Ndugu wa mume ndiyo hawa au kuna kitu nakosea?

mamii90

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
380
265
Habari,

Hili jambo limenitesa miaka nenda miaka rudi, natamani lifike mwisho.

Wakati naingia kwenye mahusiano na huyu ambae ni mume wangu sasa, alikuja binti mmoja ambaye alikuwa ndo kamaliza form 4 (mdogo wake) akaanza kusoma cozi kwenye chuo flani.

Nikapata ujauzito so ikabidi nilete binti wa kazi. Na mimi katika maisha yetu nimelelewa na mabinti wa kazi, sipendi wateseke kabisa maana niliona walivyomsaidia mama enzi tunakua, so shida ikaanza anamuachia yule binti kila kitu afanye, hadi ampikie amuamshe chumbani, yale mambo yalikua yananikera nikaanza kumsema kwa nguvu sana, hakubadilika. Ikabidi nimwambie kaka yake. Kaka yake akasema kama unamuona msichana wako anapata shida basi nitamuekea msichana wake yeye

Ile hali ikaendelea sana kwa muda na yule binti alikua mdogo kwa hiyo ikabidi niwe napika mwenyewe, siku zikaenda akaja tena mdogo wake wa kiume, wote kazi ikawa ile ile, huyu wa kiume hadi anamwambia dada amfulie nguo. Nilikua naongea napiga mzigo nadeki mpaka mimba ina miezi nane ndo mama angu akaja.

Kiukweli niliteseka mimba ya huyu mtoto, ugomvi ndani ya nyumba hautuliii kabisaa; wakaungana wote na mama zake kwamba niachike. Na kweli mume wangu akasema natamani kukuacha ni vile tu tumefunga ndoa.

Hapo nimeskip kipindi cha ndoa maana tulifunga ndoa tayari huyu binti tunaishi nae kuna mengi yalitokea lakini nitaeleza tu tukio moja.

Usiku wa kesho yake ndio ndoa akaniambia kwa hiyo kwenye hiyo saluni uliyofanya booking na mimi nitasuka? Nikamwambia ni maids tu wewe hautaenda pale, aliangua kilio imagne na kuna wageni, mume wangu haya maswala ya maids hajui anasema kwanini unaenda kuremba watu baki unamuacha huyu? Akaninuia tumeenda kusameshana wakati wakuvalishana pete ya ndoa.

Unaweza ukahisi movie ila sio movie ni maisha watu tunapitia.

Wakati wa sherehe huyu binti na wenzake kwenye ile meza ya wazazi wangu hawakupeleka vinywaji kabisa maana wao ndo walikua kwenye hiyo kamati ya vinywaji na mama zake wadogo.

Sasa huyu binti alikuja baadae kwenda hostel mimi mimba ikiwa kubwa kama miezi 8 ambapo na mama ndo akaja. Sasa wakati wa X-mass maana ilikuwa hata bado sijajifungua kaka yake akampigia simu aje kula sikukuu nyumbani, hakuja kabisa akaenda kwa dada mmoja ambae alikuja baadae kuwa mtu wa karibu na mimi. Huyo dada akamwambia mbona hujaenda kwa kaka kula sikukuu? Akasema, KAJAZA NDUGU ZAKE SIWEZI KWENDA PALE.

Kiukweli alikua kaja mama yangu na mjukuu wake na mdogo wangu, alikuja kusalimia, nikihesabu muda kwa ujumla waliokaa pale ni kama wiki tatu, dogo akaondoka na mimi nikawa nimejifungua nikakaa wiki2 nikaondoka na mama kurudi nyumbani.

Sasa imagne watu hawajakaa hata mwezi yeye kaona kero ila wenyewe miaka nenda rudi wapo.

Alikuja kumaliza chuo ila hakupata kazi, akaenda kwao akarudi tena akasoma tena akamaliza hakupata kazi. Na hii ya mara ya pili, wembe ukawa ule ule, hafanyi chochote analala tu dada amfanyie kila kitu.

Sasa hii mara ya tatu anasoma tena ila anawahi kuondoka asubuhi jion kuna siku anachelewa kuna siku anawahi kurudi, ila ndo hivyo hasaidii chochote, yaani dada ndo afanye kila kitu.

