Ndugu wa Mchungaji Nixon Isangya aliyeuawa kinyama walia na ofisi ya DPP kuwahujumu

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mahakama ya hakimu Mkazi wilaya ya Arumeru, imewafutia Mashtaka washtakiwa watatu kati ya wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya Mauaji na kubaki na mshtakiwa mmoja Simoni Kaaya ambaye anatarajiwa kujibu shtaka la mauaji ya mchungaji Nixon Isangya (71) mkazi wa Sakila wilayani Arumeru, mkoani Arusha aliyeuawa kwa kupigwa na kitu Kizito kichwani akiwa usingizini.

Shauri hilo namba 18/2018 lilikuja mahakamani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kutajwa, lakini mwendesha mashtaka wa serikali Grace Medikenya aliieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu, Pamela Meena kuwa ofisi yake haina nia ya kuendelea na washtakiwa watatu kati ya wanne waliokuwa wanakabikiwa na shtaka la mauaji.

Washtakiwa waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Dewario Nderekwa (59)ambaye ni mdogo wa askofu mku Eliudi Idangya ,Joshua Palangyo (42) na Obadia Nanyaro (60) ambaye ni afisa mwandamizi wa kanisa la International Evangelism.

Hatua hiyo imeibua mtafaruku kwa ndugu na jamaa wa marehemu wanaofuatilia shauri hilo wakihoji sababu za washtakiwa hao kuondolewa mashtaka wakati kesi ya msingi bado haijaanza kusikilizwa jambo ambalo wanahisi kuna upindishwaji wa maksudi wa sheria ili kuwalinda watuhumiwa hao.

Dada wa Marehemu Jen Isangya alisikika akilalamika kwamba maelezo ya awali ya washtakiwa hao waliyoyatoa polisi, walikiri kula njama na kushiriki mauaji ya kaka yake Nixon Isangya aliyeuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani akiwa usingizini nyumbani kwake eneo la Moivaro katika jiji la Arusha, April 7 mwaka 2017 lakini anashangaa kusikia Leo eti washtakiwa watatu wamefutiwa mashtaka.

"Mimi nashindwa kuelewa inakuwaje watuhumiwa wa mauaji wanafutiwa mashtaka kienyeji na mwanasheria wa serikali wakati kesi ya msingi bado haijaanza na hata maelezo ya awali ya washtakiwa bado hawajasomewa kuna nini hapo ,hii sio sawa namwomba rais Magufuli aingilie kati kuna rushwa imetembea hapa sio bure"Amesema.

Wengine ambao hawakuridhiwa na maamuzi ya ofisi ya mwanasheria Mkuu hapa Arusha,kuwaondolea mashtaka washtakiwa hao ni pamoja na wanandugu na majirani na marehemu ambao wamedai maamuzi hayo hayakuzingatia uhalisia wa tukio Bali yamezingatia maslahi binafsi ya watu wachache.

Akiongea nje ya mahakammara baada ya kutakiwa kutia ufafanuzi wa hatua hiyo mwendesha mashtaka wa serikali Grace Mesikenya alisema ofisi yake inamamlaka ya kuliondoa shauri mahakamani muda wowote kwani sisi ndio tumefungua shauri hilo.

Awali watuhumiwa hao akiwemo askofu Mkuu wa kanisa la International Evangelism,Eliud Isangya (69) ambaye ni mdogo wa marehemu walishikiliwa na polisi April ,mwaka 2018 kwa tuhuma za mauaji na baadae askofu huyo aliondolewa na kubaki watuhumiwa wanne na sasa amebaki mshtakiwa mmoja Simon Kaaya ambaye anatarajiwa kujibu shtaka hilo la mauaji.

Kesi hiyo inatarajiwa kuja tena mahakamani hapo April 14 mwaka huu.

Kabla ya kuuawa kwa Mchungaji Nixon Isangya anadaiwa kuwa na Mgogoro wa muda mrefu na mdogo wake Elihud Isangya ambaye ni Askofu mkuu wa kanisa la International Evangelism lililopo sakila Wilayani Arumeru kiasi cha wawili hao kutosemeshana.

Inadaiwa kuwa katika hatua ya mwisho kabla ya kukutwa Mchungaji Nixon ameuawa chumbani kwake kulikuwepo na ugomvi wa kugombea wafadhili wa kidini kutoka nje ya nchi ambapo Askofu alikuwa akimtuhumu mdogo wake kumhujumu ili wafadhili wasiendelee kusaidia kanisa lake.

images.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndio chanzo cha kifo? Dunia inaenda kasi sana
Inadaiwa kuwa katika hatua ya mwisho kabla ya kukutwa Mchungaji Nixon ameuawa chumbani kwake kulikuwepo na ugomvi wa kugombea wafadhili wa kidini kutoka nje ya nchi ambapo Askofu alikuwa akimtuhumu mdogo wake kumhujumu ili wafadhili wasiendelee kusaidia kanisa lake.
 
Mahakama ya hakimu Mkazi wilaya ya Arumeru,imewafutia Mashtaka washtakiwa watatu kati ya wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya Mauaji na kubaki na mshtakiwa mmoja Simoni Kaaya ambaye anatarajiwa kujibu shtaka la mauaji ya mchungaji Nixon Isangya(71) mkazi wa Sakila wilayani Arumeru, mkoani Arusha aliyeuawa kwa kupigwa na kitu Kizito kichwani akiwa usingizini.

Shauri hilo namba 18/2018 lilikuja mahakamani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kutajwa ,lakini mwendesha mashtaka wa serikali Grace Medikenya aliieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu ,Pamela Meena kuwa ofisi yake haina nia ya kuendelea na washtakiwa watatu kati ya wanne waliokuwa wanakabikiwa na shtaka la mauaji.

Washtakiwa waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Dewario Nderekwa (59)ambaye ni mdogo wa askofu mku Eliudi Idangya ,Joshua Palangyo(42) na Obadia Nanyaro (60) ambaye ni afisa mwandamizi wa kanisa la International Evangelism.

Hatua hiyo imeibua mtafaruku kwa ndugu na jamaa wa marehemu wanaofuatilia shauri hilo wakihoji sababu za washtakiwa hao kuondolewa mashtaka wakati kesi ya msingi bado haijaanza kusikilizwa jambo ambalo wanahisi kuna upindishwaji wa maksudi wa sheria ili kuwalinda watuhumiwa hao.

Dada wa Marehemu Jen Isangya alisikika akilalamika kwamba maelezo ya awali ya washtakiwa hao waliyoyatoa polisi, walikiri kula njama na kushiriki mauaji ya kaka yake Nixon Isangya aliyeuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani akiwa usingizini nyumbani kwake eneo la Moivaro katika jiji la Arusha ,April 7 mwaka 2017 lakini anashangaa kusikia Leo eti washtakiwa watatu wamefutiwa mashtaka.

"Mimi nashindwa kuelewa inakuwaje watuhumiwa wa mauaji wanafutiwa mashtaka kienyeji na mwanasheria wa serikali wakati kesi ya msingi bado haijaanza na hata maelezo ya awali ya washtakiwa bado hawajasomewa kuna nini hapo ,hii sio sawa namwomba rais Magufuli aingilie kati kuna rushwa imetembea hapa sio bure"Amesema

Wengine ambao hawakuridhiwa na maamuzi ya ofisi ya mwanasheria Mkuu hapa Arusha,kuwaondolea mashtaka washtakiwa hao ni pamoja na wanandugu na majirani na marehemu ambao wamedai maamuzi hayo hayakuzingatia uhalisia wa tukio Bali yamezingatia maslahi binafsi ya watu wachache.

Akiongea nje ya mahakammara baada ya kutakiwa kutia ufafanuzi wa hatua hiyo mwendesha mashtaka wa serikali Grace Mesikenya alisema ofisi yake inamamlaka ya kuliondoa shauri mahakamani muda wowote kwani sisi ndio tumefungua shauri hilo.

Awali watuhumiwa hao akiwemo askofu Mkuu wa kanisa la International Evangelism,Eliud Isangya (69)ambaye ni mdogo wa marehemu walishikiliwa na polisi April ,mwaka 2018 kwa tuhuma za mauaji na baadae askofu huyo aliondolewa na kubaki watuhumiwa wanne na sasa amebaki mshtakiwa mmoja Simon Kaaya ambaye anatarajiwa kujibu shtaka hilo la mauaji.

Kesi hiyo inatarajiwa kuja tena mahakamani hapo April 14 mwaka huu.

Kabla ya kuuawa kwa Mchungaji Nixon Isangya anadaiwa kuwa na Mgogoro wa muda mrefu na mdogo wake Elihud Isangya ambaye ni Askofu mkuu wa kanisa la International Evangelism lililopo sakila Wilayani Arumeru kiasi cha wawili hao kutosemeshana .

Inadaiwa kuwa katika hatua ya mwisho kabla ya kukutwa Mchungaji Nixon ameuawa chumbani kwake kulikuwepo na ugomvi wa kugombea wafadhili wa kidini kutoka nje ya nchi ambapo Askofu alikuwa akimtuhumu mdogo wake kumhujumu ili wafadhili wasiendelee kusaidia kanisa lake.

View attachment 1409399

Sent using Jamii Forums mobile app
DPP office sucks
 
Back
Top Bottom