Ndugu wengi wenye uwezo mkubwa kipesa hawatakagi mazoea na ndugu wenye uwezo mdogo kiuchumi

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,402
Nimekua niki-observe hili swala kwa mda mrefu kidogo na kwenye familia nyingi tofauti, utakuta ndugu wenye uwezo mkubwa kipesa wanawatenga ndugu wenzao wasio na pesa kinamna flani, sio kwamba wanawatenga kabisa..hapana..misiba na sherehe za harusi watahudhuria, michango watachangia, ila mazoea na ndugu wengine wenye kipato cha chini hawataki kabisa..mazoea kama ya kupiga story zisizo na kichwa wala miguu kwa lisaa lizima, friendly gossip, kutaniana na kucheka pamoja, kutembeleana cku ambazo si za sikukuu (yani cku za kawaida), kujuliana hali etc

Wakati ndugu wengi wasio na uwezo mkubwa kiuchumi wako more friendly, mtapiga story lisaa lizima, mtacheka na kutaniana, mtatembeleana akija kwako utamkaribisha fresh, atakula msosi na kushiba, ukienda kwake atakukaribisha vizuri. utakula ushibe, tena ndugu asie na uwezo atakuomba ww uende kwake umtembelee...mm kwa mtazamo wangu huu ndo undugu halisi.

Especially ndugu wengi wenye uwezo mkubwa wa kipesa wanaoishi dar ndo wana tabia hizo, ndugu mwenye uwezo mkubwa kipesa hata akikuruhusu umtembelee na akikukaribisha msosi wake unaona hii karibu haitoki rohoni, hii nimei-observe kwenye familia nyingi.
 
Of course nashukuru mungu hua ninawapa ndugu zangu wote Hera nikipata kea nyakati tofauti tofauti
Siku nne zilizopita numetembeza misimbazi kwa Bibi zangu wote wawili,mzaa mama na mzaa baba....
Sio mda nlikua nnawaza Kama dk20 nyuma nkipata Tena hata misimbazi
Nipasue tembo kwa dogo wa mwisho na Mtoto wa uncle kaka ake mama
 
utajiri humpa mtu ubisy ambao humfanya asiishi kimazoea tena, hapa ndo wengi huona mabadiliko kwa watu hawa coz hawawezi ishi kama ulivowazoea na hapa wengi ndo hudhani hawa watu wamewatenga.

hata nawe ukizipata hutoishi kimazoea kama unavoishi sasa, hii ndo tofauti ya maskini na tajiri
 
Eh huu ndio uungwana, hata siku ukikwama hutumii nguvu kupata msaada. Hizo ndio amali zenyewe sio mtu akipata hela anajitenga maisha yakimshinda ndio anakuja kutia huruma.

Ukiwa na kwako pia unaweza ukawa unaandaa gatherings za ndugu zako walioko karibu. Sometimes mnachinja nyama mnakula mnatia story jioni kila mtu akiondoka anaondoka na furaha na kujiona kweli ana ndugu. Hii ndio style ya ndugu wa baba kuanza baba mkubwa mpaka mdogo wa mwisho.

Hawatupani yani mpaka wote wamefika 60's wana upendo wa hali ya juu regardless ya kutofautiana vipato. Kingine saidia katika strategic issues kama elimu ama mambo ya mitaji ama ajira. Utabarikiwa sana.
 
Nitaleta mada humu niwafundishe kuhusu madaraja/matabaka/classes katika maisha.

Kuna poor class, working class, middle class, high class.

Mtu yoyote akihama kwa kupanda au kushuka kwenye hayo matabaka tabia hubadilika.

Hata tajiri akifulia huwa tunamuona kama kichaa fulani hivi.

Na maskini akipata hela hivyo hivyo anahama class anajenga urafiki na matajiri wenzie.

MATABAKA HAYAKWEPEKI. FANYA KAZI KWA BIDII NA WEWE UANZE KUTAFUTWA NA NDUGU ZAKO.
 
utajiri humpa mtu ubisy ambao humfanya asiishi kimazoea tena, hapa ndo wengi huona mabadiliko kwa watu hawa coz hawawezi ishi kama ulivowazoea na hapa wengi ndo hudhani hawa watu wamewatenga.

hata nawe ukizipata hutoishi kimazoea kama unavoishi sasa, hii ndo tofauti ya maskini na tajiri
Yes. Sababu utajiri una require bidii ili uweze kuhifadhi. Ndio maana wenye mafanikio wana fight al the time wasishuke
 
Eh huu ndio uungwana, hata siku ukikwama hutumii nguvu kupata msaada. Hizo ndio amali zenyewe sio mtu akipata hela anajitenga maisha yakimshinda ndio anakuja kutia huruma.

Ukiwa na kwako pia unaweza ukawa unaandaa gatherings za ndugu zako walioko karibu. Sometimes mnachinja nyama mnakula mnatia story jioni kila mtu akiondoka anaondoka na furaha na kujiona kweli ana ndugu. Hii ndio style ya ndugu wa baba kuanza baba mkubwa mpaka mdogo wa mwisho.

Hawatupani yani mpaka wote wamefika 60's wana upendo wa hali ya juu regardless ya kutofautiana vipato. Kingine saidia katika strategic issues kama elimu ama mambo ya mitaji ama ajira. Utabarikiwa sana.
Nashukuruu mkuu,maana Hawa dadazetu nimeona kiwingu tu
Ukiwapa ndugu wanakubariki mno,wanaelewa ugumu wa maisha na unapata zaidi na zaidi,
Hakuna Hera nliwah kuitoa nkaja kujutia
Hua zinarud fasta Sana......
Ila haya ma mbalaula ndio tatizo....unaweza mpa akampa wakwakwehivi umenielewa mkuuExtrovert
 
Wengine wakijua undani wako umekarisha husuda na matokeo yake utayaona kwa mitihani utakayopitia!

Labda inategemea na makabila na aina za watu!
 
Isipokuwa unapojaliwa nafasi kumsaidia ndugu ni jambo jema sana!
Lakini msaada siyo mpaka aje nyumbani maana unaweza kumsaidia akiwa mbali.
 
Nashukuruu mkuu,maana Hawa dadazetu nimeona kiwingu tu
Ukiwapa ndugu wanakubariki mno,wanaelewa ugumu wa maisha na unapata zaidi na zaidi,
Hakuna Hera nliwah kuitoa nkaja kujutia
Hua zinarud fasta Sana......
Ila haya ma mbalaula ndio tatizo....unaweza mpa akampa wakwakwehivi umenielewa mkuuExtrovert
Hahaaaa mpe mamako, Ila usitake vitu vya hao wadada sasa
 
Nashukuruu mkuu,maana Hawa dadazetu nimeona kiwingu tu
Ukiwapa ndugu wanakubariki mno,wanaelewa ugumu wa maisha na unapata zaidi na zaidi,
Hakuna Hera nliwah kuitoa nkaja kujutia
Hua zinarud fasta Sana......
Ila haya ma mbalaula ndio tatizo....unaweza mpa akampa wakwakwehivi umenielewa mkuuExtrovert
Hao hawafadhiliki
 
Back
Top Bottom