Namuuliza anasema naoshaga sahani yangu pekee. Namuuliza na hivyo vingine anasema nawahi kuamka kwa hiyo siwezi.

Leo mpaka naandika niko bize napika yeye amekaa anachat, nikamwambia mimi siwez kukupikia wewe unachat hapo jipe shuhuli wala hajanisikia kitu. Kaenda kununua chips.

Mbaya zaidi nyuma ya pazia kuna rafiki yake mume wangu wametafutana wanapanga yao huko (na huyo kaka alihusika sana kwa yule baby mama wa mr kumuondoa)

Na kingine kikubwa ni kwamba mama yake anaona kawaida tu hata ukimwambia.

Ashawahi iba nguo zangu akaenda kugawa, aliyempa akapiga picha akaweka Insta nikaiona ile nguo nikambana akasema alimpa, nikamwambia akaifate akampigia mama ake na mama ake akasema muulize (yaani aniulize mimi) hiyo nguo ni bei gani atume ela.

Nimeruka mambo mengi ila kuna dada wa saluni pia alishawahi kuniita akaniambia kuwa makini na huyu binti anaweza akakuua.

Sasa ndugu zangu nifanyaje hapa, wako wawili yeye na huyo shemeji wote wanataka tuwahudumie kama ambavyo namuhudumia kaka yao yaani mimi na dada ndo tuwafanyie kila kitu.

Na kingine kikubwa ana mawasiliano ya karibu mno na yule dada aliyezaa na mume wangu pamoja na yule aliyehusika kupika figisu.

Nifanyaje kuimaliza hii nightmare wandugu maana kila nikimuona anapita nakumbuka machungu hasa enzi za mimba maana ilikua niachwe kwa sababu yake.

Roho inaniuma, nina uchungu sana

=======
Michango ya wadau
Mpendwa
Pole kwa unayopitia,
Naomba kujua maswala mawili ambayo hujayaweka wazi sana
Je huyo mwana mke aliezaa na mumeo mahusiano yao yalidumu kwa muda gani na ilikua ni baada ya ndoa yenu au labla?
Na sababu ya kuachana nae ilikua nini?

Pili, wewe na mumeo mlikutana mkapendana wenyewe au mlilazimishwa na wazazi?

Cha kukushauri, kweli huwa tunaolewa kwenye familia za watu na tunakutana na ndugu wenyw tabia tofauti, cha msingi ni kutumia busara kuliko kutumia nguvu au hasira

Jaribu kutafuta better moment, ongea na mumeo, ikiwezekana hao ndugu muwatafutie shughuli ya kufanya ili waweze kujitegemea badala ya kuwategemea nyinyi

Msipofanya hivyo, hamuwezi kutatua mgogoro uliopo kati yenu na ndoa yenu haitapata amani

Usichukue hasira, enedelea na majukumu yako kama mke, wapikie wakaribishe chakula, ondoa vyombo, maana hapo ni kwako.

Jaribu kuepuka mambo ambayo yataleta ugomvi kati ya mumeo na nduguze

Ila tafuta muda uongee na mumeo hao ndugu wapate cha kufanya ila na nyinyi mpate nafasi ya kufanya maisha yenu

Mumeo ana makosa makubwa na inawezekana kuna mengi nyuma ya pazia yanaendelea kati ya mumeo na nduguze, pengine mumeo bado ana mahusianonna huyo mwanamke alise zaa nae na ndugu wapo upande wake, jaribu kuchunguza na uwe makini katika kila step

All in all mahusiano yakisha fika stage hiyo, mkiona mmeshindwa kuzungumza mkaelewana, watafute watu wa karibu yenu, ikiwezekana hata marafiki ambao wana hekima, wajaribu kuzungumza na mumeo kujua shida ipi wapi@mamii90,


Pole kwa yanayokusibu!
Kwa ridhaa yako naomba kusema nawe mambo machache yafuatayo.

Mosi: nilichokiona ni ushindani kati yako na upande wa mmeo kuonesha ni nani mwenye haki zaidi. Unapoingia kwenye ushindani huo unakuwa umejiondolea mamlaka yako ya umama wa familia.

