NDUGU HAJI MANARA ,KUKOSOLEWA SIO CHUKI NA KUSIFIWA SIO UPENDO

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
13,979
11,816
Wachambuzi wa masuala ya kimichezo duniani kote wameajiriwa na vyombo mbalimbali ili kutoa maoni juu ya matukio ya kimichezo yanayoendelea, aidha katika mechi au katika matukio ya kiuwekezaji na usajili.

Kazi yao ni maoni, uchambuzi ni kutoa maoni tu. . Wapi unakwama Haji Sunday Manara, Nani amekwambia maoni yakiwa tofauti na unavyofikiri wewe ni CHUKI.? Nani kakwambia maoni yakifanana na unavyofikiri ni UPENDO.?

Unahangaika sana na watu wanaotoa maoni na kuamini mitazamo yao, kimsingi sio dhambi wao kuamini wanachokiamini. . Kazi yako imegeuka kutengeneza sumu ya Chuki baina ya mashabiki wa Yanga na baadhi ya wachambuzi eti kisa hao wachambuzi sio wale wanaosifia kila kitu, sababu sio wale wanayumbishwa na MIKWARA yako na sababu sio wale wanaoyumbisha ukweli ili kupata lolote. .

Umejenga Sumu mbaya ya Chuki kwa mashabiki wa Yanga kwa wale watu wanaotoa maoni yao tofauti eti unalazimisha ionekane wanawachukia Yanga na maendeleo yao. Unataka kuishi kwenye dunia gani ya watu wafanane mawazo na nyie ili wasionekane wana chuki..? Hakuna maisha ya hivyo. .

HII NCHI HAITENGENEZI WATU WA HOVYO kama usemavyo, haizalishi wapumbavu, bali nchi hii inazalisha watu wenye mawazo mbadala ambao wewe mwenye matatizo ya kuelewa unaona wana Chuki. Tanzania nzima ni wewe pekee ndiye unaamini watu wakitoa maoni wana chuki. Haiwezekani.

Ifike kipindi uelewe tu, sio watu wote wanaweza kuishi kama wewe kwa kusifia sifia, kuna watu wamezaliwa kuamini mitazamo yao na kuamini katika ukweli wanaousemea hata kama ni mchungu kwa baadhi ya watu. Kaa kwenye kioo jitazame kisha Tazama nyuma, umewahi kugombana na wachambuzi wote eti wanachukia Taasisi unazofanyia kazi.

Ufike wakati ubora wa kazi yako uongee kuliko hizi POROJO zako za CHUKI. Ni nani anaweza kuwachukia mashabiki wote wa Yanga.? Ni nani mwenye chuki kiasi hiki..? Ni hawa Yanga unaosema wanachukiwa na wachambuzi uliwahi kusema HAWANA AKILI kasoro Baba yako na Mzee Kikwete.

Leo wanakupa KULA. . Ukishindwa kukua basi usituharibie mchezo wetu wa kiungwana. Sisi tunabishana vijiweni kila kukicha lakini hatujengi Chuki.

NB End Of An Era

. #FootballEconomy #Branding

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Katika wote unaowaita wachambuzi muondoe JEMADARI SAID. Neno CHUKI kwake ni sahihi, huwezi kuwa mchambuzi ambaye kwako hakuna jema linalofanywa na timu Fulani. Wengine endelea kuwatetea maana Manara Ana madhaifu mengi anayotakiwa kusahihisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom