Ndugu Mwenyekiti........Kulikoni?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, maarufu kama AU, Bwana Jakaya Mrisho Kikwete, naomba utege sikio umsikilize Mchungaji.

Najua nimekuwa nikiongelea sana kuhusu mambo ya ndani ya nchi yetu na kukutaka usimame kidete kusafisha uozo ulioleta Ufisadi, Uzemba na Uhujumu. Naam nashukuru kwa taratibu umeeanza kazi.

Lakini safari hii Bwana Muungwana, Mchungaji anaongelea nafasi yako kama Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Kiafrika.

Naomba utumie utashi wako kutatua matatizo ya Afrika bila kumuonea haya mtu!

Ulimtumia Membe kutoa tamko kuhusu Sudan, wakati jirani wa Kenya walipopata msukosuko wakati wa uchaguzi, sauti yako haikusikika. Ukasaidia Serikali ya Comoro iondokane na ugaidi.

Lakini kuna mambo ambayo yanahitaji sauti yako ya ukali na uongozi mahiri ukitumia uzoefu wako katika masuala ya mambo ya nje na kimataifa.

Nakuomba wakati unamalizia muda wako kama Mwenyekiti wa AU, utuletee ufumbuzi Zimbabwe ambako ukatili wa ndugu yetu wa awali wa mapambano, Robert Gabriel Mugabe unatishia si uhai wa Raia wasio na makosa pekee, bali ni hatari kwa usalama wetu kusini mwa Afrika.

Aidha inabidi uwakalishe chini kina Museveni na Kagame na waambie waache kumsaidia Jenerali Nkunda ambaye analeta vurugu Kongo.

Na mwisho, sauti yako inahitajika ma kwa kupeleka Jeshi lakulinda Amani au kuunda kamati ya usuluhishi ili kuleta Amani na kuwepo kwa Serikali katika Jamhuri ya Somalia.

Raila Odinga katoa kauli ambayo inaonyesha ujasiri kwa kutaka Mugabe awajibishwe, swali langu kwako je uko tayari kusimamia haki za binadamu na demokrasia Afrika kwa kumshurtisha Mugabe aachane na ubabe wake

Je uko tayai kuwakalisha chini zile koo pale Mogadishu ambazo sasa zinatambaa Bahari ya Hindi kuteka meli ili Somalia iwe na Serikali?

Je kule Afrika Magharibi anzia Nigeria, Sierra Leone na kwingine utulivu tunaounona ni wa kweli au ni mazugazuga?

Nakuomba basi uchukue hatua kubwa katika uenyekiti wako kuhakikisha unahamasisha uwajibikaji wa viongozi, kuimarika kwa Demokrasia na Kulinda haki za Binadamu ikiwa ni ziada ya cvita ya kutetea maslahi ya kiuchumi ya Afrika.

Ni hayo tuu Ndugu Mwenyekiti.
 
Ni hayo tuu Ndugu Mwenyekiti.

La hasha mtumishi wa Bwana. Si hayo tu. Muagize kwa mamlaka ya Kiroho uliyonayo atatue mgogoro wa nchi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chonde chonde 2010 imekaribia. Mficha maradhi mauti humuumbua. Neno linakupa mamlaka ya kuonya na kukaripia!Onya!Karipia!
 
Nakutaka umwambie atueleze kama wizi wa aina ya Mramba ni Ufisadi , jinai ama ni Uhujumu wa Nchi tafadhali .
 
Nakutaka umwambie atueleze kama wizi wa aina ya Mramba ni Ufisadi , jinai ama ni Uhujumu wa Nchi tafadhali .

Mchungaji kasema mara hii anazungumzia masuala ya kimataifa. Uwe unasoma basi kabla ya kukurupuka!
 
Kudos Mchungaji, Kwenye swala la Mugabe nadhani yule mzee anaogopa nini kitatokea pindi atakapoachia madaraka ndio maana ameamua kugangamara mpaka mwisho...Nadhani hapa cha kufanya kama hakijafanyika ni kumhakikishia huyu mzee kuwa hatoshitakiwa na kuwa ataishi nchi yoyote afrika bila matatizo.
 
Mchungaji kasema mara hii anazungumzia masuala ya kimataifa. Uwe unasoma basi kabla ya kukurupuka!