Ulichopaswa kufanya ni kutoshindana nao, wachukulie ni wapitaji tu na hawataishi hapo milele, lakini pia kumbuka kuwa wewe huwezi kuwa mkamilifu tu na wao ndo wakosaji tu. Kuna pahala hata wewe unakosea na kuwakosea. Shida kubwa inakuja pale kila upande unapong'ang'ania mtazamo wake wa usahihi wake hata kama hauko sahihi.

Pili unaonekana kuwa mtu asiyesamehe na kusahau mambo, badala yake unaendelea kuorodhesha na kuongezea yale waliyokukosea. Hili linakufanya uone ubaya tu na pia unazidi kujijaza chuki na hasira. Mwisho wa siku utajifukuzisha mwenyewe.

Cha kufanya, samehe yote kwa dhati na sahau, jitahidi kuona uzuri na mazuri yao hata kama ni kidogo. Jenga mtazamo chanya na usiweke maneno akilini mwao. Acha kuongozwa na hisia hasi dhidi yao.

Kuhusu mmeo, huwezijua amefikaje pale alipo, kwa hiyo inawezekana amebebwa na familia kwa namna ambayo hawezi kuilipa. Mazingira ya hivyo yanaweza kumjengea upofu, na pengine ndiyo maana kila ukimshirikisha matatizo ya nduguze anaona kama unamtenganisha nao.
Kwa upande huu, ongea na mmeo kwamba umeamua kuondoa tofauti zenu ili muanze upya. Na baada ya hapo onesha upendo wa dhati siyo wa kuigiza dhidi ya mmeo na nduguze pasipo kujalisha matatizo na mapungufu yao.

Pia keti na ongea na wifi na shemeji uwaambie nia yako ya kuishi pamoja kwa upendo na amani. Onyesha kutambua hali iliyokuwepo ya nyote kutopendana na kwamba hujaona manufaa yake ndo maana umeamua muondoe tofauti zenu. Eleza kwa uwazi wapi walipokuwa wanakukwaza na pia wape nafasi ya kueleza ulipowakwaza pia.

Muhimu, hao ni wapitaji. wewe, wanao na mmeo ndo wa kudumu pale. Hata wasipofanya kazi sawa we fanya kwani hapo ni kwako na kazi ni zakwako, jua ni suala la muda tu wataondoka na kukupisha. Acha chuki, puuza yote hata kama wakifanya kituko cha makusudi usigadhabike, hilo ndo lengo lao kukuudhi ili ufanye makosa na hivyo ujifunge bao la ushindi kwao.

Usiwape hiyo nafasi. Nimeandika haya kuongea na wewe na haina maana kuwa sijayaona maumivu yako. Samehe bure tena hata kabla ya kukosewa kwa vile kukosewa kupo tu upende usipende.

Mungu na akujalie hekima, busara na ustahimilivu katika haya mazingira magumu unayopitia.
I.......


Kwakeli dada kazi unayo unayo. Isingekua kiapo cha ndoa ningesema utoke hapo kwa mme wako na mwanao ukajitegemee kama unajiweza kwa masharti kua kurudi ni mpak Awatoe hao ndugu zake.

Ila kingine kama utaweza mshauri mumeo awatafutie ndugu zake kazi au biashara halafu iwe mbali na hapi home kwenu itapunguza ujinga wanaoufany Na wataanza kua busy na maisha yao.

Kingine mwambie dada wa kazi afanye kazi zinazo mhusu tu, maswala ya kuwaulia nguo zao aache na ww ingilia kati, usikubali wafuliwe nguo na dada wa kazi. Majukumu yao wafanye wenyewe.

Kwa sababu Mume yupo upande wao usipeleke mashitaka kwa mme wako tena Waache tu, na kwa vile hawakuheshimu na wala hawaoni umuhimu wako na ww toa umuhimu wao kwako usiwategemee kwa chochote kile, pia punguza huduma unazojitole Kwao kama sio kuacha kuwahudumia kabisa, isipokua chakula tu ambacho anatoa kaka yao. Pia hakikisha mahitaji yao yanatoka kwa kaka yao tu. Usitumie pesa yako kwao, lazima wataanza kuona tofauti.

