Cendy
JF-Expert Member
- Mar 28, 2015
- 1,249
- 2,307
Kuna rafiki yangu mmoja ameniuliza kwa nini mwl haujatuelimisha chochote kuhusiana na kesi ya makosa ya mtandao iliyofunguliwa Arusha.
Nikamjibu, mara nyingi kesi ikiwa mahakamani unatakiwa kutoa maoni yako tu kimtazamo pasipo kuingilia uhuru wa mahakama.
Akaniuliza tena swali nadhani la mtego ili nami nijikute matatani sijui, eti kama ungekuwa unamtetea yule kijana, utetezi wako ungesimamia nini? Au je kama ungekuwa mwendesha mashtaka mashtaka yako yangesimamia nini hasa?
Nikaguna kidogo halafu nikasema hebu ngoja nianze na hiyo ya mwisho ambayo kidogo iko straight foward. Huyu kijana hakuwa yeye ndo aliyeanzisha post, hilo kwanza ulijue wewe unayependa kutukana kwenye post za watu. Aliyepost alitaka kufahamu comparison kati ya Nyerere na JPM. Huyu ndo akaja na maneno yake ya bwege na siasa za maigizo. Tukumbuke kuwa waliocomment inawezekana walikuwa wengi lakini huwezi kuwa na utetezi wa kuwa wengi pia wamesema. Polisi wanakamata yule ambaye kesi yake inaushahidi wa kutosha.
Akaamua kunipa swali la nyongeza, sasa mwl wao wamejuaje kuwa bwege ndo Rais? Nikacheka kidogo, nikamuuliza hivi kwa mfano nikikuuliza pombe na mke ni kipi kizuri? Wewe ukajibu acha kufananisha vitu vya kijinga na pombe, mimi nina haja ya kujiuliza vitu vya kijinga umemaanisha nani? Obviously unaiangalia comment kulingana na context, namaanisha mazingira husika. Nikamwambia, unajua kesi ingekuwa ngumu sana upande wa waendesha mashtaka kama yule kijana ndo angeanzisha post ikiwa na neno bwege na nyerere na siasa za maigizo. Hapo usingejua amesema bwege ni nani. Sasa yeye alikuwa anajibu swali lililoulizwa na mtoa post ambaye alitaja comparison kati ya nani na nani. Ndo maana imekuwa rahisi kumfungulia mashtaka.
Akajibu aaaaaaaahaaaaaaa. Haya, sasa wewe ndo wakili ingekuaje katika utetezi?
Nikamjibu kwa kifupi kuwa subiri kama yule kijana ataniletea hiyo kesi uje mahakamani kuona nitakavyomtetea mteja wangu. Manake kila mtuhumiwa is Innocent until proven guilty.
Tukumbuke kuwa upande wa mashtaka unatakiwa kuthibitisha pasina shaka yoyote kuwa kuna kosa limetendeka na aliyetenda ni mteja wangu (they have to prove beyond reasonable doubt) na kuwa alikuwa na nia ovu. Kwa mujibu wa media, Kijana ameanza kwa kukanusha inawezekana ndivyo alivyoshauriwa, na amefanya vyema kulingana na ukweli anaoujua yeye. Lakini utetezi uko mwingi sana kisheria na wakati Mwingine unaweza kujitoa ufahamu kulingana na mazingira ya kesi ukasema kuwa unakubali kilichopostiwa na kwamba unaamini ni cha kweli. Inakuwa ni wajibu wako kuthibitisha kuwa hayo uliyosema ni ya kweli na ukimaliza upande wa mashtaka utatakiwa kuthibitisha kuwa si kweli. Hiyo inahitaji kujitoa ufahamu mkubwa. Lakini pia unaweza kusema kuwa sio wewe uliyepost, kuna mtu katumia jina lako kufungua account mtandaoni au accout yako ilikuwa hacked na mtu usiyemfahamu. Hayo yote yatatakiwa kuthibitishwa, n.k. Tuisubiri mahakama ipokee ushahidi na mwenendo wa kesi, tutapata mengi ya kujifunza katika matumizi ya mtandao na sheria zilizopo.
Basi tukaishia hapo nikamwambia tu kuwa makini sana usimkashifu mtu au serikali kwenye mitandao ya kijamii. Angalia mtu asikupanikishe mtandaoni ukaanza kuporomosha matusi yasiyoendana na uwezo wako wa kiakili. Hata kama wamarekani hawaipendi sheria yetu, sisi bado tunayo na tunaitumia ikibidi.