Ndugu Askofu Malasusa unataka kufanya kweli ama ni changa la macho hili ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Vita dhidi ya rushwa unafiki mtupu - Askofu

2007-12-25 11:14:34
Na Simon Mhina

Vita dhidi ya rushwa na ufisadi itaendelea kuwa ngumu, kwa vile wengi wanaodai kuipiga vita ni wanafiki na ndio hao hao wanaoidhoofisha.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, alipokuwa akitoa salamu za Krismasi na mwaka mpya kwa Watanzania, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema inashangaza kuona kila kiongozi na kila mwananchi anahubiri kupiga vita rushwa na ufisadi, lakini siku zinavyozidi kwenda ndivyo rushwa za kila namna zinavyozidi kukua na kujichimbia katika jamii yetu.

``Mimi nashangaa sana, kwani kila mtu anadai kupiga vita rushwa, kila kiongozi anaposimama anakemea rushwa na kudai kuchukizwa nayo.

Hivi sasa ukitembelea ofisi nyingi utakuta mabango mengi ya kupinga rushwa. Sasa kama ni hivyo, hao wanaotoa na kupokea rushwa ni kina nani? Mbona kila mtu anadai hahusiki?`` Alihoji kiongozi huyo.

Askofu Malasusa alisema kutokana na rushwa kukua siku hadi siku, huku watu wengi wakidai kupambana nayo ni ishara tosha kwamba kuna unafiki wa wazi katika vita hiyo.

Alisema katika vita yo yote hakuna kitu kibaya kama unafiki, kwa vile matokeo yake ni usaliti.

Alisema serikali haina budi kuchukua hatua za haraka ili kuwabaini wanafiki katika vita dhidi ya rushwa, vinginevyo juhudi zote zitakuwa bure.

``Kama mko pamoja kwenye vita, halafu mwenzenu, anaenda kinyume nanyi, itakuwa vigumu kushinda vita hiyo, hilo ndilo linalotokea kwenye rushwa, inakuwa vita ngumu kwa vile wapiganaji wenzetu wengi wao ni wala rushwa,`` alisema.

Askofu Malasusa aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa amani na kujiepusha na vitendo vya uhalibifu, kama ulevi na magomvi.

Alisema Kristo ambaye amezaliwa siku ya Krismasi, lengo la siku hiyo ni amani, maelewano na upendo.

Alisema katika kipindi cha mwaka ujao, KKKT itaendelea kushirikiana na serikali, katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema kanisa litaendelea kujikita katika kuendeleza huduma za jamii, kama shule na afya.

``Tunafanya hivi kwa vile mahitaji ya jamii ndiyo yale yale mahitaji ya kanisa. Kanisa halina watu wake wa pekee, bali watu wanaounda KKKT ni wale wale wanaoishi katika jamii yetu,`` alisema.

Katika hatua nyingine Askofu Malasusa aliwataka Watanzania kutumia kipindi cha Krismasi, kuombea uchaguzi mkuu wa Kenya.

Alisema Kenya ni nchi jirani na yenye changamoto nyingi za kisiasa, hivyo ni vema ikiombewa.

Alisema Watanzania hawawezi kuepuka matatizo ya ghasia iwapo yatatokea nchini humo.
SOURCE: Nipashe
 
Nimjuavyo Malasusa, huenda anataka fanya kweli..
Kwani ukifatilia hotuba zake tangu ashike madaraka haya, amekuwa siku zote akiiita spade a spade not...
 
asante kwa post hii, NINGEPENDA KUONGEZA KUWA RUSHWA IMESHAMIRI KUTOKANA NA MABADILIKO YA KIITIKADI,WAKATI WA MWL. NYERERE NA SIASA ZA UJAMAA RUSHWA ILIKUWEPO LAKINI ILIKUWA SIYO YA KUTISHA KAMA ILIVYO SASA.KWA UJUMLA WATU WENGI WALIUKUBALI UJAMAA NA KUAMINI MALI ZA MSINGI NI MALI ZA UMMA. LAKINI BAAD YA WAJANJA KUFANIKIWA kubadili ITIKADI KWA KIZINGINZIO cha globelazatin and free market,ubinadamu umetoweka bali sasa ni fedha.LAKINI FEDHA HUPATIKANA KWA KUFANYA KAZI SI KWA NJIA YA RUSHWA.ILI KUKOMESHA RUSHWA, VIONGOZI WAWE WA KWANZA KUJITAZAMA MAISHA YAO KISHA WAWATAZAME WANANCHI VIJIJINI NDIPO WATAKAPOJUA UBAYA WA RUSHWA.IWAPO HAWATABADILIKA HISTORIA ITAWABADILISHA
 
Back
Top Bottom