Usijishushie thamani kisa mume ambae anamwanamke mwingine ambae anampa furaha, maumivu ni yako hakuna cha kuhofia hapo, mume mwambie ukweli kua kuanzia sasa ahudumie mwenyewe ndugu zake kama hawatakubali kukusikiliza mama wa nyumba na kama hata kubali kukusikiliza basi awahudumie yeye.

Jukumu lako lipo kwa mume wako, hao ndugu zake ni huruma zako mwenyewe ambazo mwisho wa siku unaishia kuwalaumu kwa ujinga wako (am very sory kwa kusema ujinga wako) ila unaonekana mjinga kwa kua upo concerned kwao. Acha kua concerned sana kwao usijitolee hakikisha wanakula tu, inatosha hayo mengine usishughulike nayo. Nadisitiza mwambie dada wa kazi asiwafanyie chochote kile akatae kabisa na wala asiogope.

Nb: kitu ambacho hukijui ni kua sisi wanaume huwa tunapata wakati mgumu kuamua nani nimsikilize kati ya mke niliyekutana nae ujanani na ndugu zangu nilikua nao na mama yangu mzazi aliye nizaa. Nafsi zetu zinashikwa sana na mama zetu na ndugu zetu hasa wa kike. Hivyo unatakiwa kua na msimamo imara usiyumbe watakuelewa, au waamue kuondoka au kubaki.
Kama watabaki badi wakusikilize na wafanye yale unataka kana hawataki watoke tu.
 
Nakumbuka kuna siku niliamka njaa inaniuma enzi hizo nina tumbo langu nikakpika mtori.

Huyu binti akaamka jua linawaka kabisa akawa anakunywa chai hapo kaka yake akapita akamuona akauliza mbona huli mtori, hakujibu kitu, basi kuna mahali tulikua tunaenda jamaa alikimbiza gari mpaka nilitamani kushuka.

Kumuuliza eti ananiambia kwanini ujawapikia wadogo zangu, sa hiyo tumbo liko kuleee. Binti wa chuo nimpikie, nikamwambia anashindwa nini kupika mwenyewe? Jamaa akasema mpikie wewe.

Mwanangu anaelekea miaka miwili ila haya mambo yananipa uchungu huyu binti sitaki hata kumuona akikatiza ndani.
 
Daaaah pole sana. Wanapokukera na wewe ukakereka wanafarijika sana.

Fanya unaloweza hasa kwa mumeo na watoto, hao wengine achana nao, jifanye huwaoni. Mawifi n mashemeji hao mara nyingi ni wivu unawasumbua wanaona unafaidi cha kaka yao.

Kuna siku wataondoka tu. We kama unapika chakula cha wote pika tu. Dada afanye kazi zinazomhusu tu. Furaha jipe mwenyewe, jifanye huwaoni ingawa ni ngumu ila ukizoea watanunde. Hahahah
 
Just potezea, jifanye fala, dunia ndo itanyoosha.
Atasoma hata mara hamsini, kazi olaa, umri unaenda hajapata mume, mvivu. Kiufupi anaweza asioleke na ndo atatia akili.

Mwache tu, akifika miaka 60 bado yuko hapo, huyo kashindikana.
 
Kuna Nyuzi mbili niliziandika nikashambuliwa kwa matusi ddq haya ndio madhara. Kwa mwanamke kabla hujaolewa na jamaa hakikisha unaijua Vizuri familia yake ndio maana kuna kipindi cha uchumba. Hzii feelings zinafanya maisha yenu yakose furaha ndoa inakuwa kama kageleza. Nyumbani kwako panakuwa kama utumwani. Poleee
 
msindikizaji,
Anaeteseka ni dada kwa hiyo inabidi nifanye tu na mimi.

Ila kikubwa ni ninayakumbuka mateso yote aliyonipitisha kadri navyozidi kumuona.

Mi mwanangu kaungua sana tumboni ana mabaka baka meusi mengi tu miguuni.

Nina uchungu juu yake nahisi ndo maana hapati hata kazi na juu ya hilo anavyozidi kufanya mambo yake hapa ndo ananikumbusha machungu mengi ya nyuma.
 