Kaka sijakurupuka ila nimemuunga mkono mwananchi mmoja kwamba pamoja na yale ya AU bado tuna shida hapa Tanganyika mkuu .Wewe bila kunitaja hupati raha kwikwikwiw
 
Mchungaji kasema mara hii anazungumzia masuala ya kimataifa. Uwe unasoma basi kabla ya kukurupuka!

Kwani hilo la Zanzibar si la kimataifa? Jk si alisema kuna nchi ya Zanzibar na nchi ya tanganyika?
 
Je uko tayai kuwakalisha chini zile koo pale Mogadishu ambazo sasa zinatambaa Bahari ya Hindi kuteka meli ili Somalia iwe na Serikali?

Kati ya yote, hili la Somalia linabaki kuwa doa kwa muungwana kwa sababu it is clear that hajafanya chochote cha maana
 
Nafikiri bado anakosa nguvu za kufanya haya baba mch.Kama nyumbani kwake anaonesha kushindwa atawezaje ya watu? Si hata kwenye biblia Kanisa huanzia nyumbani? Tena kwaya moja iliwahi kuimba baba awe askofu,mama mchungaji na watoto wawe wainjilisti.Si unaona mkuu anaonesha udhaifu nyumbani? Huko nje atawezale? Au ndo nabii hana heshima kwao? Nisaidie Baba Mchungaji!
 
Kudos Mchungaji, Kwenye swala la Mugabe nadhani yule mzee anaogopa nini kitatokea pindi atakapoachia madaraka ndio maana ameamua kugangamara mpaka mwisho...Nadhani hapa cha kufanya kama hakijafanyika ni kumhakikishia huyu mzee kuwa hatoshitakiwa na kuwa ataishi nchi yoyote afrika bila matatizo.

Naomba nitofautiane na wewe hapo. Kwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kukubaliana na yale aliyoyatenda akiwa madarakani. Nchi yoyote ya Kiafrika ikifanya hivyo itakuwa inapiga hatua kurudi nyuma katika mambo ya haki za kibinadamu, demokrasia, na utawala wa sheria.

Huyu Mugabe kakiuka kila aina (kama zipo nyingi) ya haki za kibinadamu. Kavunja misingi yote ya kidemokrasia na utawala wa sheria, kwa nini Waafrika tumpe deal ya namna hiyo huyu mnyama? Just like my gal Hill said, no way, no how, no sweet deal for Mugabe!! He needs to go and go now. After that he needs to face lady justice. Afterall, who is he not face justice after comitting ineffable crimes to innocent people?
 
Nafikiri bado anakosa nguvu za kufanya haya baba mch.Kama nyumbani kwake anaonesha kushindwa atawezaje ya watu? Si hata kwenye biblia Kanisa huanzia nyumbani? Tena kwaya moja iliwahi kuimba baba awe askofu,mama mchungaji na watoto wawe wainjilisti.Si unaona mkuu anaonesha udhaifu nyumbani? Huko nje atawezale? Au ndo nabii hana heshima kwao? Nisaidie Baba Mchungaji!

Calnde,

Nimekuelewa mkuu, ndiyo tunamtaka asawazishe ya nyumbani (nikimjibu Lunyungu), lakini pia si vibaya kumuomba asawazishe yaliyoko nje.

Uenyekiti wa AU ni mara moja na hakuna kupewa tena na waliompa hawana uwezo kuamua kuhusu Urais wake wa Tanzania na hao ninaoomba awashughulikie hawana nguvu za kutusaidia kwa chochote zaidi ya kutuongezea shida.

Kuna ule wimbo Urafiki waliimba wakimuomba Mwalimu Nyerere kama mwenyekiti wa nch zilizo mstari wa mbele, basi kutumia tenzi hizo na umaarufu na umahiri tuliokuwa nao, kwa nini basi Kikwete wetu asitung'arishe kwenye sura ya dunia?

Yanayotokea Zimbabwe, Kongo, Sudan na hata Somalia si mchezo na ni rahisi sana kusambaa ama kuigwa na nchi nyingine.

Raila anapeleka kilio kwa nchi za magharibi ambazo zilikuwa wakoloni zije kusadida suala la Zimbabwe, tujiulize je Afrika tuko wapi? je hata kuleta Amani tuwasubiri wahisani?
 
