Ndugu yangu wa damu hana uaminifu kwenye pesa, amenidhulumu mara kadhaa

new level

JF-Expert Member
Apr 21, 2021
269
567
Wakuu hopefully amjambo ngoja niende kwenye point ..

Nina Kaka yangu ambae ndie first born wafamilia .. nashindwa kumuelewa kabisa .. kila Ela yangu ikipitia mkononi mwake hua airudi Ni Mara kwa Mara ili tatizo linajirudia ..

Mwaka Jana nilikuw na kias cha pesa over 700k pesa niliotaka ku boost kwenye biashara yangu ila kutokana na janga la Corona business yangu ilisuasua kidogo nikahmua kumpa brother ili anitunzie adi Mambo yatakapo kaa sawa kwakuwa brother anabiashara kubwa niliamin itakuw rais kwamimi kuchukua iyo pesa yangu pindi nitakapoitaji .. kuliko kukaa nayo bila kuifanyia kazi

Kipindi Mambo yamekaa sawa nilimuomba brother iyo pesa ila ikawa Dana Dana yani niliumia Sana na kwavile siwez mpeleka brother mahakaman nikahmua kupotezea

Me nikijana ninaye taka kusogea mbele kila siku ivyo nilipoanza Maisha ya getto nilianza navitu vyakawaida I mean kitanda Cha mbao vikombe vya plastic navitu vingine cheap Sana .. nikaona siyo sawa aiwezekani nikulie kweny ivyo vitu adi Sasa pia niendelee navyo ..nikaona iko haja yakubadili mazingira ..

Ilipongia January mwaka huu nikahnza kubadili kitu kimoja kimoja na deadline yangu ilikuw mwezi huu wa 11 niwe nimeshamaliza ilo zoezi namshukuru mungu nimeweza kwa kias fulan nilitoa kitanda Cha mbao nikaweka Cha kisasa tv flat subufa DStv sofa zakisasa toa toa ma tray ya plastic Kama kwa mama recho dressing salon nikaweka kabat lavyomb kabati la nguo show case .. nimepambana Sana ili kuleta hayo mabadiliko ..

Sasa kilicho nileta uku Ni ili la mwezi wa 9 kunamtu nilikuw namdai pesa 300k pesa ambayo ilikuw ndo itimisho la malengo yangu ya mwaka huu Ela niliotaka kununua dressing table .. ili 2022 ni fight nakitu kimoja tu KIWANJA ..

Sasa uyo jamaa niliekua namdai Kuna siku hakupokea sim yangu bahati mbaya nilikuw karibu na brother ikabidi nimuombe brother sim ili nione Kama atapokea nilivyo piga sim akapokea akadai nimpe namba ya wakala kwavile brother hua ananamba ya uwakala ikabidi nimtajie iyo number .. kweli akatuma na brother kweli akaniambia katuma ila 295k na siyo 300k Kama ilivyo takiwa nikaona siyo mbaya .. Sasa brother akasema nisubiri adi jion mahna ndo atakuw amepata cash ikabidi niingie zangu mishe jion naenda kuifata iyo Ela nakuta kashafunga nikampgia sim akasema utaijia kesho ..

Kesho yake akaniambia amesafiri mahna hua Ana office nyingne mkoa mwengine kufupisha story huo ndo ukawa mwisho wamatumain ya iyo Ela na matumaini ya undugu wangu kwake ..

Ivi ma brother wadogo zenu mnataka tuishije au furaha yenu nikutuona tunalala seblen kwenye makochi yenu kila siku ?

Nakumbuka kipindi naenda kupanga getto nilienda kwa shemeji mke wa brother kumuomba ndoo moja yakuifadhia maji nilishangaa alininyima live akat amejaza mandoo Kama yote ndan aisee ..

Yani inanikata mood kitu nilichotaka kukamilisha ndani ya muda husika ila Sasa naona naendanacho tena adi mwaka ujao ..

Kama kunamtu ameshawai kupitia changamoto izi za ndugu Tena wa dam anishauri namna naweza jikwamua kwenye ili tatizo mahana naona kabisa next time tutafika pabaya Sana.. Asanteni ..
 
Izo ni dharau , ingekuwa mimi kingenuka mzee , hiyo hela ingerudi kivyovyote "tena ningeenda kumdai huku nimeuvua kabisa undugu.

Haiwezekani ya kwako yaende yangu yasimame, eti kisa kaka " kaka gani mpumbavu ivo

Kaka yupo kwa ajili ya kuwaweka wadogo zake kwenye ramani na sio kuwatoa kwenye ramani ....
 
Yani nikimuwazia hua naumia Sana Yan mtu amekuzidi kila kitu ila Bado tu anataman ubaki Apo Apo au kurudi nyuma kabisa
 
Kuna rafiki yangu mmoja yalimkuta kama yako mpaka sasa hana ham na kaka yake wa damu, na sina imani kama watazikana.

Kipindi Ruby inatoka kweli kweli Montepues Ruby maning, miaka ya 2013 mpaka 2015.

Nakumbuka jamaa alikuta na mgao wa USD 170,000. Kama milioni miatatu na chenji juu.

Jamaa kwafura alisivusha pesa zote mpaka TZ, na kumkabidhi kaka yake kwalengo wafungue biashara ya magari ( kwa mujibu wake mwenyewe)

Kaka mtu alipo ipokea ile pesa akatimukia zake Kenya, ambako anaishi mpaka leo na maisha yake ni mazuri, wakati mtafutaji wa pesa hizo tunateseka nae huku mpaka leo.

Kiufupi usimuamini mtu kwenye mambo ya pesa.
Kama umeweza kuitafuta pesa, inakushinda vipi kuihifadhi mpaka umpe mtu akushikie?
 
Izo ni dharau , ingekuwa mimi kingenuka mzee , hiyo hela ingerudi kivyovyote "tena ningeenda kumdai huku nimeuvua kabisa undugu.

Haiwezekani ya kwako yaende yangu yasimame, eti kisa kaka " kaka gani mpumbavu ivo

Kaka yupo kwa ajili ya kuwaweka wadogo zake kwenye ramani na sio kuwatoa kwenye ramani ....
Tuheshimu kaka zako, sisi ndio tulikua tunakubeba kipindi bimkubwa anafua.
 
Tuheshimu kaka zako, sisi ndio tulikua tunakubeba kipindi bimkubwa anafua.
"Ukiniheshimu ntakuheshimu mbona , tena ntakupa majina yote mazuri yakuhusuyo kaka.

Ila ukiniona wa nini mi ndo huwa na dharau kupitiliza....
 
Kuna rafiki yangu mmoja yalimkuta kama yako mpaka sasa hana ham na kaka yake wa damu, na sina imani kama watazikana.

Kipindi Ruby inatoka kweli kweli Montepues Ruby maning, miaka ya 2013 mpaka 2015.

Nakumbuka jamaa alikuta na mgao wa USD 170,000. Kama milioni miatatu na chenji juu.

Jamaa kwafura alisivusha pesa zote mpaka TZ, na kumkabidhi kaka yake kwalengo wafungue biashara ya magari ( kwa mujibu wake mwenyewe)

Kaka mtu alipo ipokea ile pesa akatimukia zake Kenya, ambako anaishi mpaka leo na maisha yake ni mazuri, wakati mtafutaji wa pesa hizo tunateseka nae huku mpaka leo.

Kiufupi usimuamini mtu kwenye mambo ya pesa.
Kama umeweza kuitafuta pesa, inakushinda vipi kuihifadhi mpaka umpe mtu akushikie?
Binadamu wengine sijui wana roho za aina gani, unaweza hisi huyo sio ndugu wa damu
 
Broo wako anadharau sana inawezekana anafanya hivyo kwakua anaona hutamfanya kitu na siku utakapo amua kumwanzishia varangati ndo siku mtakayoa acha kuangaliana usoni

Kiufupi hata huyo aliekua na hiyo laki 3 yako alikua anaelekea kukutapeli ndo mana hata ungepiga Mara 20 asingepokea

Hapo unajiuliza kwenye hizo biashara zake huyo broo ako hapati pesa mpaka achukue zakwako?
 
Back
Top Bottom