Ndugu wa Hamza, mhalifu aliyeua Askari Selander bridge watiwa mbaroni na polisi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,796
141,693
Ndugu wa kijana Hamza aliyeuwa polisi watatu na yeye kuuawa pale daraja la Salenda wametiwa mbaroni na polisi usiku huu.

Ndugu wote wamekamatwa na nyumba yao imefungwa na iko chini ya ulinzi.

Chanzo: Ayo tv
===

kutoka Upanga Dar es Salaam kwenye nyumba aliyokua akiishi Hamza, Mwanaume aliyefyatua risasi na kuwauwa Watu wanne leo Jijini Dar es salaam ( Askari Polisi watatu na Mlinzi wa Kampuni binafsi mmoja).

Polisi wameifunga nyumba hiyo na kuondoka na Ndugu wa Hamza kwenda nao Polisi usiku huu ambapo walifika hapa toka saa kumi na moja jioni, endelea kukaa karibu na AyoTV na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.

olisi wameifunga nyumba aliyokua akiishi Mwanaume aliyefyatua risasi leo na kuuwa wanne Dar es salam, baada ya kuifunga nyumba hii iliyopo Upanga Dar es salaam wameondoka pia na Ndugu wa Mtu huyo aitwae Hamza kwenda nao Polisi usiku huu pamoja na Pikipiki aliyokua akiitumia.

Hamza amekua gumzo leo hii Dar es salaam baada ya kuwaua kwa risasi Watu wanne leo na kujeruhi wengine sita, endelea kukaa karibu na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.
 
Kama ni kweli huu ni upumbavu wa KUKURUPUKA. Ndugu kuwa mhalifu haina maana ndugu zake wote ni wahalifu labda kama kuna ushahidi wa uhalifu wa ndugu zake. Wakamate na maccm yote basi yaliyokuwa karibu na huyo muuaji.

1629921896157.jpeg
 
Back
Top Bottom