Huyu Raila na yeye asianze za upambe wake..Mugabe this Mugabe that...Afix kwanza mambo hapo Kenya..Asije akaanza kujiingiza kwenye siasa za makundi na migawanyiko kama walivyozoea huko Kenya...Nilishasema toka awali kuwa matatizo ya Africa ni sisi wenyewe tutayatatua na si kuendelea kuwa vibaraka tu.
Yes Mugabe labda wananchi walio wengi hawampendi tena,lakini mgogoro huo kwanini ulianza baada ya mashamba ya wazungu kugawanywa upya?
 
Mchungaji,

Kudos for good analysis. I once asked, when JK does not take any actions against Mugabe, does it mean that he endorses Mugabe's action? If he does, that means it's okay with him and something like that happens to our country, we shouldn't be surprised...we had clear signs!

Mr. Chairman/Mr. President,

Recently, Tanzanian military have been part of peacekeeping effort in West Africa and even in the Middle East. A lot of lives were lost in these areas and we did our part in peacekeeping process. A few years ago, Tanzanian military members served honorably to liberate our brothers and sisters in the whole Southern Africa region. We have a good history of fighting for those who are oppressed and can't fight for themselves. We also sent our troops to Anjouan in one the most successful military missions.

What I fail to understand, Mr. President, is how you choose your battles. Gen. Nkunda is making the lives of our brothers and sisters in DRC a nightmare. A little further South, tyrant Mugabe's inaction (needs to step down) kills Zimbabweans every single day in scores. People's quality of life has been taken away and some of them are paying the ultimate price, death. Why, Mr. AU-Chairman, are you looking away from these problems? Why have turn into deaf ear? You may argue that AU (or Tanzania, for that case)have a policy of not intervening domestic issues...well, wasn't Apartheid system a domestic issue in South Africa a few years ago? What about the Ngazijas problems?

As Tanzania celebrates its 47th year of independence, we need to send a message to our brothers and sisters in Bulawayo, Harare, Mashonaland, Matebeleland and other parts of Zimbabwe thata we have not foresaken them. We hear their cry, we sympathize with their sorrows, help is on the way. We need to cut ties with Mugabe but not Zimbabweans. We need to send him a strong message that he needs to step down. To paraphrase Madeline Albright who once said to a certain tyrant "you need to step down voluntarily and soon, or be forced to step down and soon" Mugabe needs to be told the same. The lives of Zimbabweans are in your hands, Mr. Chairman, you are the steward of their well-being.

I hope you will use wisdom to evaluate and take actions in timely manner as Zimbabweans face cholera epidemic, food shortage, inflation, oppression and everything that you and I don't wish to experience.
 
Huyu Raila na yeye asianze za upambe wake..Mugabe this Mugabe that...Afix kwanza mambo hapo Kenya..Asije akaanza kujiingiza kwenye siasa za makundi na migawanyiko kama walivyozoea huko Kenya...Nilishasema toka awali kuwa matatizo ya Africa ni sisi wenyewe tutayatatua na si kuendelea kuwa vibaraka tu.
Yes Mugabe labda wananchi walio wengi hawampendi tena,lakini mgogoro huo kwanini ulianza baada ya mashamba ya wazungu kugawanywa upya?

Mushi,

Labda Raila anaweza kumwonesha Mugabe kuwa japo nchi inaweza ikawa na mgawanyiko wa kisiasa, wanaweza kuendesha serikali kwa pamoja kwa kuheshimiana na kwa manufaa ya nchi na si chama wala mtu binafsi. Nafikiri Raila ndio mtu mwenye cred ya kuzungumzia suala hili kwani ni mfano hai.

Kwa suala la matatizo yalianzia wa wapi na baada ya nini, ina maana wazimbabwe hawana kiongozi mwingine anayeweza kutatua matatizo yao isipokuwa Mugabe, au? Ina maana leo Mugabe akifa Zimbabwe itasambaratika? Tusiwafanye wazimbabwe vilaza wa kufikiri na tusilaumu kila tatizo kwa mataifa ya nje. Ni kweli ulivyosema waafrika matatizo yetu tunajitakia na ni budi Mugabe awajibishwe!
 
