Ndugu wa Hamza, mhalifu aliyeua Askari Selander bridge watiwa mbaroni na polisi

Hivi kama walitaka kujua mengi ya Kiundani njia sahihi ilikuwa ni Kutomuua Kwanza bali wampige tu Risasi za Miguuni au Mikononi wayajue au Kumuua kisha waanze Kusumbua hivi Ndugu zake? Police wetu ni very unprofessional kwakweli.
Tayari wanajua sababu iliyomsukuma kuwafanyia ugaidi polisi - jambo ambalo hawakulitarajia kabisa toka kwa Mtanzania. Maswali yanayowasumbua sasa ni: wapi na lini alipata hiyo jeuri, mafunzo na silaha (kama si mmiliki halali)?

Watumie fursa hii kujua na kujiandaa kukutana na Watanzania "vichaa" wachache ambao hawatakubali kuwa "wapole" wakidhulumiwa au kunyanyaswa kama wengi tulivyo.
 
Wadau wanasema jamaa si Gaidi ila kuna dhulma kafanyiwa. Sema sina uhakika, lakini polisi wamefanya jambo la maana kuwachukua wanafamilia ili kukusanya dots
Vipi na ile kadi ya uanachama wa CHADEMA umepata majibu yake?
 
Polisi wa Tanzania huo ndio uwezo wao ulipoishia
1629986175712.png
 
Inamaana hutambui polisi waliouawa na hilo gaidi?
Duuh, police wanne wameuawa na sita wamejeruhiwa na mtu moja aliyerusha risasi ovyo juu??? inahitajika mafunzo zaidi, na IGP Sirro (zero) angejiuzulu tu, hakuna jinsi jambazi (kada wa CCM) akiua PolisiCCM. Duuh ni hatari sana haya mambo.
 
Polisi wetu walivyo na uwezo hafifu watamsumbua huyo ndugu hata kama hajui kuhusu tukio alilofanya mtu mwingine.
 
Hawajakurupuka wala hakuna mahala polisi wamesema ndugu wa Hamza ni waharifu. Kuwa chini ya ulinzi au kukamatwa haimaanishi mtu anatuhumiwa.

Nakupa kisa. Nchini Russia mwaka 2014 wasichana wawili wenye asili ya Chechen walitengeneza bomu la kienyeji na kumpa kaka yao aliyejilipua kwenye airport ya Domodedovo (2nd largest in Russia) na kuua watu 32. Hawa wawili walishashtukiwa ila kaka akaachwa. Hata taarifa za FBI na mashirika mengine ya uchunguzi zinaonesha ⅓ ya magaidi wana uhusiano wa kifamilia.

Watatoa taarifa muhimu kama sababu ya kushika silaha, mwenendo wake, hali yake kiakili na mengine. Na pia yawezekana wamekamatwa ili kupewa ulinzi, what if kuna watu wanapanga retaliation kwao
Uko sahihi Hii pia yaweza kuwa ni kwa usalama wa ndugu wa marehemu pia
 
Ndugu wa kijana Hamza aliyeuwa polisi watatu na yeye kuuawa pale daraja la Salenda wametiwa mbaroni na polisi usiku huu.

Ndugu wote wamekamatwa na nyumba yao imefungwa na iko chini ya ulinzi.

Chanzo: Ayo tv
===

kutoka Upanga Dar es Salaam kwenye nyumba aliyokua akiishi Hamza, Mwanaume aliyefyatua risasi na kuwauwa Watu wanne leo Jijini Dar es salaam ( Askari Polisi watatu na Mlinzi wa Kampuni binafsi mmoja).

Polisi wameifunga nyumba hiyo na kuondoka na Ndugu wa Hamza kwenda nao Polisi usiku huu ambapo walifika hapa toka saa kumi na moja jioni, endelea kukaa karibu na AyoTV na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.

olisi wameifunga nyumba aliyokua akiishi Mwanaume aliyefyatua risasi leo na kuuwa wanne Dar es salam, baada ya kuifunga nyumba hii iliyopo Upanga Dar es salaam wameondoka pia na Ndugu wa Mtu huyo aitwae Hamza kwenda nao Polisi usiku huu pamoja na Pikipiki aliyokua akiitumia.

Hamza amekua gumzo leo hii Dar es salaam baada ya kuwaua kwa risasi Watu wanne leo na kujeruhi wengine sita, endelea kukaa karibu na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.
KWA MAKOSA GANI ?
 
ccm polisi ZERO BRAINS
Shukuru kwa yoote mkuu! MMungu ndie Mjuzi wa yoote!
Hujui na mimi sijui kama kwa dhahama hiyo MMungu #Ametuepusha na #janga Kubwa!

1 THE. 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ

[ LUQMAN - 16 ]
Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, Mwenye khabari za yote.
 
Hili linafanyika ili kutoa fundisho kwa mtu yoyote ambaye anataka kufanya ugaidi. Ukifanya ugaidi, utaisumbua na kuiletea matatizo familia yako kwa hiyo ni bora usifanye. Ni aina ya deterrent. Tena afadhali ya Bongo, kule Israel serikali wanavunja kabisa nyumba za familia ya yoyote anayefanya ugaidi ili iwe ni fundisho kwa yoyote anayetaka kufanya ugaidi.
 
Tayari wanajua sababu iliyomsukuma kuwafanyia ugaidi polisi - jambo ambalo hawakulitarajia kabisa toka kwa Mtanzania. Maswali yanayowasumbua sasa ni: wapi na lini alipata hiyo jeuri, mafunzo na silaha (kama si mmiliki halali)?

Watumie fursa hii kujua na kujiandaa kukutana na Watanzania "vichaa" wachache ambao hawatakubali kuwa "wapole" wakidhulumiwa au kunyanyaswa kama wengi tulivyo.
Uko sahihi mkuu.
Hadi sasa hivi bado hawaamini kilichotokea maana wamekariri kwamba Watanzania ni watu wanyonge na wanaweza kuwafanya chochote
 
Ilikuwa ni lazima. Hata marafiki zake nao watatafutwa, hiyo ni njia tu ya upelelezi na kutaka kuujua ukweli.

Haishangazi
Wasiwasahau na viongozi wa CCM ,maana hao ndio walikuwa wanashinda nae na kuzunguka nae
 
Back
Top Bottom