Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 116,476
- 215,295
Hakuna mtu yeyote anayeishi kwa uongo ambaye anaweza kupambana na Lissu ( unajua kwa nini nimetaja uongo ) na hili nimeona nikutahadharishe mapema usije ukasema umeviziwa , Tundu Lissu The Greatest , kama vijana wa Tanzania wanavyomwita siku hizi si mtu wa mchezo , huyu sasa ni International figure , Mataifa makubwa hayawezi kumkubali mtu kama huyu kijinga tu hivi hivi , unapaswa kuwa makini na maapizo yako , vinginevyo utapandisha kisukari na kuishia kupalaraizi na kupoteza fahamu .
Njia pekee ya kupambana na Lissu ni kuongea ukweli , jambo ambalo wewe mwenyewe na aliyekuteua hamliwezi wala hamtawahi hata kuthubutu , Kumwangusha Lissu unapaswa uwataje kwa majina yote matatu waliomshambulia mchana kweupe bungeni Dodoma , uwataje na waliowatuma , utaje na waliowaondoa walinzi siku ya shambulio , jambo hili hutaliweza hadi unaingia kaburini , kifupi ni kwamba umefeli kabla hata hujaanza , ni vema kabla ya kudandia ya Lissu ungewaambia wananchi yalikoishia makinikia yaliyokamatwa bandarini , ni vema ukiweka wazi ulikookota muswada kandamizi wa vyama vya siasa , muswada ambao hakuna mtu yeyote mwenye maono awezaye kuukubali .
Ni lazima pia utuambie kama Kabudi wa Tume ya Warioba na Kabudi huyu anayetokwa povu kama wana uhusiano wowote , vinginevyo utaingia kwenye kundi la wachumia tumbo walio tayari kudhalilika kwa ajiri ya njaa ya siku chache , Namshukuru Mungu kwa kukuzuia kuwa mwalimu wa wanangu .
.........Itaendelea .....