Kati ya yote, hili la Somalia linabaki kuwa doa kwa muungwana kwa sababu it is clear that hajafanya chochote cha maana
Wala hajathubutu hata kupoteza muda wake kuongelea Somalia zaidi ya suala la utekaji wa meli (pengine kwa sababu meli hizo zinatoka huko kwa miungu-watu). Somalia inasikitisha; hivi hawa jamaa hawajagundua madini/mafuta?!
 
Ndugu Mwenyekiti,

Najua baadhi ya wasaidizi wako wa karibu husoma magazeti ya kimataifa na kukupa nyeti. Je wakupa hii taarifa ya maoni ya leo kutoka gazeti la New York Times? Kama hawajakupa fununu, basi naiweka hapa kila mtu asome jinsi suala la Zimbabwe na Gabrieli wa Mugabe linavyovunda na kulidhalilidha bara letu la Afrika.

http://www.nytimes.com/2008/12/13/opinion/13sat3.html?ref=opinion

spacer.gif

December 13, 2008
Editorial
Nowhere to Hide

Here are the fruits of Robert Mugabe’s rule of horrors: political chaos, economic collapse, desperate food shortages, violence and now a fierce cholera epidemic. Eight-hundred people have died. More than 16,000 are infected, and there is no end in sight.
The increasingly delusional Mr. Mugabe — Zimbabwe’s illegitimate president — announced on Thursday that the cholera crisis is over. Tell that to the Chigudu family which, as The Times’s Celia Dugger reported, lost five children, aged 20 months to 12 years, in a matter of hours. Or to the World Health Organization, which warns that the crisis now poses a regional threat.
Mr. Mugabe blames the West for the epidemic that is spread by water contaminated with human excrement. The blame is all his. Water taps in the capital’s dense suburbs went dry last week, so people could not wash their hands or food. Hospitals are closed. Garbage is everywhere. Sludge spews from burst sewer lines.
The international community must provide emergency shipments of food, water purification tablets and anti-cholera drugs. The United States has allocated another $6.2 million for supplies like soap, rehydration tablets and water containers. Unfortunately, the dying will continue until Mr. Mugabe allows international health care workers to enter the country and do their jobs.
There will be no end to these horrors until Mr. Mugabe is gone. He stole this year’s election and has blocked a unity government. South Africa and other states that insist on an African-led solution to this crisis must stop enabling Mr. Mugabe and lead. They must renounce their recognition of Mr. Mugabe as president and press him and his cronies to cede power. The cholera epidemic, spilling into South Africa and other border states, shows there is nowhere to hide from Mr. Mugabe’s legacy.

Copyright 2008 The New York Times Company
 
Yes Mugabe labda wananchi walio wengi hawampendi tena,lakini mgogoro huo kwanini ulianza baada ya mashamba ya wazungu kugawanywa upya?

Jmushi, usitetereke;

Kwanza si kweli kuwa wana-nchi wengi wa Zimbabwe hawampendi Comrade Mugabe. Wengi tunaoonyeshwa wanampinga ni wale tu wanaofatwa na makamera ya CNN na BBC.

Pili; ni kweli kuna matatizo ya kiuchumi na kijamii Zimbabwe lakini mleta matatizo sio Mugabe bali hayo hayo mazungu yenu!!!!

Inasikitisha kuona wengi wetu hatutaki kuona ukweli kuwa Mugabe anapigania Uhuru na Heshima ya Zimbabwe na watu wake!!! Shida iliyopo ni kuwa mapambano hayo ni dhidi ya ubeberu uliokomaa na hivyo unasababisha madhira makuwa kwa nchi na raia wake.

Kwa kizazi hiki kilicholishwa propaganda za ukoloni mamboleo, chaweza kuona Mugabe ni muovu, lakini kwetu sisi wa fifties, Mugabe ni ishara ya mpiganaji halisi wa Afrika.

Vita ya Mugabe na hao mashetani haikuanza leo! Hao BBC na CNN walikuwa wapi wakati Jongwe likiwika kumuondoa kibaraka Smith Rhodesia???? Je hawakuona, unyama waliofanyiwa wananchi wa Zimbabwe na Mkoloni Smith???? Kwa Mugabe, na Wanaharakati wa ukombozi Afrika, hivyo vikwazo vya uchumi na madhira yake ni gharama ileile kama ilivyokuwa kupoteza roho za watu wakati ule wa mapambano ya kuleta uhuru wa kweli Rhodesia.

