Ndugu na marafiki zako ndio maadui zako wakubwa

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
NDUGU NA MARAFIKI ZAKO NDIO MAADUI ZAKO WAKUBWA

Ndugu zako na marafiki zako wa karibu wanakupenda sana. Ndio maana mpaka sasa mpo karibu na mkishirikiana kwenye mambo mengi.Lakini hawa hawa ndugu na marafiki zako wa karibu, ni maadui wakubwa sana kwako.

KUWA MAKINI, WATU WENYE NIA NJEMA NA WEWE WANAWEZA KUWA MAADUI WAKUBWA.
Sio maadui kwamba wanataka kukuua au kukupoteza, hapana. Ni maadui kwa sababu wana nia njema sana na wewe. Katika nia hii njema wanageuka kuwa maadui.
Ndugu na marafiki zako ni maadui wako pale unapotaka kufanya kitu cha tofauti. Kitu ambacho hakijazoeleka.

Kitu ambacho kimebeba hatari kubwa. Watakushauri sana usifanye, watakusihi sana usiingie kwenye hatari hiyo. Watakupa mifano ya wengine waliojaribu kama wewe na wakashindwa. Na wewe utaona hawa ni ndugu zako au marafiki zako mnaopendana, na utawasikiliza, hutafanya, maisha yako yanabaki vile vile.

Maadui.
Ndugu na marafiki zako ni maadui zako wakubwa sana unapotaka kubadili tabia. Labda kuna tabia ambayo umejijengea, ambayo unaona ni kikwazo kwako kufikia malengo makubwa uliyojiwekea, kwa mfano kukutana kila jioni baa. Kwa bahati mbaya sana, tabia za aina hii hufanyi peke yako, bali na watu hawa wa karibu kwako.

Hivyo ili kuvunja tabia kama hizo, unahitaji kuacha kuwa na watu hawa wa karibu. Sasa utakapojaribu kufanya hivyo, watakuona umebadilika, unajitenga, hutaki kuwa nao na mengine mengi. Na wewe kwa kuogopa kuonekana wa tofauti au hujali, unarudi tena kwenye tabia ile, ukiona unawafanyia wema watu wako wa karibu. Maadui.

Sasa mchezo hauishii kujua kwamba hawa watu wema kwako wanaweza kuwa maadui wakubwa, mchezo mgumu kuliko wote ni wa kuweza kuwashinda maadui hawa. Kwa sababu hakuna vita ngumu kama ile unayopigana na adui anayekujua vizuri.

Anayejua uimara wako na madhaifu yako na watu wako hawa wa karibu watatumia vizuri madhaifu yako ili kuhakikisha huendi tofauti na mlivyozoea.Lakini kama wakale walivyosema, ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni, kwa kuwa sasa umeshawajua hawa ni maadui, na umeshajua wanatumia nini kuendelea kukufanya mateka, basi wakati mwingine utakapoamua kuondokana na kitu USIWAANGALIE USONI.
BAADAE WATAKUELEWA.
 
Last edited by a moderator:
Nimeshangaaa sana hata kina smaki, Mshana jr, Mtalazaki,Nyarusare, Khantwe hawajachangia mada hiii mpaka wa leo!! Maadui hawa siyo wa kunywa Bia tuuu!!

bali wanataka sometimes uharibikiwe kabisa watoto wo ndo wawe juu!! hawataki wala kupendelea unasoma Zaidi ya watoto wao! wla upande Zaidi kimaisha kuwa zidi wao!

hawa hawaui ila cha moto utakiona!! hata kuua ikibidi wanakuchukua msukure!!...na ndg ndo hawahawa wafuga misukule mtu baki hawezi kufanya ivo!! na haohao ndo wanao suka na majambazi mipango ya wewe kuvamiwa!!

wana ujasiri sana!! katka kukuangamiza na watu hao hutakaa uwadhanie hata siku moja ...ukitaka kujua maneno yangu …….kaa peke yako kwa muda flani bila Rafiki wala ndugu uone kama utapata pigo lolote!

Biala haoa utapita katikati ya vibaka na hutaguswa kamwe!! adui mwingine mke!!! huyu ni msema hovyo kwa kila mtu hata adui aweza mtongoza au yeye mwenyewe kakuunganishia uadui kwa majamabazi!! siyo ndg yako!! ni adui huyo!
 
Oh nimeelewa hapo kwenye upendo wa ndugu marafiki vinaweza kukufanya usifike mbali . Ni kama vile mtoto anapoataka kwenda hatua nyingine eidha kutambaa au kutembea mwanzo wazaz mnakua mnamuogopea kua ataanguka mnamzuia zuia kumbe mnamchelewesha.
Safi mada nzuri.
 
Back
Top Bottom