Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Km hujui cha kufanya sikushauri upokee hizo pesa..kaa chini waza cha kufanya na utakachoweza...usingie ingie tu kokote...kwenye biashara inaweza toweka yote usijue imeenda wapi..km bado hujajua vzr cha kufanya




By the way hizo hela sasa..tungepata sie ambao tyr tuko kitaa tunachakarikaa
Bonge la bingoo...
Wenye idea hawana hela
Wasio na ideas hela wanazo daaah

Mungu nijalie muujiza atokee mfadhili baishara zangu zikue
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Ulianza kuajiriwa mwaka gani?
 
Wewe unaakili kumzidi mtu alie ulaya ? Unachokiwaza wewe yeye yuko mile 100 mbele.
Je akimwita huko ulaya akae miezi 5 hivi huoni utapeli wake utajulikana.
Yani mtu anakupa mill 200 halafu unawaza kumfanyia utapeli hujui kuwa utapoteza.
Kwani kuwa ulaya ndo nini jmn.?
Ni makazi tu
Unaweza mzidi akili and that is obvious
Akikuita kwani lazma uende?
Si unapiga chenga.,biashara nani atasimamia huku?
Nnachokataa ni mtu kukupangia maisha

Ht km anakusaidia
Asaidie alale mbele mi nipambane na mbinu nnazo amini kwa hapa bongo ntatoka
 
Wewe jamaa sijui hujui kiswahili, kaambiwa achague kimoja tu.
Mshauri jambo moja tu aaache kazi au aziache milioni 200. Mwenye hela yake kesha toa masharti .
Ni kweli katoa masharti ila ni magumu..
Aache kazi biashara ikimshinda?.!

We talking abt a backup plan
 
Mkuu mie ni graduate, lakini sijasomea mambo ya biashara, na sijawahi kufanya biashara yeyote ile. Niliwahi kulima mazao nikafeli vibaya mno hata hela ya mtaji haikurudi kutokana na kuanguka kwa soko la mazao
Graduate yoyote anatikiwa awe na akili hasa za kufanya alysis, research nk.
Nachosema mitaani kwetu hakuna watu wengi wenye mitaji ya milioni 200 wengi tuna tumitaji tudogo hao wanaokwambia ni hela ndogo wemgi hawajawahi shika hata cash 20milioni.
Tafuta wataalamu wa biashara wenye uzoefu wa kusimamia biashara wakuongoze, mtu ambae hajawahi wekeza biashara ya pesa kama hio atakupa uahauri wa kukisia tu.
 
Screenshot_20211230-184220_Instagram.jpg


mdanganye umeacha akutumie mpunga, tengeneza apartment kama hizi nne ule hela isiyo na usumbufu.

biashara ngumu sana ni bora ungekuwa unafanya biashara inakuwa rahisi lkn hizi biashara za kuanza bila kuwa na uzoefu nayo mara nyingi huanguka.
 
Naomba kujua mambo yafutayo (1) Profession yako na experience yako ni katika nini, (2) Umebakiwa na miaka mingapi kabla ya kustaafu (range inaweza kutosha) (3) Ulikulia mazingira ya mjini au shamba na ni mkoa gani?
 
Biashara ya madini itakutoa faster mkuu, japo ni biashara ambayo inahitaji muda wa kujifunza kwanza kabla hujaianza,, Ndani ya miaka miwili nakuhakikishia ni lazima utakua mbali sana.
 
Jf inakuja juu sana kwa fictional threads.

We are tired of listening of lies.

Nyuzi za uwongo wa kutunga ni nying sana.
na jukwaa la MMU ni kinara.
 
Kuna mdau katoa hapo ushauri wa 150m bonds 50m biashara
Ila mi nashauri na kazi usiache
Raha ya utajiri ni double or triple sources of income
1.bonds
2.biashara hio ya 50m tafta kitu simple tu kiwe kinaingiza hela ya kawaida tu
3.usiache kazi km unaipenda

Ndugu foji mabarua nk
Yaani mnavyomshauri na mimi ninayetaka kumpatia huo mtaji nafuatilia kwa ukaribu huu mjadala wenu! Yaani aniletee documents fake? Nitakuwa namna ya kumdhibiti! Bora kama anaona kazi ya kuajiriwa ni bora kwake basi asichukue hela yangu!
 
Yaani mnavyomshauri na mimi ninayetaka kumpatia huo mtaji nafuatilia kwa ukaribu huu mjadala wenu! Yaani aniletee documents fake? Nitakuwa namna ya kumdhibiti! Bora kama anaona kazi ya kuajiriwa ni bora kwake basi asichukue hela yangu!
Anamwaga ugali unamwaga mboga sio?
Uwekezaji wa bonds ni uhakika
Stress free money na anaendelea kufanya kazi na kabiashara pembeni
Vipato 3 huoni ushamkomboa mwenzio?.!
Acha ubinafsi mkuu
 
It seems huna experience ya biashara yoyote, biashara ya mazao utafirisika ndani ya mwezi, biashara ya kilimo ndio kabisa utakufa na presha ndani ya wiki...
Bora ujenge Lodge zako 3 za maana sehem 3 tofaut yaaan mfano moja tabata, kimara na goba.
Au jenga shule mbili za Day Care sehem mbili tofaut, hii haitaji utaalam zaid ya kusimamia tu watoto wafikishwe center salama wacheze wale walale wajifunze na warudi nyumban salama...
Ukitoka kazini unazungukia lodge zako na Daycare zako. Kwani usipo acha kazi atajua, foji documents za kuacha kaz muonyeshe. Million 200 ni ndogo sana kama una mipango mizur ya biashara unayoijua... Lakini pia 200M ni nyingi kama hujui uzifanyie nini, hivyo ni rahisi kuisha ndani ya muda mfupi na hakuna cha maana ulichofanya...
 
