Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sabi Sanda, Aug 2, 2010.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1. Leo (02/08/2010) umechukua fomu ya kugombea Urais mwaka huu. Ni nini hasa unataka kuifanyia nchi yetu ambacho umeshindwa kukifanya toka Mwaka 2006?

  2. Katika zile fedha za EPA, je kampuni ya KAGODA imesharudisha shilingi ngapi mpaka sasa?

  3. Ni kweli kuwa gharama za kujenga kilomita moja ya barabara ya lami ni zaidi ya shilingi bilioni moja za kitanzania?

  3. Tatizo la nchi yetu kwa upande wa barabara si ukosefu wa barabara za lami bali ni ukosefu wa barabara zinazopitika mwaka mzima bila kujali kama ni za lami au laa.

  4. Ni lini utatembelea vyuo vyetu vya ualimu hasa vinavyofundisha Walimu wa masomo ya Sayansi na kujionea hali halisi?

  5. Kutokana na ombi ulilolitoa kwa Serikali ya Marekani kwa ajili ya kupatiwa Walimu wa Sayansi, je ni Walimu wangapi wamepatikana toka nchi hiyo mpaka sasa?

  6. Ni lini hasa utaweka hadharani majina ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya hapa nchini na kuchukua hatua zinazopasa?

  7. Unaonaje kama ukaamua kutogombea mwaka huu ili Watanzania tukukumbuke milele? Tunaomba sana uige mfano wa Mzee MADIBA.   
Loading...