Ndugu Lissu, ukitaka kurejea nchini rejea; usiweke masharti haina maana

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,839
Habarini za jioni,

Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara kadhaa nimeona katika mitandao Ndugu yetu,kaka yetu Lissu akizungumza kuwa atarudi Tanzania endapo jambo fulani na fulani litafanyika.

Hii sio sawa kwa sababu zifuatazo:

Kusema kuwa mukitaka nirudi basi mufanye kadhaa wa kadhaa hii ni kauli jnayotakiwa kuitoa na tena kumtolea mtu ambae amekutaka urudi.

Bwana Lissu sidhani kama kuna ambae kakuomba urudi tanzania mpaka inafika hatua unaweka masharti,

Watu wanajiuliza nani ambaye kakutaka urudi mpaka unaweka masharti hayo?

Nikukumbushe tu kuwa mwaka 2017 ipopigwa risasi uliondoka kwenda kwenye matibabu na baadae ukarudi.

Hapa kwenye kurudi nina maswali kwako.

1. Wakati unarudi Tanzania kutoka kwenye matibabu uliweka masharti yeyote ambayo yalitimizwa mpakka ukashawishika kurudi kama unavyoweka sasa masharti ?

2. Ulikuja ukafanya uchaguzi japokuwa kimagumashi na kero za hapa na pale, lakini je ulinzi ulioupata wakati wa uchaguzi kwa nini usikushawishi wewe kurudi tanzania kukaa wakati huu ambao sio wa uchaguzi?

Kwa nini haukuwa na masharti yeyote ulipotska kurudi tanzania wakati ule wa uchaguzi badala yake masharti haya unayaweka sasa hivi katika wakati huu ambao sio wa uchaguzi?

Pengine ukasema "uliruhusiwa na daktari wako kurudi Tanzania"

Sawa, kwanini hiyo ruhusa ya daktari kuhusu wewe kurudi Tanzania isiwe na masharti ukizingatia pale ndo ilikuwa wakati wa mwanzo kurudi tanzania baada ya kupigwa risasi hivyo ilikuwa uwe na hofu zaidi kuhusu usalama wako?

Lakini pia ukisema ulirudi kwa ruhusa ya daktari sasa hivi tunauliza ile ruhusa ya daktari haiendelei mpaka hivi leo au imekoma baada ya uchaguzi hivyo kakutaka usirudi tena Tanzania baada ya uchaguzi ?

Almuhimu ni kuwa daktari alikupa ruhusa kwamba ikiwa utataka kutoka unaweza lakini haikuwa lazima kwako kurudi Tanzania.

Lakini pia katika kauli zako iwahi kusema hivi

"Nataka nielezwe waliotaka kuniua ni kina nani na nikirudi Tanzania nitakuwa salama kiasi gani."

Kwanini hukutaka kufuatilia mambo haya wakati uliporudi Tanzania kwenye uchaguzi?

Ukisma kuwa ulikuwa bize na uchaguzi maana yake unatuambia kuwa uliweza kufuatilia na kufanya harakati za uchaguzi lakini wakati huo huo ukashindwa kufuatilia madai yako haya.

Lakini ukisema ulifuatilia tunaomba ushahidi wa hatua zote ulizofanya kama kweli ulifuatilia na mpaka ilipofikia.

Na ukisema kuwa ulifanyiwa zengwe na ukanyimwa fursa ya kufuatilia mambo yako kwa nini usirudi huko nje badala yake ukaendelea kupambana na uchaguzi?

Ukisema kuwa ulibaki kwa sababu ya uchaguzi na taratibu zilishapita hivyo haikuwa busara kuacha uchaguzi naomba nniulize.

Je, ulikuwa na imani utashida uchaguzi chini ya tume hii ambayo sio huru?

Kama uliamini utashinda basi hakuna haja ya kuwa na tume huru inayodaiwa.

Na kama uliamini hautashinda basi haina haja ya kusingizia uchaguzi kwa sababu matokeo yake uliyajua tokea mwanzo.

Lakini pia katika maneno yako ulisema kuwa

Kwani uliporudi ukaja kwenye uchaguzi mpaka unaisha ulikuwa salama kiasi gani mpaka ile hi ya kupigwa risasi haikujirejea tena?

Unaamini ulipewa ulinzi mzuri kiasi kwamba hukupigwa risasi ama unaamini ni Mungu alikulinda tu?

Kama ni Mungu tu alikulinda basi rudi Tz Mungu huyo huyo atakulinda mpaka ukirudi.

Na kama ni ulinzi,basi ulinzi huo huo upo hadi hivi leo.

Usiseme kuwa unataka ulinzi kama ule wa uchaguzi haiwezekani kwa sababu wagombea wote mpaka hivi sasa hawana mlinzi yeyote anayewalinda hivyo sio kwako tu.

Haya na mengine mengi nimeona niyaweke hapa ili tujadili na wanajukwaa mwisho wa yote....

Naomba Mungu awadhihirishe na wahukumiwe wote waliothubutu kukupiga risasi pale dodoma,ni ukatili unaopaswa kupigwa vita bila kutizama itikadi za kisiasa.
 
Atakuwa ana yake anayoyajua usimpangie cha kusema!
 
Nami najiuliza kwani amelazimishwa kurudi? Naelewa alipitia kipindi kigumu, kama anaona hayuko safe asirudi. But seriously anahitaji kupumzika hizi siasa, arefresh kwanza
 
Swali moja la msingi ni je,kuna mtu kamtaka Lissu kurudi nchini hadi atupangie masharti ya kutimiza ili arudi?yeye akitaka arud au aendelee kula ugali wa bure huko we dont care after all Tanzania ni kubwa kuliko mtu yeyote na itaendelea kuwepo safe n sound with his absence Lissu kwani umeitwa baba?
 
Back
Top Bottom