Elungata,
Nasema hivyo kweli yaani nasema mateso aliyonipitisha uchungu anaonipa naona ndo maana hapati kazi.

Na ninasema akija kuolewa naomba ayapitie machungu ninayopitia mimi.

Yaani dada wa kazi ananiambia huyu akija kupata ela akiajiri msichana wa kazi atamtolea hadi chupi amfulie.
 
Pole Sana dada, japo uandishi ulkuwa unanichanganya sometimes but nmekuelewa sana. Ndoa ni uvumilivu wa hali ya juu sana, kwa ninachokushaur naona n bora uvumilie tu. Ikiwezekana mfanyie hayo anayotaka huyo wifi tena bila kinyongo kwa sababu huyo ni mtu wa kupita tu nayeye ataolewa hlf ndio atajua nn maana ya majukumu ya mwanamke.

Wewe usigombane nae tena kisa usafi wa vyombo na kupika, fanya kila kitu, fanya Kama unaish na kilema, akiolewa dunia itamfunza vema kabisa. Wew baki na mmeo na usishindane na mwanadamu.
 
Glenohumeral joint,
Asante sana kwa ushauri hayo yanavumilika ila kuna figisu nyingi nimeskip sijaandika.

Kuna siku aliamka usiku kujiandaa kwenda huko anaposoma akafungua bomba la chooni akaacha wazi na la nje akaacha wazi dada anakuja aamka maji yameshatoka kama lisaa hivi.

Bill ilikuja kama elfu 60 hivi ya maji.
Nilikuja muuliza kwanini anafanya hivi haya mambo akakana akasema hajaacha maji yeye. Ila kuna siku anatoka kuoga na dada ndo anaingia bafuni akakuta bomba linamwaga tu maji ndo nikambana kwamba anafanya makusudi na sio kupitiwa.

Embu niambia nifanyaje jamani moyo unashindwa kuyabeba yote haya
 
Hamna binadamu anayestahili kupitia haya unayoyapitia. Pole sana.

Nimekosa nguvu pale mume anapojuta hata kwanini alikuoa. Kwangu kitu kama hiki nakiita RED FLAG, ni ishara mbaya sana. Ni makosa sana pale mume wako anakutamkia maneno magumu kama hayo na ana side na wadogo zake kwenye tabia ambazo zinapaswa kukemewa vikali.

Natamani nikushauri maamuzi ambayo ingekuwa ni Mimi ningeyachukua ila naogopa. Kumbuka siku zote usipuuze hizi red flag/ishara za hatari.

Kaa na mume wako mweleweshe asipokusikiliza na kukuheshimu basi utafanya vile 'roho wa bwana atakavyokuongoza'.
 
Pambana na mwili upate ushindi wa kiroho, ushauri wangu kwako wewe vumilia tu huyu ni Mgeni atapita tu na hayo ndiyo matatizo yetu ya Mfumo wa kuwa tegemezi wa akili mpaka mwili sema tu namshangaa huyo mwanamme mwenzangu kuwa anasikiliza kila anachoambiwa na ndugu zake

Au haukuwahi kumweleza kinaga ubaga kwamba mambo unayotendewa na ndugu zake haufurahishwi nayo

Sometimes Ndoa ni Ndoano, gangamara na kupigania kwako huku duniani kupokelewa ni ngumu
 
mamii90, Inabidi umwachilie asikae ndani ya nafsi yako, unavyomfikiria na kufikiri wewe ndie mshindi nawe unamkosea Mola.

Umeshauriwa utafute kuwapotezea, acha kuwalalamikia na waombee msamaha kwa Mola.

Usipowaachilia kwenye moyo wako ukawa unawawaza, shetani anapata penyo kukuvuruga zaidi. Na huyo wifi wanakufanyia zaidi, sababu unaongea sana nao kulalamika.

Mama wa baby wao, unampa nafasi pia kuendepea kuwepo. Mke mwenza. Sali omba toba na waachilie, salia hapo kwako.

Mpe mzigo wako Mola, pika chakula cha wote acha roho mbaya wewe si umewazidi au?

Be free Be happy utaugua bure. Sali fungua redio ya dini usikilize maombi.
 
Back
Top Bottom