Ndugu wana JF ni mabadiliko gani yaliyotokea Tanzania kupitia jukwaa hili? Embu tujitathmini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu wana JF ni mabadiliko gani yaliyotokea Tanzania kupitia jukwaa hili? Embu tujitathmini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by everybody, Nov 15, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kusema la ukweli huwa wakati mwingine nakaa na kutafakari ni jinsi gani mtu unaweza kuingia pale ikulu na kumwambia yule bwana mkubwa Rais kwamba hali huku mtaani imekuwa ngumu na tunataka mabadiliko ya kweli. Ni muda mrefu hili jukwaa la Jamii Forum limeanzishwa ila nashindwa kuona ni kwa jinsi gani ambavyo tumeweza kuleta mabadiliko katika utendaji wa viongozi wa nchi yetu.

  Huenda kuna mabadiliko ambayo yameshatokea siku zilizopita ambayo yametokana na mijadala yetu humu JF. Ila kwa upande mwingine naona kama hawa viongozi wa serikali yetu wanaishia kuyasoma maoni yetu na kuyaweka kapuni na kuendelea na style yao ya kucheza ngoma waliyofundishwa toka utotoni.

  Naomba wana jamii forum tujitathmini na kujadili ni kwa jinsi gani hili jukwaa limeweza kuleta mabadiliko katika utendaji wa nchi yetu. Kama kuna mifano halisi tuwekeane humu walau itasaidia kututia moyo wengine tunaokaribia kukata tamaa ya mabadiliko katika hii nchi yetu kuona kwamba kumbe kelele, mawazo na mapambano yanayoendelea humu JF yanasidia kubadilisha tabia zilizoshindikana za viongozi wetu.

  Tujadili.
   
Loading...