Ndugu wengine wana roho mbaya, hawataki wageni.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,597
154,865
Umekuja mjini kwa ajili ya kushughulikia udahili wa chuo.
Ndugu uliyefikia kwake anakunyima chakula, anakwambia kwake ni marufuku mgeni kuangalia tv, kusikiliza redio, kuchaji simu wala kupiga pasi.
Hayo ndo yaliyomkuta dogo mmoja toka Kigoma, na amefikia kwa kaka yake wa damu moja.
 
Inawezekana yeye anajua huyo ni kaka yake damu damu lakini kumbe mwenzake kaambiwa na mama yake kuwa baba yake ni tofauti na aliyekuwa akimdhania ni baba yake
 
sasa udahili wa mtihani na kugusa gusa tv na radio za watu
ambao pengine wamekopa saccos ndo wamenunua vinahusu nini

yeye ajihusishe na kilichomleta tv za watu asiguse
 
sasa udahili wa mtihani na kugusa gusa tv na radio za watu
ambao pengine wamekopa saccos ndo wamenunua vinahusu nini

yeye ajihusishe na kilichomleta tv za watu asiguse

helooo, mkopo wa sakos unanunulia tv ya mchina? Unalo.. Limekuganda ndiii
 
Umekuja mjini kwa ajili ya kushughulikia udahili wa chuo.
Ndugu uliyefikia kwake anakunyima chakula, anakwambia kwake ni marufuku mgeni kuangalia tv, kusikiliza redio, kuchaji simu wala kupiga pasi.
Hayo ndo yaliyomkuta dogo mmoja toka Kigoma, na amefikia kwa kaka yake wa damu moja.
Hayo yote kwenye RED....si kitu kama kweli unazingatia ulichokifuata hapo kwa ndugu.
Mvumilivu ula mbivu...daima.
 
....kuchaji simu, kupiga pasi.. Hapo kama huja add salt basi huyo ndugu ni soo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom