Dar es Salaam. Familia ya Hamza Mohamed aliyewapiga risasi na kuwauwa askari watatu, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi na kisha naye kuuawa kwa kupigwa risasi, wameeleza kusikitishwa na taarifa kutoka polisi kuwa ndugu yao alikuwa gaidi.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, jana Alhamisi, Setemba2, 2021 msemaji wa familia ya Hamza, Abdulrahman Hassan amesema wamekuwa wakimuona marehemu akiwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa na tabia yoyote ya kigaidi.
‘‘Dah! Sisi tulikuwa tukimuona Hamza kama mtu wa kawaida asiye na mwenendo wa kigaidi, amesema kwa mshtuko.

Kuhusu Hamza kujifunza ugaidi kupitia mitandao, amesema: “Dada….! Hamza anajulikana, watu wamemzungumzia wanavyomfahamu, sisi hatuna cha kuongeza kama polisi wanadai hivyo.’’

Alipoulizwa kama familia inafahamu lolote kuhusiana na viashiria vya ugaidi vinavyodaiwa kuwa Hamza alikuwa navyo, Hassan amesisitiza walikuwa wakimuona Hamza ni mtu wa kawaida na si mwenye nyendo za kigaidi.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS,
msemaji huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya jambo hilo

Maelezo hayo ya Hassan yametokana na taarifa ya polisi iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura ambaye amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Source: Mwananchi
Kwanini Mwananchi hawajamuuliza msemaji wa familia kuhusu iwapo Hamza alikuwa akijihusisha na biashara ya madini au la!
 
Dar es Salaam.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS,

Bado polisi wakamuacha tu akitesa mtaani. Au ndio ile ya kusubiri tukio/uharibifu utokee ndipo matamko yatolewe
 
Hamza hakuwa na viashiria vya ugaidi. Polisi imejitungia ikiamini hakuna wa kuwajibu.
tuna ushahidi na mambo mengi polisi waliyojitungia,mengi sana
Walishawahi kumkamata ndugu yetu usiku wa saa tatu akiwa amelewa,tena nyumbani wakaenda naye
kesho yake wakatangaza wamemkuta kwenye tukio la uvamizi wa duka la hardware akiwa na silaha na wamemuua
 
Aisee poleni sana
 
Kwa
Dar es Salaam. Familia ya Hamza Mohamed aliyewapiga risasi na kuwauwa askari watatu, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi na kisha naye kuuawa kwa kupigwa risasi, wameeleza kusikitishwa na taarifa kutoka polisi kuwa ndugu yao alikuwa gaidi.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, jana Alhamisi, Setemba2, 2021 msemaji wa familia ya Hamza, Abdulrahman Hassan amesema wamekuwa wakimuona marehemu akiwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa na tabia yoyote ya kigaidi.
‘‘Dah! Sisi tulikuwa tukimuona Hamza kama mtu wa kawaida asiye na mwenendo wa kigaidi, amesema kwa mshtuko.

Kuhusu Hamza kujifunza ugaidi kupitia mitandao, amesema: “Dada….! Hamza anajulikana, watu wamemzungumzia wanavyomfahamu, sisi hatuna cha kuongeza kama polisi wanadai hivyo.’’

Alipoulizwa kama familia inafahamu lolote kuhusiana na viashiria vya ugaidi vinavyodaiwa kuwa Hamza alikuwa navyo, Hassan amesisitiza walikuwa wakimuona Hamza ni mtu wa kawaida na si mwenye nyendo za kigaidi.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS,
msemaji huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya jambo hilo

Maelezo hayo ya Hassan yametokana na taarifa ya polisi iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura ambaye amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Chanzo: Mwananchi
Kwa sasa ni busara kuiacha hii familia ipunzike wanapitia maumivu mengi. Japo hili nalo litapita nasi tutasahau na kusubiria tukio lingine
 
Ubalozi wa ufaansa hawajatoa footage? Camera zitakua zimenasa mwanzo wa mtanange
 
Tuseme Hamza sio gaidi haina noma!
Kwa nini alimuua askari wa kampuni binafsi ???ya ulinzi
Hukusikia yule askari wa kampuni binafsi alijiandaa kumshambulia hamza ndio hamza akamuwahi? Nadhani hamza alimuua yule wa binafsi kwakua yule wa binafsi alikuwa anakoki gobole lake ila wale wengine waliuawa kwasababu ndio walikuwa lengo la Ndugu hamza
 
Back
Top Bottom