Wote tunajua kuwa madhira yote yanayotokea Zimbabwe leo, ni zao la vikwazo vya kiuchumi ambavyo Zimbabwe imewekewa kwakuwa tu Mugabe kachukua sehemu ya ardhi yenye rutuba iliyokuwa inamilikiwa na Wazungu na kugawia waswahili ambao hawakuwa na hata sehemu ya kulimia tembele!!! Kwa hayo mazungu, ni bora waafrika wafe kwa njaa/kipindupindu ili muradi wazungu warudishiwe ardhi yao ili watoto wao wacheze na farasi ktk mashamba hayo ambayo kutokana na ukubwa wake mengine hata hayakuwa yanalimwa!!! Hivi nani amewaroga nyie??? Vipi tuone ushauri wa watu hao kuwa ni wa kibinadamu???

Kama kweli wana JF mnaona suluhisho la kutatua tatizo linaloikabili nchi ya zimbabwe ni kumtimua Comrade, basi acheni kupigia kelele unyonyaji unaofanywa na makampuni ya Migodi ya madini hapa bongo. Kwa taarifa yenu hata hao kina Anglo gold/Barick wakitimuliwa yale ya zimbabwe yatatokea hapa pia!!!! Wote ni haohao tu!!!!!!!

Swala la msingi kwa Mwenyekiti wa AU na mataifa yote ya Afrika ni kuangalia jinsi ya kuisadia Zimbabwe dhidi ya ubeberu wa nchi za magharibi. Afrika iwe kitu kimoja, kutetea uhuru wake. Kwa hilo tutashinda kama walivyoshinda kina Nyerere miaka ya sitini walipokuwa wanapambana na mababu wa hao mabeberu wa sasa!!! Kauli za kina Odinga ni za kibaraka na ni za kupingwa wala si kushabikiwa!!!

Kwangu mimi, alichofanya Odinga ni kuuza sura tu kwa wazungu ili apate support yao kuwa Rais wa Kenya. Ni ulevi tu!!!!!!

Wa kumuondoa Mugabe madarakani ni Wazimbabwe wenyewe na wala si ma-wakala wa ubeberu!!!!!

WAAFRIKA TUSIKUBALI KUUZA UHURU WETU KWA SABABU YA KUOGOPA KUTENGWA KIUCHUMI NA MABEBERU.
 
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, maarufu kama AU, Bwana Jakaya Mrisho Kikwete, naomba utege sikio umsikilize Mchungaji.

Najua nimekuwa nikiongelea sana kuhusu mambo ya ndani ya nchi yetu na kukutaka usimame kidete kusafisha uozo ulioleta Ufisadi, Uzemba na Uhujumu. Naam nashukuru kwa taratibu umeeanza kazi.

Lakini safari hii Bwana Muungwana, Mchungaji anaongelea nafasi yako kama Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Kiafrika.

Naomba utumie utashi wako kutatua matatizo ya Afrika bila kumuonea haya mtu!

Ulimtumia Membe kutoa tamko kuhusu Sudan, wakati jirani wa Kenya walipopata msukosuko wakati wa uchaguzi, sauti yako haikusikika. Ukasaidia Serikali ya Comoro iondokane na ugaidi.

Lakini kuna mambo ambayo yanahitaji sauti yako ya ukali na uongozi mahiri ukitumia uzoefu wako katika masuala ya mambo ya nje na kimataifa.

Nakuomba wakati unamalizia muda wako kama Mwenyekiti wa AU, utuletee ufumbuzi Zimbabwe ambako ukatili wa ndugu yetu wa awali wa mapambano, Robert Gabriel Mugabe unatishia si uhai wa Raia wasio na makosa pekee, bali ni hatari kwa usalama wetu kusini mwa Afrika.

Aidha inabidi uwakalishe chini kina Museveni na Kagame na waambie waache kumsaidia Jenerali Nkunda ambaye analeta vurugu Kongo.

Na mwisho, sauti yako inahitajika ma kwa kupeleka Jeshi lakulinda Amani au kuunda kamati ya usuluhishi ili kuleta Amani na kuwepo kwa Serikali katika Jamhuri ya Somalia.