Pesa bwana unaziona nyingi ukiwa hujazishika ila ukizishika sasa zinayeyuka hata hujui zimepotelea wapi.
Yes..hizi ni kauli za watu wengi wasiokuwa na ulewa na masuala ya ,biashara,uwekezaji na uchumi mkuu!
 
Usiwekeze kwenye kilimo usiwekeze kwenye daladala.
Nunua ardhi sehemu potential ambapo ardhi ni ghali angalau eka moja kwa milioni 10 unapata eka 20.Zisajili kata viwanja panga mitaa chonga barabara weka nguzo za tanesco kila plot,weka plot number hapo hapo fungua ofisi huku ukianza mradi wa matofali na vifaa vya ujenzi.Anza kuviuza viwanja hivyo kwa cash na Mkopo KILA eka moja gawa viwanja 6 uza milioni 10 KILA kiwanja so heka moja unapata milioni 60 so kwa heka 20 utapata bilioni 1.2 unaendelea kununua mashamba mengine kwa plan hiyo hiyo.Ndani ya miaka 2 sio wewe tena.
Real estate ukiijulia inalipa sana.
Hii aina stress wala hasara we Kazi yako ni kuwapigia tu simu wateja.
Hakuna kupewa hati bila kumaliza kulipa, unaruhusiwa kujenga huku ukiendelea kulipa sharti vifaa vya ujenzi ununue kwangu.
Real Estate,

Real Estate

Real estate..!!!

Hapa hakuna hasara ..

Umakini unaohitajika nikuangalia maeneo mzuri jirani na mazingira rafiki kwa makazi au biashara!!

Zungumza na wamiliki halisi nunua kiwanja kwa bei ndogo , kiboreshe..!

Pia unaweza ukawa unanuua nyumba nzuri zinazouzwa ..unaziboresha kidogo kisha unapingashisha!!

Huu ni uwekezaji utakokufanya uje kuwa billionaire, trust me
 
It seems huna experience ya biashara yoyote, biashara ya mazao utafirisika ndani ya mwezi, biashara ya kilimo ndio kabisa utakufa na presha ndani ya wiki...
Bora ujenge Lodge zako 3 za maana sehem 3 tofaut yaaan mfano moja tabata, kimara na goba.
Au jenga shule mbili za Day Care sehem mbili tofaut, hii haitaji utaalam zaid ya kusimamia tu watoto wafikishwe center salama wacheze wale walale wajifunze na warudi nyumban salama...
Ukitoka kazini unazungukia lodge zako na Daycare zako. Kwani usipo acha kazi atajua, foji documents za kuacha kaz muonyeshe. Million 200 ni ndogo sana kama una mipango mizur ya biashara unayoijua... Lakini pia 200M ni nyingi kama hujui uzifanyie nini, hivyo ni rahisi kuisha ndani ya muda mfupi na hakuna cha maana ulichofanya...
Hizi lodge tatu za maana kwa milioni 200 na day care ni za aina gani?
Mbona na wewe unaongea kama hujaona hela hiyo iliyoandikwa. Milioni 200 ufanye yote hayo. Unajenga nini? Kua serious alafu ni seniour member wa JF
 
Exactly! Nina hofu kubwa mno ya kufeli. Nina mke na watoto wadogo
Ukifukuzwa kazi hapo sasa hivi utafanya nini? Utaishi vipi? ,
Ukipoteza uwezo wa kufanyakazi ,ukastafishwa itakuwaje?

Ama kweli "Rat Race is for real".. ..

Mentality yako ina kuaminisha kwamba

Money = salary earned from Job

Haya sasa itakuchukuwa miaka mingapi ? kufanya kazi kwa mshahar wako wa ...

1.5mil - (toa kodi, na expenses, bills zako) ili kupata 200mil...???
Na baada ya kupata hizo 200mil utakuwa umeshapoteza na kusota kwa miaka mingapi??

KUMBUKA TIME - Muda ni kitu cha thamani sana kwenye maisha ya mwanadamu.. ishi sasa usije baadae kuona jmehangaika na kazi na msoyo weee na bado hujawahi kuinjoi maisha hata kidogo
 
Real Estate,

Real Estate

Real estate..!!!

Hapa hakuna hasara ..

Umakini unaohitajika nikuangalia maeneo mzuri jirani na mazingira rafiki kwa makazi au biashara!!

Zungumza na wamiliki halisi nunua kiwanja kwa bei ndogo , kiboreshe..!

Pia unaweza ukawa unanuua nyumba nzuri zinazouzwa ..unaziboresha kidogo kisha unapingashisha!!

Huu ni uwekezaji utakokufanya uje kuwa billionaire, trust me
Huwezi pata maeneo jirani na watu kwa bei rahisi
 
Back
Top Bottom