavyohusiana na manunuzi ili upunguze net profit. Halafu unaweza kutumia wahasibu wenye mauzoefu yao watakujuza zaidi
 
Kodi halali itakuumizaje mkuu?? Ama ulidanganya mapato yako kwa maafisa wa TRA ili uonekane Billionea

Mkuu kwa taarifa yako wakwepa kodi ndio wanafanikiwa sana, hiyo halali ndo nataka kuikwepa kabisa...
makampuni yanabilisha majina kukwepa kodi, na mimi nipeni mbinu....
 
Sasa kufundishwa kukwepa kodi ni somo karibia la miezi 6 au mwaka. Kodi inapigwa kwenye faida yako sasa faida = mauzo - manunuzi, sasa hapo kwenye uwe mjanja kwenye kuongeza vigharama vinavyohusiana na manunuzi ili upunguze net profit. Halafu unaweza kutumia wahasibu wenye mauzoefu yao watakujuza zaidi

ahsante coz wewe umenielewa vizuri kabisa...
vp kodi ya kuingiza bidhaa nchini nayo naikwepa vipi?
 
Mkuu kwa taarifa yako wakwepa kodi ndio wanafanikiwa sana, hiyo halali ndo nataka kuikwepa kabisa...
makampuni yanabilisha majina kukwepa kodi, na mimi nipeni mbinu....

Basi tusilalamikie wale waliotuibia pesa za ESCROW maana wote nyie ni wahujumu uchumi
 
Labda wewe ni wa TRA au huwajui hao TRA. Yaani wanavyofanya assessment ya kodi unaweza ukabwaga mizigo airport. Just unrealistic kabisa. Mali uliyonunua $3,000 watakwambia ina thamani ya $8,000

hahahaha sasa mkuu wao si wanapiga kwa market value. Kama ulinunua Galaxy ya mchina kwa laki 2 wao watakupigia ulinunua kwa price ya OG Galaxy laki 9...
 
mkuu nenda chanika kuna dokta kifimbo hulipi hata kodi na mzigo unakuja dukani kwako ulitaka namba yake nitakupa.
 
hahahaha sasa mkuu wao si wanapiga kwa market value. Kama ulinunua Galaxy ya mchina kwa laki 2 wao watakupigia ulinunua kwa price ya OG Galaxy laki 9...

Market value walifanya wapi research? Kuchukua MSRP kutoka kwenye kwenye google? Bila kujali "factored in" taxes za kule Marekani iliko google?
 
kwanini documents zangu za manunuzi wanazikataa? kwanini watumie market value zao?
Maskini kweli ntabaki kuwa masikini tu ila matajiri kina African Barrick na Tigo wao wanabadilisha majina tu...
 
Ukitaka kuwini Bongo cheza dili na wale magwiji.

Wewe watafute wataalam wa hio biashara wakupe maujanja.

Kifupi Tanzania mfanyabiashara anaelipa kodi kiuhalali ni wa kutafuta na tochi.
 
Market value walifanya wapi research? Kuchukua MSRP kutoka kwenye kwenye google? Bila kujali "factored in" taxes za kule Marekani iliko google?

Mkuu Price si ziko online, Ukinunua Toyota Rav 4 model fulani si wao wanaangalia kwenye websites za Toyota tu wanapata actual cost?? Au ulitaka wao wafanyaje labda??
 
Kijana nimejichanga hela kidogo nikaagiza mzigo wa simu na bidhaa zingine kutoka china kupitia shirika la usafirishaji wa DHL,sasa biashara yangu hii naona karibia nafilisika kabisa kutokana na kodi ninazolipa TRA.

Sasa wadau naomba njia yoyote itakayoniwezesha mimi kukwepa kodi au kuniwezesha nipunguze kiasi cha kodi nacholipa.

Nalipa kodi halali ila kiasi ni kikubwa sana kinaniumiza kwa kuzingatia Biashara hii yangu bado ndogo.

Nakaribisha maoni yenu na hata watakaonipa ushauri PM kunisaidia mimi mdogo wenu njia za kuweza kukwepa kodi.

Ahsante na karibuni.

View attachment 205505
Note: mambo ya #escrow pia yananipa machungu. :confused2:

cc: you

tafuta ashomile yoyote aliekula escrow awana hiana kukusaidia
 
Back
Top Bottom