Ndugu wauawa wakijaribu kupora baiskeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu wauawa wakijaribu kupora baiskeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  NDUGU wawili akiwamo mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lukangao katika Manispaa ya Sumbawanga wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wameuawa na wananchi na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya jaribio lao la kutaka kupora baiskeli kugonga mwamba.

  Aidha, marehemu hao pamoja na majeruhi wote ni wa familia moja wakiwa ni wakazi wa Kitongoji cha Bangwe katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, iliwataja waliokufa kuwa ni Geoffrey Kanoka (22), George Kanoka (19), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili wa Lukangao.

  Kamanda Mantage ilimtaja majeruhi mmoja kuwa ni Dk. Kanoka Mwanandenje, aliyepatiwa
  matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa na kuruhusiwa huku jina la majeruhi mwingine likiwa halikupatikana, na hali yake ni mbaya na amelazwa katika wadi ya wagonjwa mahututi.

  Akifafanua tukio hilo, Kamanda Mantage alisema lilitokea baada ya Geoffrey kufika eneo la Miti Mirefu lililopo katika Kata ya Katandala, baada ya yeye na wenzake kutoroka baada ya kumvamia mwendesha baiskeli kwa nia ya kumpora baiskeli hiyo na ndipo wananchi walipomzingira na kuanza kumshambulia.

  Wakati akishambuliwa na wananchi, Kamanda alidai Geoffrey aliwaeleza wananchi kuwa yupo tayari kuwapeleka na kuwaonesha nduguze wengine wanaoshirikiana katika uhalifu.

  Aliwapeleka nyumbani kwa kaka yake, Dk. Kanoka wanapoishi kifamilia na walipofika hapo, mwanafunzi huyo ambaye naye aliuawa, alifungua mlango wa nyumba yao baada ya kusikia kelele za wananchi.

  Mwanafunzi huyo alipoona wananchi wanaendelea kumshambulia kaka yake, aliingilia ugomvi huo kwa lengo la kumsaidia nduguye, ndipo wote wakaambulia kipigo kilichosababisha mauti
  yao.

  Kamanda Mantage alifafanua kuwa Dk. Kanoka wakati akijaribu kutoroka, alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali mkononi na mdogo wake ambaye jina lake halijafahamika, naye akijaribu kutoroka, alipigwa na jiwe kichwani na kuanguka mbele na wasamaria kumuokota na kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
   
 2. damtu2

  damtu2 Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  inakuwaje watu wanaruhusiwa kuua wenzao kwa ajili ya baskeli. ikowapi sheria? mbona tunachezea roho za watu hivi? disgusting
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tatizo wakipelekwa kwenye vyombo vya sheria, wanaachiwa!
   
Loading...