Raila Odinga katoa kauli ambayo inaonyesha ujasiri kwa kutaka Mugabe awajibishwe, swali langu kwako je uko tayari kusimamia haki za binadamu na demokrasia Afrika kwa kumshurtisha Mugabe aachane na ubabe wake

Je uko tayai kuwakalisha chini zile koo pale Mogadishu ambazo sasa zinatambaa Bahari ya Hindi kuteka meli ili Somalia iwe na Serikali?

Je kule Afrika Magharibi anzia Nigeria, Sierra Leone na kwingine utulivu tunaounona ni wa kweli au ni mazugazuga?

Nakuomba basi uchukue hatua kubwa katika uenyekiti wako kuhakikisha unahamasisha uwajibikaji wa viongozi, kuimarika kwa Demokrasia na Kulinda haki za Binadamu ikiwa ni ziada ya cvita ya kutetea maslahi ya kiuchumi ya Afrika.

Ni hayo tuu Ndugu Mwenyekiti.

Amani iwe kwako Rev. Kishoka:

Katika posti naomba nikupinge. Kwa sasa nchi nyingi za kiafrika zinakaribia kufikisha miaka 50 toka zipate uhuru wake. Projects mbili kubwa na ambazo zimetumia rasimali za waafrika kwa kiwango cha juu sana ni fikra za viongozi wa juu kuwa mawazo yao ni sahihi na wanatumia rasimali za nchi kulinda itikadi hizo au kuwanyamazisha wenye mawazo tofauti. Mradi mwingine ni huu wa Afrika kubwa.

Kwa maoni yangu, vitu hivyo vimeshafanyiwa kazi na wakina Nyerere, Nkrumaha, Kaunda na wengine na juhudi zao zimeishia kugonga ukuta. Kwa maana nyingine mfupa alioshindwa fisi, sijuhi kama JK ataweza.

Wakati umefika wa kujaribu something new. Tanganyika wakati inapata uhuru ilikuwa na wakazi kati ya 11-12 Milioni na robo tatu ya aridhi ilikuwa ardhi isiyotumika. Kwa sasa idadi imeongezeka kufika 40 Milioni. Na migogoro ya ardhi kati ya jamii za wafugaji na wakulima inajitokeza. Hii ni migogoro iliyopo Darfur. Na migogoro ilyopo Nigeria ingawaje ina sura za kidini, lakini ni ya resource kati ya wafugaji, wengi wao wakiwa ni waislamu wa makabila ya kaskazini, na wakulima, ambao wengi wao waKristu wa makabila ya kusini.

Kuna uwezekano mkubwa sana, kutokana na uchunguzi ninaofanya, kuwa amani inayotajwa sana na viongozi wa Tanzania sio matokeo ya siasa zao, bali neema ya maliasili zilizopo ndani ya nchi zilizoweza kusaidia jamii mbalimbali kukidhi mahitaji yao bila ya kugombana na jamii zingine.

Mfano wa wakazi wa Mara kuvamia mgodi wa dhahabu na mapigano kati ya wafugaji wa kimasai na wakulima wa Morogoro unaonyesha kuwa matumizi ya mali ya asili kuwatuliza wananchi umefika kikomo na mbinu mpya ni lazima zitafutwe.

Sasa haya ni mapendekezo yangu. Tanzania ni lazima ijitoe katika maisha ya kijima kwa haraka sana ili iwe mfano kwa mataifa mengine. Kwa mfano jamii za kifugaji ni lazima zifanye mapinduzi katika maisha yao kwa haraka sana kwa sababu ardhi aiongezeki. Jamii za wakulima ni lazima zifanye mapinduzi kwa sababu kutegemea kilimo cha kijikimu hakusadiii maendeleo ya nchi.

Haitasaidia kwa kiongozi wa Tanzania kutafuta amani kwa wakazi wa bara la Afrika bila kuonyesha juhudi au model ya maisha ya wakazi wa Tanzania. Model yetu ya kuwachanganya watu wa kutoka mikoa mbalimbali mashuleni na makazi haina wasikilizaji barani Afrika. Watu wanaopigana kwa ajili ya resources, wanatakiwa watafutiwe model ya kuonyesha kuwa wanaweza kuishi kwa amani kwa kutumia resources walizonazo bila kutamani za wengine. Na hiki ni kitu waafrika wengi bado hatujakipa umakini.
 
Back
Top Bottom