Ndugu wa mume kuwasiliana na mume tu imekaaje?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,348
40,220
Kumekuwa na tabia ambayo si nzuri kwenye mahusiano, unakuta kijana wa kiume ameoa, ana mke na watoto; Mbaya zaidi ndugu wa mwanaume wanakuwa wanaegemea upande wa mwanaume tu, watafanya naye mawasiliano vizuri ila kwa upande wa mke wa ndugu yao, hawafanyi mawasiliano iwe kwa kupiga simu au kwa kutuma ujumbe wa meseji.

Undugu wa aina hii tunaita undugu wa ki-unafiki, kama mwanaume atakuwa na kipato na hatakuwa makini anaweza kuishia kupigwa mizinga isiyoeleweka na ndugu zake....huku mkewe na watoto wakiwa wako katika hali isiyoeleweka.

Hii inamaana wewe baharia ukifa, mkeo na watoto wako wanakuwa hawana undugu tena na ndugu zako; au wanaishia kwenye manyanyaso ya mashangazi n.k

Kuwa makini na ndugu wanaofanya mawasiliano na wewe tu, bila wao kuwa na ukaribu au mawasiliano na mkeo na watoto wako; hao ni wanyonyaji.
 
Namshukru Mungu kwa hili, mke wangu anahusiano mzuri na ndugu zangu kuliko hata, taarifa nyingi za nyumbani nazipata kupitia yeye, anaweza ongea na wadogo zangu hata masaa 2 kwenye simu.

Tatizo lake wivu.
 
Namshukru Mungu kwa hili, mke wangu anahusiano mzuri na ndugu zangu kuliko hata, taarifa nyingi za nyumbani nazipata kupitia yeye, anaweza ongea na wadogo zangu hata masaa 2 kwenye simu.

Tatizo lake wivu.
Kama kuna uhusiano wa namna hiyo huo ni mzuri
 
Back
Top Bottom